Jameni mnisaidie kupata wimbo wa zamani, huenda ni wa Marehemu Aziz Abdi. Ulikuwa na maneneo: "Nakuambia mbele ya Mungu mama, ndiye ajuaye Mola wangu mama... Siku ya kwanza tulipendana mimi na wewe, hakuna mwingine... Hivi sasa mapenzi yamekwisha..." Sehemu yake ya pili inasema: "Mimi sikudharau chunga penzi letu lisiharibike, tulipopendana tulikuwa wawili, hivi leo sasa unanifanyia visa... Tulipendana mimi na wewe, tukaelewana sisi wawili. Leo mwenzangu unanifanyia visa..." Mtakuwa mnanisaidia na Mungu awabariki sana.