Рет қаралды 9,251
Fungu 1:
Na tuumwabudu huyo mfalme,
sifa za nguvu zake ziimbe;
Ni ngao, ni ngome, Yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.
Fungu 2:
Tazameni ulimwengu huu,
Ulivyoumbwa, ajabu kuu;
Sasa umewekwa pahali pake,
Hata utimize majira yake.
Fungu 3:
Kwa ulinzi wako,kwetu Bwana,
Twakushukuru, U mwema sana;
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kina mahali pake.
Fungu 4:
Wanadamu tu wanyonge sana,
Twakutumaini Wewe, Bwana;
Kamwe haupungui wako wema,
Mkombozi wetu, Rafiki mwema.