Рет қаралды 5,693
Yapo Maandazi ya namna mbalimbali kulingana na upishi na mpishi mwenyewe na yote ni dhahiri yanatofautiana ladha mdomoni
KAJEM TV hii leo imekuwekea namna ya kupika Maandazi ya Nazi yenye ladha na utamu Tofauti na Maandazi ya kawaida ambayo walio wengi hupendelea kupika
Maandazi haya mara nyingi hupendelewa kupikwa maeneo ya pwani kama vile, Tanga, Dar es salam, Pwani na Morogoro ambapo upatikanaji wa Nazi ni rahisi Tofauti na mikoa mingine
ni vyema ukaangalia mwanzo mpaka mwisho ili ujifunze na utanue wigo wa ujuzi katika mapishi