Рет қаралды 114,274
Lyrics
Tabibu Mkuu Yesu aletaye faraja kwetu, Mwenye huruma nyingi, Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
1. Pindi tuwapo wagonjwa, twatafuta madakitari, washindwapo twaugua nini, ndipo waita wataalamu. Yaweza chukua muda mrefu, huenda hata miaka, kupata utambuzi sahihi, miili yetu iuguayo.
2. Hata hivyo tunaye, tabibu mmoja wa kweli, hahitaji miadi kumwona, anahudumu wakati wote. Hakuna bima, madawa, matibabu yake ni bure, majibu ya yale uuguayo yeye Mungu anajua.
3. Tenga muda rafiki naye muuguzi wa ajabu, upate ukaguzi maalum, kuelewa ikuumizayo. Mweleze unavyohisi, kimwili, hisia, kiroho. Usimtafute tu Mungu wakati afya yako idororapo.