PUTIN AGOMEA HUKUMU YA KIFO, ASEMA HAYAFUATI MATAIFA YA ULAYA

  Рет қаралды 1,855

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

WAKATI baadhi ya mataifa ya Ulaya na Marekani yakitekeleza hukumu ya kifo, hali ni tofauti kwa Rais wa Russia Vladimir Putin ambaye amesema hatoridhia tena utekelezwaji wa adhabu ya kifo nchini humo.
Uamuzi huo ni mwendelezo wa misimamo ya Rais Putin kuhusiana na adhabu mbalimbali kwa watu wanaokutwa na hatia za kutenda makosa ya uhalifu nchini humo huku imani yake ikitajwa kumzuia kuridhia adhabu hiyo.
Tovuti ya Russia Today imeripoti kuwa Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo halina mpango wowote wa kurejesha adhabu ya kifo kwa raia wake badala yake litaendelea na utoaji wa adhabu kwa wanaobainika kuwa na hatia katika makosa mbalimbali kwa kutumia sheria nyingine za kihalifu.
Alitoa kauli hiyo Jumanne alipohutubia Barala la Jumuiya za Kiraia na Usimamizi wa Haki za Binadamu nchini humo, baraza ambalo lina jukumu la kumsaidia Rais huyo kulinda haki na uhuru wa wananchi wake.
Ameswma Msimamo wa Russia unaonekana kitobadilika pamoja na kuwa inaendelea na mapambano dhidi ya Ukraine.
“Tunaishi katika uhalisia ambao asilimia kubwa ya maisha yetu yanetawaliwa na vita na hatutopitisha adhabu ya kifo kwa mtu yoyote. Tutasimalia msimamo huo pamoja na kuwa nimekuwa nikikumbana na msukumo wa watu wengi hususan ni wanasiasa wanaotaka nipitishe na kuanza kutekeleza adhabu ya kifo,” amesema Putin.
Putin amesema pamoja na kuwa Russia inapitia wakati mgumu ambao ni wa gita ila tafa hilo haliko tayari kuanza kutoa adhabu ya kifo kwa sababu utu ndiyo kipaumbele chake katika mfumo wake wa haki.
Wakati huo huo, kiongozi huyo amesema Russia unaendelea na jitihada zake za kupunguza idadi ya wafungwa nchini humo hususan ni waliofungwa kwa makosa ya jinai kwa kuwajengea uwezo wa kuondokana na kurudia makosa hayo.
Russia iliwahi kupitisha adhabu ya kifo miaka 1997, muda mfupi baada ya kujiunga na Baraza la Ulaya na adhabu ya mwisho ya kifo ilitekelezwa mara ya mwisho mwaka jana tangu hapo Rais Vladimir Putin amegomea utekelezwaji wa adhabu hiyo kwa wafungwa.
Pia utoaji wa adhabu nzito kwa wafungwa haukuondolewa japo wanasiasa na viongozi wakubwa wa taifa hili wanaongeza msukumo wa kuanza kutolewa adhabu hizo jambo ambalo kwa Putin limegonga mwamba.
Uamuzi wa kusitisha adhabu ya kifo kwa raia ulifikiwa na Valdimir Putin nchini humo baada ya Russia kutangaza kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya na kudai kwamba kufanya hivyo ni kuendelea matendo ya mataifa ya magharibi badala ya kutawala kwa kufuata miongozo ya Russia.
Uamuzi huo wa Putin hautofautiani na kile ambacho Kanisa analosali Rais huyo la The Russia Orthodox ambalo lilipendekeza Novemba 6,2024 kuwa adhabu hiyo iondolewe na isirejeshwe nchini humo.
Kiongozi wa Kanisa hilo, Patriarch Kirill, alisema kanisa hilo linaungana naye na halikubaliani na utekelezwaji wa adhabu hiyo.
Mapendekezo ya kurejeshwa kwa adhabu ya kifo nchini humo yalichochewa na tukio la mauaji lililotokea Aprili mwaka huu katika Ukumbi ulioko Mji wa Crocus jijini Moscow. Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu 145 na mamia kujeruhiwa baada ya watu wanaodaiwa kuwa magaidi kutekeleza unyama huo.
Kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa ka Orthodox, alipotakiwa kuzungumzia tena adhabu hiyo ya kifo kwenye Ibada ya Jumapili iliyopita alisema;
“Adhabu ya kifo imekuwa katika historia ya maisha ya mwanadamu. Hata hivyo Jesu Kristo hakuiruhusu kuendelea kuwepo pamoja na kwamba alihukumiwa na kufa kifo cha mateso,” alisema Kirill.
Patriarch Kirill aliita kitendo cha kutoa adhabu ya mtu mwingine kuuawa kama uhalifu wa mauaji pia na kusema njia pekee nzuri ni kupambana kuzuia vitendo vya uhalifu visitekelezwe nchini humo.
“Kanisa halipogani nayo japo pia halikubaliani nayo kwa sababu ni adhabu ambayo haiwezi kukubaliwa sehemu yoyote duniani,” amesema kiongozi huyo.
Kirill alisema kama itafaa ni vyema watu ambao wanastahili adhabu ya kifo wakaadhibiwa kutumikia kifungo cha maisha jela ambacho ni kifungo kikubwa zaidi nchini humo.
“Tunapaswa kuangalia adhabu inapotekelezwa inaleta matokeo gani kwa taifa letu je inapunguza uhalifu ama bado utaendelea kuwepo. Tunashukuru Mungu kwa sababu kumuua mtu hakuondoi uhalifu,” alisisitiza kiongozi huyo.
Swali la kujiuliza, ni Je, unadhani adhabu ya kifo ndiyo njia ya kuumaliza uhalifu duniani?

Пікірлер: 8
@rashidichuri1149
@rashidichuri1149 3 сағат бұрын
tofautisheni sheria zakijeshi namahakama zaraia.
@rasnchimbi
@rasnchimbi 5 сағат бұрын
Wakati yeye anauwa wapinzani wake?
@rashidichuri1149
@rashidichuri1149 3 сағат бұрын
eleweni neno( kwaraia)
@hazygardmericho9571
@hazygardmericho9571 4 сағат бұрын
aache uongo, kwani prigozin alimhukukumu miaka mingapi jela
@JohnValle-xn1dx
@JohnValle-xn1dx 5 сағат бұрын
Mbona alimuuwa prigozin leo anataka kufumba watu macho
@rashidichuri1149
@rashidichuri1149 3 сағат бұрын
przigon aikuwa nahak yakuuliwa maana alilisaliti taifa
@SalehLoffy-kn6oh
@SalehLoffy-kn6oh 3 сағат бұрын
Kwani prigozin alipelekwa Mahakamani? Na mnauhakika prigozin kafa maana Kuna habari tofauti tofauti wengine wanasema yupo chichnia huko
@JonasPhilimon
@JonasPhilimon Сағат бұрын
Rijitu linauwa watu zaidi ya million alaf leo hii aseme anaogopa kuuwa kweli unafki umezidi
RUSSIA YASHAMBULIWA TENA, ENEO LA VIWANDA LAHARIBIWA NA UKRAINE
5:31
Mwananchi Digital
Рет қаралды 3,4 М.
Арыстанның айқасы, Тәуіржанның шайқасы!
25:51
QosLike / ҚосЛайк / Косылайық
Рет қаралды 639 М.
Новости дня | 11 декабря - дневной выпуск
11:40
Euronews по-русски
Рет қаралды 6 М.
Новости дня | 11 декабря - утренний выпуск
11:37
Euronews по-русски
Рет қаралды 83 М.
IRAN YAIWAKIA MAREKANI, ISRAEL KUPINDULIWA KWA ASSAD
5:19
Mwananchi Digital
Рет қаралды 1,2 М.