Рет қаралды 3,640
BWANA YESU asifiwe, karibu na ahsante kwa kujumuika nasi katika ibada njema, ya kipekee ya MADHABAHU YA EBEN-EZERI. MADHABAHU YA EBEN-EZERI ni madhabahu maalum sana inayosimamia masuala yote yanayohusiana na kazi na biashara za kila mtu inayokujia leo Jumapili ya tarehe 2 Februari 2025 mubashara kutoka Heart of Worship Ministry HQ Mbezi Beach Dar Es Salaam.
Madhabahu na Ibada inasimama katika neno la MUNGU kutoka kitabu cha 1 Samweli 7:12 "Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake EBEN-EZERI, akisema, hata sasa BWANA ametusaidia".
Ibada hii maalum in kichwa cha somo; "ZIDISHA KAZI ZA MIKONO YANGU NIKUTUMIKIE" na inaongozwa na mtumishi wa Mungu Amoke Nkonoki.