Рет қаралды 31
Chama cha msingi cha ushirika cha watumishi wa Mkoa wa Simiyu kimeshindwa kufikia malengo ya kulima ekari 1000 za pamba ambazo ilijiwekea ili kuendana na sera ya wizara ya kilimo ya kuzalisha tani milioni moja kwa nchi nzima ambapo mkoa wa Simiyu ulipanga kuzalisha tani laki tano sawa nusu ya pamba yote itakayozalishwa nchini.
Awali wakati wa utekelezaji wa mpango mkakati wa kulima pamba mkoani hapa watumishi walianzisha chama cha msingi cha ushirika (Watumishi Amcos) chenye lengo la kuwa mfano katika maswala ya kilimo.