Рет қаралды 77,339
Misa Amecea Lyrics
BWANA UTUHURUMIE (MISA AMECEA)
[ s/a ] { Bwana utuhurumie (ee Bwana)
[ w ] Bwana utuhurumie } *2
[ t/b ] { Kristu utuhurumie (ee Kristu)
Kristu utuhurumie } *2
[ s/a ] { Bwana utuhurumie (ee Bwana)
Bwana utuhurumie } *2
UTUKUFU KWA MUNGU (AMECEA)
[ t ] Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni
[ w ] Na amani kote duniani
( Kwa watu ) wenye mapenzi mema
Tunakusifu Baba, tunakuheshimu,
Twakuabudu sisi tunakutukuza
Twakushukuru Mungu kwa tukufu
Wako mkuu ewe Mungu mfalme
(Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu
Bwana wetu Mwokozi Yesu Kristu
Mwana wa pekee wake Mungu
(Uliye) Mwanakondoo wa Mungu
Unayeziondoa dhambi zote
Za dunia utuhurumie
(Pokea) pokea ombi letu
Wewe unayeketi kuume
Kwake Baba utuhurumie
(Sikia) sikia ombi letu
Kwani pekee yako ndiwe Bwana
Peke yako mkuu na mkombozi
(Pekee) pekee Yesu Kristu
Kwa umoja wa Roho Mtakatifu
Ndani yake Baba watukuzwa
(Ee Yesu) milele na milele
#catholicsongs #glory #utukufu #catholic