IJUE HISTORIA YA KISIWA CHA PATMO

  Рет қаралды 4,325

GODFREY KITOKI

GODFREY KITOKI

Күн бұрын

Patmo kilikuwa kisiwa kame na chenye miamba katika Bahari ya Aegea; kilikuwa na urefu wa maili 10 na upana wa maili sita katika eneo lake pana zaidi. Warumi walitumia kisiwa hiki pamoja na visiwa vingine jirani kama koloni la kuadhibia wahalifu wa kisiasa walioondoshwa kwenye nchi yao. Waandishi Wakristo wa awali walioishi takriban wakati wa kuandika kitabu cha Ufunuo hutamka, kwa kauli moja, kwamba mamlaka za Kirumi zilikuwa zimemfukuza Yohana kwenda uhamishoni Patmo kwa sababu ya uaminifu wake katika injili. Mtume huyu mkongwe akiwa Patmo hakika alistahimili taabu zote za kifungo cha Rumi. Pengine alitendewa ukatili kama mhalifu, akafungwa minyororo, akapewa chakula haba, na kulazimishwa kufanya kazi ngumu huku askari wa Kirumi wasio na huruma wakimpiga mijeledi.
“Patmo, kisiwa kame na chenye miamba katika Bahari ya Aegea, kilikuwa kimechaguliwa na serikali ya Rumi kama mahali pa kifungo cha uhamishoni kwa ajili ya wahalifu; lakini kwa mtumishi wa Mungu makazi haya ya kuhuzunisha yakawa lango la mbinguni. Hapa, akiwa amefungwa mbali na mandhari ya maisha yenye shughuli nyingi, na kutoka kwenye shughuli halisi za miaka ya awali, alikuwa na ushirika wa Mungu na Kristo na malaika wa mbinguni, na kutoka kwao alipokea maelekezo kwa ajili ya kanisa kwa ajili ya wakati wote ujao.”-Ellen G. White, The Acts of the Apostles, uk. 570, 571
Je, ni wahusika gani wengine wa Biblia ambao wamestahimili mateso, hata licha ya (au pengine hata kwa sababu ya) uaminifu wao kwa Mungu? Angalia Dan. 3:16-23, Mdo. 7:54-60.
Wafuasi wa Kristo hawapaswi kusahau kwamba pale wanapojikuta kwenye mazingira yafananayo na yale ya Yohana, hawajaachwa peke yao. Yesu yuleyule, aliyekuja kwa Yohana akiwa na maneno ya tumaini na faraja katikati ya dhiki ya Patmo, bado yu pamoja na watu Wake ili kuwategemeza na kuwasaidia katika hali zao ngumu.
Tunawezaje kuelewa tofauti kati ya mateso kwa ajili ya Kristo na mateso kwa ajili ya sababu zingine, ikiwa ni pamoja chaguzi zetu mbaya? Au habari gani kuteseka kwa ajili ya kile ambacho, huonekana, si sababu nzuri hata kidogo? Tunawezaje kujifunza kumtumaini Bwana katika kila hali?

Пікірлер: 2
@sofialinus8241
@sofialinus8241 3 жыл бұрын
Nzuri muendelezo tafadhali
@angelmussa8709
@angelmussa8709 Жыл бұрын
Samahn nin swali ety yohan alik Kwa muda gn ndan ya icho kisiwaa
Nastya and balloon challenge
00:23
Nastya
Рет қаралды 15 МЛН
Kimeumana: Bad news from JKIA shakes the world
10:55
Rogers Kakasungura
Рет қаралды 10 М.
Kaminula Choir - Stephano
3:33
WOKOVU MEDIA
Рет қаралды 56 М.
Ijue historia ya wimbo wa Usinipite mwokozi,
2:28
GODFREY KITOKI
Рет қаралды 912
NABII ELIYA ASHUSHA MOTO TOKA MBINGUNI
4:01
GODFREY KITOKI
Рет қаралды 15 М.
NABII DANIEL TUNDUNI MWA SIMBA
6:31
GODFREY KITOKI
Рет қаралды 659
Mnara wa Babeli-Mwanzo 11:1-9
2:38
Hadithi za Biblia
Рет қаралды 2,6 М.
ULIMWENGUNI MNAYO DHIKI JIPENI MOYO
1:14
GODFREY KITOKI
Рет қаралды 850
Nastya and balloon challenge
00:23
Nastya
Рет қаралды 15 МЛН