163-Anakuja, Bwana Yesu It May Be At Morn (SDAH207) Doh ni D Pengine ni saa ya kupambazuka, Mishale ya jua ipenyapo giza, Kwamba atakuja Yesu mtukufu, Awapokee wake. CHORUS Bwana itakuwa lini Tutakapoimba, "Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin, Aleluya, Amin?" Pengine mchana, pengine jioni, Pengine usiku wa manane, giza Itatoweka kwa fahari akija, Awapokee wake. Majeshi yake yataimba 'hosana', Na watakatifu waliotukuzwa Watamsifu kwa kuwa amekuja Awapokee wake. Furaha tukiitwa pasipo kufa, Pasipo kuona maradhi, machozi; Kuchukuliwa winguni kwa fahari Akija kwa watu wake.