MKULIMA SMART INITIATIVES ni kampuni binafsi iliyoanzishwa na Ndugu Engineer Honoratus Salvatory. Ambaye ndiye mkurugenzi mtendaji.
DIRA: Kuona kila mtanzania akipata chakula cha kutosha,salama na chenye viini lishe muhimu.
MOTO: KILIMO MIFUGO NI BIASHARA
Malengo:
1. Kutoa taarifa muhimu za chakula kama vile bei za vyakula masokoni,hali ya hewa n.k
2.Kutoa mafunzo kwa njia ya semina,kozi fupi,makongamano,warsha na mashamba darasa
3.Kutoa huduma ya ushauri na ugani kwa wakulima,wafugaji na watanzania wote kwa ujumla ili kuzalisha chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
4.Kusimika miundo mbinu mbalimbali ya kilimo na ufugaji kwa ajili ya mashamba darasa.
Ili kufikia malengo hayo njia zifuatazo zitatumika:-
Kutumia TEHAMA/ICT kama kifaa muhimu cha kupeleka tahaarifa kwa walengwa kama vile:-
1.Mitandao ya kijamii facebook,KZbin,whatsup n.k
2.Radio za kijamii na televisheni
3.Tovuti
4.Majarida na vijitabu.
Call/Whatup +255 713 178 868
Email:
[email protected]Website