Рет қаралды 1,642
Mkurugenzi wa kampuni ya IMARA TECH Alfred Chengula inayojihusisha na shughuli za uzalishaji wa mashine za kilimo jijini Arusha ameeleza kuwa kampuni yake imeweza kubuni mashine yenye uwezo wa kupura na kupeta mazao aina tisa (9) tofauti kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo ambayo imepata umaarufu mkubwa sana na kuweza kuwafikia zaidi ya wakulima mia nne (400) na kuuzwa Nchi za nje kama vile; Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Zimbabwe na Malawi.
Alfred ameongeza kuwa, Mashine hiyo inaenda kuongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa na kuongeza ajira kwa Watanzania hususani bodaboda ambaomashine hii inauwezo wa kubebwa kwenye pikipiki hivyo ameomba msaada kwa Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuendelea kutoa ushirikiano ili kuahakikisha mazingira ya uzajilishaji yanakuwa rafiki.