BREAKING: MWAKYEMBE AAGIZA DUDU BAYA AKAMATWE "NI MPUUZI"

  Рет қаралды 30,180

Global TV  Online

Global TV Online

Күн бұрын

BREAKING: MWAKYEMBE AAGIZA DUDU BAYA AKAMATWE "NI MPUUZI"
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amelielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua Msanii Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ kwa kumdhihaki aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba ambaye alifariki jana nchini Afrika Kusini.
Aidha, Dudu Baya amemjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure, badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.
“Nipo nyumbani, Mheshimiwa Mwakyembe umeagiza polisi kunitafuta, usisumbue difenda kumaliza mafuta, bora wakakamte majambazi, niambie polisi waniite kituo gani, nipo tayari kufika hapo,” amesema Dudu Baya.
Hata hivyo, Watanzania wengi ambao kwa sasa wapo kwenye majonzi mazito, wamechukizwa na kitendo cha Dudu Baya kumdhihaki Ruge tena hadharani kwenye mitandao ya kijamii ilihali hatupo naye tena badala ya kumuombea apumzike kwa amani.
Pia, wamedai kupitia mitandao ya kijamii amekuwa akitumia maneno kwa kuandika, kujirekodi video na kuzisambaza kumshashifu Ruge huku akimtaja Mwenyezi Mungu kinyume na matendo ambayo anayafanya.
www.youtube.co.... Watch More Videos here: goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook:
globalpublishers Instagram: globalpublishers Twitter: GlobalHabari Install Global App: ANDROID: goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: goo.gl/2jDyho

Пікірлер: 125
@ngianasiakisamo9557
@ngianasiakisamo9557 5 жыл бұрын
Asante Mheshimiwa mimi mwenyeye nimeumia sana kwa maneno ya kejeli ya msanii huyu
@jamesoduororawo8379
@jamesoduororawo8379 5 жыл бұрын
Criticism is there even in the USA...if Tanzania is a democratic Nation then there should be freedom of expression . Dudu Baya just expressed his views.. Government of Tanzania needs to address serious threats like un employment, corruption,gold being smuggled out of the country, infrastructure and building hospitals and schools. Let's celebrate our heroes when still alive, appreciate them and honour them...we all no the founder of Bongo records is P Funk Majani he come up with the brand.we no sugu started music when it was only Tbc on the air waves..Let's champion for economic freedom in Africa..God bless Tanzania,God bless East Africa,God bless Africa,God bless the World.
@hilarymungure8590
@hilarymungure8590 5 жыл бұрын
Watanzaniaa ni zero
@lubavaclassic7048
@lubavaclassic7048 5 жыл бұрын
Correct friend
@salhatyswai679
@salhatyswai679 5 жыл бұрын
Asante mzee wetu mwakyembe
@salehsalhamselem3285
@salehsalhamselem3285 5 жыл бұрын
Munge mchukulia amber Ruth nandi na machupi yake na yule alie kwenda na bunduki clouds na askari mbona uliu fyata mzee ukifa utasifiwa mazuri yako na yeye katoa mabaya yake konki konki gonga like
@f.a6043
@f.a6043 5 жыл бұрын
Kweli kabisa Mh. Waziri uko sahihi kabisa!
@zuberimgawilo2639
@zuberimgawilo2639 5 жыл бұрын
Safi sana mwakiyembe. Amezidi kumdhalilisha boss ruge
@badmanno.1650
@badmanno.1650 5 жыл бұрын
Dudu baya hana kosa kisheria..labda mumkandamize tu..ila alivofanya sio ubinadamu lakini pia sio makosa ...
@young_wizzjimmy6296
@young_wizzjimmy6296 5 жыл бұрын
w4k1- 70wn hujui lolote bora unyamazeeee
@ototek8037
@ototek8037 5 жыл бұрын
young_wizz jimmy ni kweli kwani kikatiba yupo sawa.. Kibinadadam kakosea. Kama ndugu yetu kuongelea ughaibuni wakati anakwao.. Yupo sawa kikatiba lakini kiuzalendo kakosea! Ni makosa y kibnadam2 Mungu ndo anayejua kwann dudu bay pepo kamchukua
@young_wizzjimmy6296
@young_wizzjimmy6296 5 жыл бұрын
bro unajua maana ya penal code???
@young_wizzjimmy6296
@young_wizzjimmy6296 5 жыл бұрын
katika rugha zake hakuna matusi na kejeli? au hujui kejeli na matusi ni kosa la jinai????
@wolvespack3255
@wolvespack3255 5 жыл бұрын
Freedom of speech 🏃‍♂️
@blasiusmwnje359
@blasiusmwnje359 5 жыл бұрын
wolves pack ndo hayo mnavyopotosha jamii,huyu katukana sasa Aachewe eti kwa sababu ya freedom of speech?
@khamisali5444
@khamisali5444 5 жыл бұрын
Safi sana mkuu
@rajabshaban4985
@rajabshaban4985 5 жыл бұрын
safi sana Baba tena mumfunge maisha
@hamidajuma7804
@hamidajuma7804 5 жыл бұрын
safi sana baba msweke ndani hana hakili huyu jama kabisa
@samwelmunish4500
@samwelmunish4500 5 жыл бұрын
Nimeipenda hiyo
@maryamm7765
@maryamm7765 5 жыл бұрын
Safi sana atiwe akili kidogo
@chrisantushokororo8450
@chrisantushokororo8450 5 жыл бұрын
Mtumie sheria inavyotaka
@faridalundenga8696
@faridalundenga8696 5 жыл бұрын
Asante
@Rogathe-Rogathe
@Rogathe-Rogathe 5 жыл бұрын
Mungu akubariki muheshima Dr. Harrison Mwakyembe kwa hilo..
@samwel.matemu957
@samwel.matemu957 5 жыл бұрын
Anyongwe shetani huyo
@omarmussa5755
@omarmussa5755 5 жыл бұрын
Asante Muheshimiwa.
@assengajoseph8825
@assengajoseph8825 5 жыл бұрын
Me nadhan muelimisheni tu maana kwenye kutaja watu mashoga mlimlinda kwa sbbu mlijua anasema kwel mlisahau mtoto umleavyo ndivyo akuanvyo so wajibeken
@shaabanbaiya8090
@shaabanbaiya8090 5 жыл бұрын
Kabisa. Umleavyo ndivyo akuavyo
@zakayoyohana4200
@zakayoyohana4200 5 жыл бұрын
baba tena munyonge kabis
@manjalejuniorlg7024
@manjalejuniorlg7024 5 жыл бұрын
Safi sana Mzee huyu jamaa ni mpumbavu
@mwebraniaonline7001
@mwebraniaonline7001 5 жыл бұрын
Kweli ukicheza na ubwa anakufata msikitini
@mariachombo9482
@mariachombo9482 5 жыл бұрын
Yah huo sio utaTanzania anhitaji kuonwa na sakatric dr
@jamilsalanga4193
@jamilsalanga4193 5 жыл бұрын
Kwa heri dudu baya,no one above the law,umemtukana sana marehem ruge,umemtabilia kifo,but now ur going to suffer
@njugunajessy1857
@njugunajessy1857 5 жыл бұрын
JAMIL SALANGA
@jamilsalanga4193
@jamilsalanga4193 5 жыл бұрын
nambie
@ibrahimmzee3237
@ibrahimmzee3237 5 жыл бұрын
Sukuma ndani...akakutane na makonki uko
@dicksonulotu9717
@dicksonulotu9717 5 жыл бұрын
Barikiwa Mtumishi Mhe Waziri kwa atua ulizo zichukuwa nikweli anaweza kufanyiwa kitu kibaya bora akasukumwa umo lupango na adhabu Kali iwe fundisho kwake na kwa watz wote.R.I.P Ruge Mutahaba.
@jessykaelus1579
@jessykaelus1579 5 жыл бұрын
Asante baba: kwa kuliona hilo.
@hadijalungate8981
@hadijalungate8981 5 жыл бұрын
Asante baba
@hadijalungate8981
@hadijalungate8981 5 жыл бұрын
Safi sana waziri
@lubavaclassic7048
@lubavaclassic7048 5 жыл бұрын
Akuna kitu Pumba tupuu wafwasi wa vibweteleeeee...!!
@bonnysureolkokolaboy4342
@bonnysureolkokolaboy4342 5 жыл бұрын
Dudu naona atageuzwa Gugu daaaah
@drmsouthsmalltrader1138
@drmsouthsmalltrader1138 5 жыл бұрын
Hongera mwakyembe Lau utafanya hivyo mtatutia moyo wakereketwa
@uwezomayonko371
@uwezomayonko371 5 жыл бұрын
serikali ujitahidi kutenda haki pande zote ktk sheria! pasiwepo na watu ambao wakifanya makosa wanaachwa huru ila wengine wakikosea wanashughulikiwa kama kitoweo! hii siyo haki bali inajenga chuki kubwa sana miongoni mwa Jamii.
@zulfatothman1051
@zulfatothman1051 5 жыл бұрын
Kasema mumtajie kituo gan aende km mabatini salenda ostabey au wp yule co mzm milembe 1kwa1
@aminabukenya231
@aminabukenya231 5 жыл бұрын
Gud job bila shaka hta jipanga hko chezea serekali wwe utajuta kuharisha kutumia mdomo wko
@blacknature7637
@blacknature7637 5 жыл бұрын
Asante Sana mh dudu amezidi Bora atiwe adabu mwana wa zinaa huyo dudu
@uwezomayonko371
@uwezomayonko371 5 жыл бұрын
kiukweli mm siungi mkono kauli za dudu baya zidi ya marehemu! lkn pia sheria zetu zutumike pande zote! wapo watumishi wa serikali ambao wamekuwa wakihamasisha umma tundu lisu auliwe! lkn hadi leo Hawajachukuliwa hatua yoyote???
@sharifaabdullah6825
@sharifaabdullah6825 5 жыл бұрын
Safi sana mzee mwakiyembe nikweli kabisa amefanya vibaya sana
@abezotillya9668
@abezotillya9668 5 жыл бұрын
Anasema ukwel
@kiulaleonadi1091
@kiulaleonadi1091 5 жыл бұрын
Sawa kabisa
@boomaxboomax8535
@boomaxboomax8535 5 жыл бұрын
iwe fundisho kwa wengine
@florambwambombwambo1322
@florambwambombwambo1322 5 жыл бұрын
akamatwe bila uchunguzi afungwe mbwa Huyo anafikiria serikali yababa yake kilakitu anachoongea anaona ananyamaziwa anaonasifa lifungeni kabisa
@mamachris6811
@mamachris6811 5 жыл бұрын
Dhamira yake imetimia maana inaonesha kuna biashara anafanya huko mahabusu Anatafuta kila sababu afungwa Mpuuzi mkubwa sana
@zakaliazefania1391
@zakaliazefania1391 5 жыл бұрын
NAOMBA AFUNGIWE MAISHA YAKE YOOTE KUJIUSISHA NA MAMBO YA SAANA, AMETUVUA NGUO,
@zeynabali573
@zeynabali573 5 жыл бұрын
Zakalia Zefania
@halimatanzania645
@halimatanzania645 5 жыл бұрын
Hata kama mtu amekukosea umauti umempata huwezi ukamkejeri huyo akapimwe akili hayupo sawa
@diyaosman8992
@diyaosman8992 5 жыл бұрын
Poa Mzee ubarikiwe poleni wa Tanzania.r.i.p
@abezotillya9668
@abezotillya9668 5 жыл бұрын
Dudu baya msema ukweli
@priscaphedrick1579
@priscaphedrick1579 5 жыл бұрын
Inahitajika busara upendo nauvumilivu kwa watu woote heri kupigwa kibao namwenye hekima gizani kuliko kusifiwa nampumbavu hadharani
@sethkivuyo3342
@sethkivuyo3342 5 жыл бұрын
Hii yenye viongozi wenye PHD za Unafiki kuliko Upendo wa kweli.ivi ni lazima isiwe na Mawazo ya Mkuu yawe ya Watu wote??. Nakumbuka waziri pia uliwahi kushinikiza maslay ya Mzee majuto baada ya yeye kufa. Doo kweli Ishi usakamwe Kufa Usifiwe.
@sethkivuyo3342
@sethkivuyo3342 5 жыл бұрын
Mawazo yako c mawazo yangu. Ucnifunge mdomo kuyasema ninayoamini
@manjalejuniorlg7024
@manjalejuniorlg7024 5 жыл бұрын
Huyu Dada ni wakuchotwa kusukuma ndani
@adammangula2521
@adammangula2521 5 жыл бұрын
Mpelekeni huko wakafirane ametuchosha
@giftedpowerj790
@giftedpowerj790 5 жыл бұрын
sheria inaenda na sheria na sio matamko ya MTU , tukumbuke nchi yetu ni ya kidemocracia kwa hivyo kama sheria zipo atafungwa kama hakuna basi nyie mumbeeni Mungu ALIE tangulia kwani huyo Dudu katamka maneno haja UA na mbaya zaidi katamka ki mtego hataamka kitandani , wana sheria njoni musaidie wa Tz wanazani kila jambo mkuu kasema
@mangulymanguly139
@mangulymanguly139 5 жыл бұрын
Tatizo ao tulowapa zamana ujiona wao ndo wao wao mangapi wanafanya mabaya mengi sana na cc wananchi atuna pa kukimbilia yy katoa hisia zake tu Co kosa
@classicwaisala6677
@classicwaisala6677 5 жыл бұрын
Sio Tanzania basi tui ite Marekani sasa; Tanzania enyewe ni inchi yakidemocrasia sasa mtu anatoa isiya zake hataki awe mnafiki anaongea ukweli wake.. Muacheni jamaa afu wwe Makiembe wacha u dicteta
@mangulymanguly139
@mangulymanguly139 5 жыл бұрын
Ao ndo viongozi wa kiafrica wanayo fanya wao wanajiona wako sahihi izo ni hisia zake kama mtu umpendi kwa nn usitoe yalio moyoni
@edwinkicha14
@edwinkicha14 5 жыл бұрын
huyo mbwaa akae sana mpaka ajitambue bangi zake nizake na familia yake ruge wengi tumenufaika nae sana sana
@janengowi3011
@janengowi3011 5 жыл бұрын
Sawa kabisa anamkejeli MTU ambaye ameshalala usingizi wa milele asukumwe ndani
@mkwipunda2036
@mkwipunda2036 5 жыл бұрын
Ukiona gari inatembea kuna sehemu zinapata joto karibu na kuyeyuka lakini wakat huo huo kuna sehemu zinapata baridi kali zinakaribia kuganda Huwezi kuwa mwema kwa kila mtu wala kinyume chake....
@emmanuelbonifas3517
@emmanuelbonifas3517 5 жыл бұрын
Mzee hapo ndio tujue kuwa muumba wetu ana kazi kubwa sn wote ni wakwake ila kwa mila za kwetu mtu akifa atakama kulikuwa kosa lolote bc usamehewa yote na kumuombea heri anakokwenda sio kumtukana na kukejeri kswb akuna mkamilifu
@zammaulidi7507
@zammaulidi7507 5 жыл бұрын
Ndio lakini joto jamani alicho mfanya au kuwafanyia kimewakost japo kwa wengine kikwazo apewe onyo Tu so kumuweka ndani kwani hapo hapo ndio walio fangiwa watajuwa hawana serekali wala watetezi mana mengi yanafungiwa macho baadhi wanaumia
@fadhilisaidy2444
@fadhilisaidy2444 5 жыл бұрын
Vicha kama awa Mweshimiwa sweka lumande waka weweseke uko mana ana faida kweny hi nch ata kdg
@salummkwawa4348
@salummkwawa4348 5 жыл бұрын
Konki konki konki master
@georgeheke4514
@georgeheke4514 5 жыл бұрын
Dudu baya hajaikosea selikali ila anamkosea mungu mungu ndiyo anapaswa kumpa adhabu kubwa sana
@peacelanda192
@peacelanda192 5 жыл бұрын
ruge kaniuma nimeumia nimeumiaaa nimeumiaaaaa mungu amlaze mahari pema peponi😢😢😢baba mfunge ata miaka 10 tuuu yaan simpendi mm
@azizamkindi1784
@azizamkindi1784 5 жыл бұрын
M
@snasirsaid2153
@snasirsaid2153 5 жыл бұрын
JAMANI PAKA ANAKULIA KITEWEO ALWAYS SIKU AKIULIWA AU AFE BAHATI MBAYA UNALIYA KAMA MTOTO 😭 NA SHERIA YA DINI ZOTE INA HIMIZA KUWA HUKUMU ANAYO MUNGU SIO BINADAMU LEO ASEMA HUYO KENDA LEFT DAHH PESA MBAYA KUNA WATU WAMTUMIA HUYO DUDU NA VILE ANAJIONESHA HAOGOPI BASI ATUMIWA AU MGONJWA APELEKWE HOSPITAL
@saleheramadhan5442
@saleheramadhan5442 5 жыл бұрын
Sukumani uyoooo
@rajabshaban4985
@rajabshaban4985 5 жыл бұрын
tena uko gerezani wamfile kabisa
@claralassonn8833
@claralassonn8833 5 жыл бұрын
Nilikuwa shabiki sana was dudu lakini umenichefua wewe
@lovenesslyimo763
@lovenesslyimo763 5 жыл бұрын
Afadhali akamatwe sijui ana matatizo gani tokea mwenzie mgonjwa anamwandama mpaka amefariki bado tu jamani 😥
@rahmansbsbsbs6096
@rahmansbsbsbs6096 5 жыл бұрын
Mumuweke kbs uyo sheitwani
@godfreyjoseph9422
@godfreyjoseph9422 5 жыл бұрын
Asante Mh Mwakiyembe ngoja akakutane na makonki uko ndo ataisoma namba 'SUKUMA NDANI'
@arafazakir1763
@arafazakir1763 5 жыл бұрын
Ningekuwa na uwezo ningelishia watu wote pilau nimefrai sana sana hili dudu kukamatwa na yy likafie mbele uko na uso wake mbaya km limau
@sophicatesalim9757
@sophicatesalim9757 5 жыл бұрын
ata sisi tusiomjua tumeumia jamani mbona sharia ifanye kazi yake kwa kosa gani kubwa jamani tangu yuko kitandani anaumwa anamtolea maneno mazito nakejeli paka ameondoka ulimwenguni bado tu so bad mbona akamatwe uyo mtu
@stevensemkiwa1833
@stevensemkiwa1833 5 жыл бұрын
yeye anadai Rais ni kabila lake haogopi mmemlea wenyewe wanafiki ninyi
@zeynabali573
@zeynabali573 5 жыл бұрын
sophicate Salim
@herifredrickson2040
@herifredrickson2040 5 жыл бұрын
Serikali iangalie vitu vya maana na sio kukurupuka kwani ameuwa? Acheni hizo Sio Kila marehemu asifiwe.
@mamachris6811
@mamachris6811 5 жыл бұрын
Ni mpuuzi kweli,kwani kama alidhulumiwa hakujua hatua za kupitia apate haki take ? Tatizo alivamia Dani si yake Mwenye akili akifeli jambo moja,unatafuta jingine sio kukaa unamlalamikia mtu
@farajaluvanda1242
@farajaluvanda1242 5 жыл бұрын
Sukuma ndani mpuuzi sana huyo mpumbavu kabisa
@mosesmkoma6882
@mosesmkoma6882 5 жыл бұрын
Ssfi saana akamatwe na apigwe saana viboko
@manyaramrema6531
@manyaramrema6531 5 жыл бұрын
Mhhh kwani huu msiba ni wa kitaifa??? Sio lazima kila mtu amsifie ni hisia zake tu
@mamahustru
@mamahustru 5 жыл бұрын
Ndio, sababu hakuna mtanzania mwingine wakawaida kabisa ambaye hana ofisi ya umma, aliyeweza kuwa na mchango mkubwa kwenye jamii, watu wengi mmoja mmoja hasa walio mikoani kusikokuwa na mitandao kama Ruge. Ruge aliwafungulia watu dunia, waliopata bahati ya kukutana naye. Wapo ambao walitumia fursa alizowapa vizuri kama akina Mond japo walipopata kumzidi wakasahau fadhila, na wapo walioshindwa kutumia fursa kama akina konki.
@ngianasiakisamo9557
@ngianasiakisamo9557 5 жыл бұрын
Ni wa kitaifa ndio ndo maana umewagusa watanzania wengi
@rayaalaisari4592
@rayaalaisari4592 5 жыл бұрын
Hata kama anamchukia sio hivyo Tena yeye angenyamaza tu sio kwa maneno hayo... Mwenzengu kifo nikitu kingine hata ukisikia adui yako kafa wallahi utasikitika.... Tuuu
@manyaramrema6531
@manyaramrema6531 5 жыл бұрын
@@ngianasiakisamo9557 unaposema msiba ni wa kitaifa ina maana hata shughuli za kiserikali zinasimama kitu hicho hakipo
@azizaabeid123
@azizaabeid123 5 жыл бұрын
Ndio maana hata waziri amefika msibani
@allyshen525
@allyshen525 5 жыл бұрын
uo ni unyanyasaji mbona ommy dimpoz amechafuliwa sana pindi anaumwa na haukua na neno lolote au ommy dimpoz nani
@alexjosephat9030
@alexjosephat9030 5 жыл бұрын
Huyu ni marehemu ndg yangu. Pia nafasi yake ni kubwa mno
@mkanduzmussaz2288
@mkanduzmussaz2288 5 жыл бұрын
Ukiumiza nawe utaumizwa na ndio maana tunahaswa kutenda mema kabla ya kifo chetu
@chancelinechuchu7333
@chancelinechuchu7333 5 жыл бұрын
ili dudu baya alina akili sawa litupwe jela myaka yote
@jacksonrabson6439
@jacksonrabson6439 5 жыл бұрын
Asantee,, Dudubaya alihisi watanzania wote niwanywa konyagi
@Anonymous00018
@Anonymous00018 5 жыл бұрын
Muulizeni kwanza ana machungu gani, kwani kafanya kosa gani? Wacheni upuuzi huo. Mnajuwa kufanyiwa nn hata akasema anayoyasema? Are u going to do this for everyone else or just him? Anyway, as long as mnafata sheria then it's ok. Watu wangapi wametukanwa na kukashifiwa, what have u done? Kumbe likiwauma mna-react? Konki konki konki 🔥🔥🔥 anatowa dukuduku lake, guide him the right way to do it, sio mumkataze his "right of speech". Anatukanwa trump rais wa dunia na hakuna alokamatwa...
@samohboy9937
@samohboy9937 5 жыл бұрын
Poor Millionaire Kwann machungu yake asinge onyesha kipindu ruge yupo hai na wewe unamuunga mkono na wew ni kuku wa mayai Huyo Dudu akamatwe tena apigwe jera au fain
@agaaah6697
@agaaah6697 5 жыл бұрын
Tatzo hawa Jamaa wanaangalia nan anaefanya kitu dimond kafanya mangp na akina wema lkn akaa mnaona kawaida mnawafungia Leo kesh mnawaamchia xx dudu mnajua kafanyiwa nn au mnaangalia upnd 1 tu wasanii wangap wnalalamika juu hyo my wenu au kwakuw kafalik ndo anaonekana mwema
@stephenherbert3221
@stephenherbert3221 5 жыл бұрын
Baba lifungeni maisha lisirudi huku uraiani linasumbua eti linajiita konki
@Anonymous00018
@Anonymous00018 5 жыл бұрын
Samoh Boy inaonesha ndio kwanza leo unasikia habari za dudubaya. Kaanza kusema tokea mwaka jana km wewe umemsikia jana na leo pole yako. Simtetei cos mengine kapitisha mipaka ya ubinaadamu ila hajavunja sheria in my point of view. Km mm kuku Wa mayai basi ww Wa nyama. Na wamkamate ila wajuwe km wanavunja sheria itakula kwao.
@mamachris6811
@mamachris6811 5 жыл бұрын
Tatizo la kulazimisha mlango wa kutokea,wakati milango ipo mingi
@luomusicchannelfromtanzani5650
@luomusicchannelfromtanzani5650 5 жыл бұрын
Yaaaniii hata kama ni hukumu ya kunyongwaa apeweee. Mh. Mwakyembe hakuna kifungu cha kumnyonga kweeliii huyuu mbwaa?
@samohboy9937
@samohboy9937 5 жыл бұрын
Tuhukumie huyo Anataka kutufanya watanzania wote hatuna akil mkuu Mtupen jera huyu mtu hato uona ufalme wa mungu Dudu asukumwe ndan hatumtak huku ulaian huyo kuku wa maziwa
EXCLUSIVE: PASHA Amerudi Tena / ASLAY Hapana / Dudu Baya Mhm!
9:14
Global TV Online
Рет қаралды 3,4 М.
TAZAMA BASHE, MPINA WALIVYOKUTANA USO KWA USO
10:18
Mwananchi Digital
Рет қаралды 20 М.
The Joker wanted to stand at the front, but unexpectedly was beaten up by Officer Rabbit
00:12
I Took a LUNCHBAR OFF A Poster 🤯 #shorts
00:17
Wian
Рет қаралды 16 МЛН
А ВЫ ЛЮБИТЕ ШКОЛУ?? #shorts
00:20
Паша Осадчий
Рет қаралды 2,8 МЛН
SENTENCING OF ACTING INSPECTOR GENERAL OF POLICE GILBERT MASENGELI
19:01
Citizen TV Kenya
Рет қаралды 41 М.
Ip Man 2 | The Boxing Competition
15:57
Cinewatch
Рет қаралды 8 МЛН
7 Signs That Someone Dislikes You and is Hiding it | STOIC PHILOSOPHY
27:50
How to win a argument
9:28
ajaxkmr
Рет қаралды 531 М.
The Joker wanted to stand at the front, but unexpectedly was beaten up by Officer Rabbit
00:12