Рет қаралды 333
Rais Samia Suluhu amewataka viongozi kuacha kukusanya kodi kwa kutumia mabavu ikiwemo kufunga biashara za watu kisa wanadaiwa kodi.. Amesema licha ya kuwa sheria zinawaruhusu, lakini wakifunga biashara, wafanyabiashara hao wanahamia nchi jirani, hivyo kuikosesha serikali mapato.
-
"Wizara ya Fedha naomba mkasimamie Swala la Fedha Hasa Kwenye kulipa kodi, Lengo la serikali sio kuwaminya wafanya biashara, Kama mtakuwa mnawaminya Wafanyabishara Kwenye Kodi Mwisho wa Siku watafunga biashara zao na kwenda Nchi nyingine kuwekeza na tunakuwa tumepoteza kila kitu, naomba Waziri wa Fedha Ukalisimamie hili" Rais wa Tanzania Samia Suluhu
Kutokana na maono haya ya muongoza njia nayo TRA imeamua kuwa na utaratibu kabambe wa kutoa elimu kwa walipa kodi na Hii inaongeza tija na ufanisi zaidi endelea kufuatilia CB ONLINE TV kwa habari moto moto za Biashara hapa hapa.