Рет қаралды 6,743
BWANA YESU asifiwe, karibu na ahsante kwa kujumuika nasi katika ibada njema, ya kipekee ya NYUMBA KWA NYUMBA. Ibada hii ya NYUMBA KWA NYUMBA ni maalum sana inayosimamia KUTOA MAPANDIKIZO YA GIZA KWENYE KILA NYUMBA NA FAMILIA NA KURUHUSU UFALME WA MUNGU USIMAME inayokujia leo Jumapili ya 1tarehe 11 Novemba 2024 mubashara kutoka Heart of Worship Ministry HQ Mbezi Beach Dar Es Salaam.
Ibada za nyumba kwa nyumba inaongozwa na maelekezo "KUJENGA UFALME WA MUNGU NA KUBOMOA UFALME WA GIZA NYUMBA KWA NYUMBA" na neno la MUNGU kutoka kitabu cha Danieli 2:44 "Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele."
Ibada hii inaongozwa na kichwa cha somo; "MADHABAHU ZA MAUTI NA MAGONJWA FEKI ZILIZOWEKWA TAREHE HUSIKA ZINIPATE ZIVUNJWE "
Ibada hii inaongozwa na Mtumishi wa Mungu Amoke Nkonoki.