Рет қаралды 23,547
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 62 huko kisii amezua gumzo mtaani kutokana na kazi yake ya uendeshaji bodaboda. Licha ya umri na jinsia yake, ajua huyo anajitafutia tonge la siku kupitia kazi ya bodaboda akishikilia kuwa ana nguvu na ustadi wa kufanya kazi hiyo. Na kama anavyoarifu Chrispine Otieno, mojawapo ya masharti yake ni wateja wake kutomshika kiunoni anapowabeba kama inavyofanyika kwa kawaida.