Рет қаралды 8,093
Utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza uliwekwa kwenye darubini na wakenya waliojitokeza kwa vikao vya umma vinavyolenga kumbandua naibu rais Rigathi Gachagua ofisini. Katika maeneo mengi nchini, shughuli hii iligeuka kuwa kura ndogo ya maoni kuhusu utendakazi wa serikali, kutoka kwa wakenya walioonekana kujawa na ghadhabu. Waliozungumza maeneo mbalimbali wakiikosoa serikali kwa kujipa shughuli na mambo yasiyo na msingi, badala ya kuangazia maswala muhimu kama afya, elimu na hata vita dhidi ya ufisadi.