VIONGOZI Simba ongezeni nguvu kwenye timu ili iwe rahisi kuvuka kwenda nusu fainali. Bila kuongeza wachezaji atleast wawili akiwemo striker hatutaweza kufika nusu fainali. Kiwango kilichopo sasa hivi ni cha robo fainali tu. Tusijidanganye kwamba tutafika nusu fainali au fainali bila kuongeza wachezaji wapya wawili wenye uwezo mkubwa. Vunjeni kibubu mumchukue Rupia wa SBS na huyo Kipre tena msichelewa kwani muda unakwenda inabidi wachezaji waje wafanye mazoezi na wenzao mapema ili kufahamiana.