Рет қаралды 10,191
Wakati wa Mkesha wa Kuelekea maadhimisho ya Miaka 25 ya Kuundwa tena kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Usiku wa Alhamisi ya Novemba 28, 2024, Miongoni mwa yaliyokuwa kivutio kwa Mamia ya wana Afrika Mashariki waliokutana kwenye Barabara ya Mnara wa saa (Clock Tower) Jijini Arusha ilikuwa ni burudani ya Muziki iliyotolewa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanafanyika Novemba 29-30, 2024 Jijini Arusha na kuongozwa na Marais nane wa nchi zinazounda Jumuiya hiyo ya Kikanda.