Рет қаралды 308,888
Available on all platforms: album.link/ke/...
Performers: Christ the King Catholic Church Choir - Masii
Producer: Verony Productions Ltd.
Copyright ©Verony Productions Ltd.
Utukufu juu kwa Mungu Baba,
Utukufu juu mbinguni,
Na amani kote duniani Baba,
Kwa watu wenye mapenzi mema *2
Twakusifu Baba, tunakuheshimu
Tunakuabudu, tunakutukuza *2
Ewe Mungu ndiwe, Mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba Mwenyezi, Mungu Baba Mwenyezi
Tunakushukuru mwenye utukufu,
Mfalme wa mbinguni, Mungu Baba yetu
Mwana Yesu Kristu, mwana wa pekee,
Ee mwanakondoo, mwana wake Baba *2
Mwenye kuzifuta dhambi za dunia,
Utuhurumie, utusikilize *2
Mwenye kuketi kuume kwa Baba,
Pekee yako mkuu ewe Yesu Kristu *2
Pamoja na Roho Mtakatifu,
Katika utukufu wa Mungu Amina *2