Рет қаралды 772,908
Yanga SC wamebeba Kombe la Shirikisho la Azam Sports #ASFC kwa kuitandika Coastal Union penati 4-1 kufuatia sare ya mabao 3-3 katika dakika 120.
Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Feisal Salum dakika ya 57, Heritier Makambo dakika 82 na Denis Nkane dakika ya 113 huku magoli yote ya Coastal Union yakifungwa na Abdul Suleiman Sopu ambaye amefunga #Hattrick dakika ya 11, 88 na 98.
Katika mikwaju ya penati, Yanga wamefunga penati zote nne walizopiga kupitia kwa Yanick Bangala, Heritier Makambo, Dickson Job na Khalid Aucho huku Coastal wakipoteza penati mbili na kufunga moja kupitia kwa Victor Akpan.
Fainali hii imepigwa kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha......
Kutazama magoli na penati pekee ingia hapa • Magoli na penati | Yan...