Рет қаралды 54,766
Ilikuwa ni siku ambayo Moza alitoka kupokea ela ya mchezo kiasi cha shilingi elfu sitini. Kilikuwa ni kiasi kidogo sana kulingana na mahitaji yake yote yaliyomo kwenye akili yake. Alifika nyumbani kwao na kuingia ndani moja kwa moja. Jambo lililomshangaza ni pale alipomuona Mama ake akiwa amekaa sebuleni kwa unyonge sana huku mkono ukiwa shavuni. "Haya kumekucha!" Moza aliongea mara baada ya kumuona Mama ake. Mama Moza alikuwa akijihusisha na biashara ya pombe za kienyeji, na mara kwa mara alikuwa akianguka kwenye mtaji na hiyo ilitokana na kutokuwa na uelewa wa mahesabu hivyo aliishia kudhulumiwa na wateja wake.