Рет қаралды 18,052
Shinikizo zaidi zimeendelea kumtaka waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi kujiuzulu kufuatia msimamo wake kuhusu serikali na utekaji nyara. Waziri wa mazingira Aden Duale na baadhi ya viongozi wa UDA wakisema matamshi ya waziri Muturi yanadunisha serikali anayotumikia. Matamshi haya yanajiri siku moja baada ya waziri Muturi hapo jana aliendeleza shutuma zake, akimtaka Rais William Ruto kukomesha visa vya utekaji nyara