BI ZAHARA (SIMULIZI YA KICHAWI YENYE MAFUNZO NDANI YAKE)

  Рет қаралды 6,863

GO-GO STUDIOS

GO-GO STUDIOS

Күн бұрын

Пікірлер: 34
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
KAMA BADO HAUJA-SUBSCRIBE CHANNEL YETU,BONYEZA ALAMA YA SUBSCRIBE. KWA WALE WANAOTAKA KUSOMA NIMEWEKA HAPA HAPA CHINI KWENYE COMMENTS (1--4)
@MOBISKOFILM
@MOBISKOFILM 13 күн бұрын
Nimefika leo hapa❤
@fatihiyadossa375
@fatihiyadossa375 7 ай бұрын
Hongera msimuliaji hizi ndo story ninazozipendaga zakichwawi chawi
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Yes,hii story na zingine zaidi utazipata hapa hapa ,na Kama bado hauja subscribe bonyeza alama ya subscribe, hii simulizi utaipenda Sana,kesho mwendelezo
@kombomvungi730
@kombomvungi730 7 ай бұрын
Kazi hii ni nzuri sana. Hongera mtunzi na msimuliaji
@JodaKissana
@JodaKissana 7 ай бұрын
Asante Sana,endelea kufuatilia zaidi hapa hapa,kuna mengi zaidi yanakuja
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Shukurani, mambo mazuri yanazidi kuja
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
UCHAWI WA Bi ZAHARA SEHEMU YA KWANZA MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA MAWASILIANO: 0748862999 ** Ilikuwa yapata majira ya saa nane usiku,katikati ya uwanja wa mpira wa miguu uliopo kijijini Mashene,walionekana wachawi saba wakiwa wamekusanyika huku wakiimba nyimbo zao. Wachawi hawa walivalia Mavazi yenye rangi nyeusi,sura zao zilichafuliwa kwa rangi nyeusi ya dawa ambazo huwa wanajipaka kwa ajili ya kuwasaidia kutokuonekana na watu wa kawaida. Uwanja wa mpira wa miguu ndio sehemu yao ya kujidai hasa nyakati za usiku, wanakijiji wa Mashene huwa wanapatwa na msisimko pindi wanapopita katikati ya uwanja huu,vilevile uwanja wa Mashene umezua gumzo kwa miaka ya karibuni Kwani, kila mwaka lazima mchezaji mmoja wa mpira wa miguu apoteze maisha ndani ya hiki kiwanja. Kutokana na sifa yake kuwa mbaya,wanakijiji waliamua kuuacha uwanja wa Mashene, hakuna ambaye alikuwa anaenda kucheza mpira katika uwanja huu wa Mashene. Sifa nyingine kubwa kuhusu hiki kiwanja ni kwamba,ukipita nyakati za mchana katikati ya uwanja huu utaanza kupigwa makofi na watu wasioonekana,wanakijiji wa Mashene wanasema,hata Kama ukiwa na njaa iliyoje lakini usithubutu kula Chakula utakachokiokota barabarani. Kutokana na mambo haya yanayoendelea katika kijiji cha Mashene,wanakijiji wake huwa hawali Chakula barabarani, hata Kama Chakula umenunua wewe lakini usithubutu kula barabarani, ukithubutu kufanya hivyo basi siku tatu zijazo utakuwa maiti. ** Wachawi saba wakaendelea kuimba nyimbo zao kwa furaha,walizunguka katikati ya uwanja wakiyatoa macho yao pamoja na vicheko vya kutisha,familia za watu wanaoishi jirani na uwanja huu huwa wanapitia magumu hasa nyakati za usiku,Milio ya fisi na mbwa huwa ni kawaida kusikika masikioni mwao. Wachawi saba wakazunguka takribani mara saba,mara ghafla ngoma wakaizimisha ngoma,wote kwa pamoja wakashikana mikono kisha wakatazama juu,walianza kuongea maneno ya kichawi ambayo wanajua yana maana gani. Punde si punde kuna mwanga mkali wa radi ukang'ara kutokea juu na kupiga katikati yao,huu ulikuwa ni ujio wa mkuu wao ambaye anafahamika kwa jina la Bibi Zahara. Bibi Zahara alifika akiwa amevalia Mavazi yafananayo na wachawi wenzake, umri wa Bibi Zahara ni miaka sabini na tano,anasifika kwa kuwa na nguvu nyingi za kichawi kuliko wachawi wote wa kijiji cha Mashene na wilaya nzima ya Rorya mkoani Mara. Ujio wa Bibi Zahara kwenye kikao cha wachawi ulikuwa na maana kubwa kwao,kuna ajenda zao za siri za kichawi ambazo wamepanga kuzitimiza siku ya Leo. Sikuzote wachawi huwa hawapendi maendeleo ya wenzao,Furaha yao ni kuona mwanadamu anashindwa kutimiza ndoto zake kwa kumzuia kupitia nguvu zao walizonazo. Kwa mantiki hiyo,hata ajenda kuu ya siku ya Leo ilikuwa inahusu kuharibu mipango ya mmoja wa wanakijiji cha Mashene. Bibi Zahara akacheka kicheko ambacho kilisambaa kijiji kizima halafu kikawa kinajirudia kwa mwangwi. "Hahahah,hahahahha,hahahah" Bibi Zahara aliachia kicheko ambacho kilipelekea mapengo yake ya mbele kuonekana. Wachawi wenzake wakampatia sapoti kwa kuangua kicheko,mbwa walibweka na fisi nao wakaanza kulia milio ambayo ilitisha Sana. Bibi Zahara akainua mikono yake miwili juu,mara ghafla anga la kijiji cha Mashene likabadilika na kuwa jekundu. Ingawaje ulikuwa ni wakati wa usiku lakini kubadilika kwa rangi ya Anga ilionekana, wanakijiji hawakuweza kuona mabadiliko ya anga kwa sababu walikuwa wamelala. Bibi Zahara akacheka tena kicheko kilichosambaa kila kona ya kijiji,alitumia dakika mbili kucheka ndipo akashusha mikono chini,aliposhusha tu mikono anga nalo likarudi katika hali yake halisi. Bibi Zahara akasema "Mbona hamjaagiza viti?" Wachawi wakatazamana,Bibi Zahara akasema "Hebu kila mmoja aite kiti chake" Kila mchawi akachukua tunguli lake lililo na sehemu ya kupulizia,wakatamka maneno kadhaa kupitia tunguli walizonazo,papo hapo wakashuka marehemu saba waliokufa siku nyingi. Marehemu saba wameshageuzwa kuwa misukule,kazi yao kubwa ni kufanya kazi wanazopatiwa na wachawi,vilevile huwa wanatumika Kama viti endapo wakihitajika.Misukule hawakuwa wanajitambua,walikuwa wamepauka huku wakiwa wanatokwa na udenda mdomoni,kila msukule ulikuwa unamjua bosi wake,walienda wakapiga magoti kisha migongo wakaiweka juu mithili ya ng'ombe ama punda abebapo mizigo. Wachawi saba wakakaa juu ya migongo ya marehemu(misukule),Bibi Zahara hakuwa ameita kiti kwa siku ya Leo,akawa amesimama katikati ya wachawi wake. Bibi Zahara akapaza sauti kwa kusema "Wahalooooo" Wachawi wenzake wakaitikia "Wahalooooo" Hii ni salamu inayotumika kufungua maongezi yao,Bibi Zahara akaendelea kwa kusema "Nadhani wengi wetu mmeshangaa kuona kikao cha dharura tumekiitisha hapa,bila kupoteza wakati ningelipenda kuwaambieni jambo gani ambalo limepelekea niwaite hapa" Wachawi wakatega masikio yao "Kuna mwanakijiji mmoja anataka kujiona yeye ndiyo yeye,eti anataka kufunga ndoa ndani ya kijiji chetu,mbaya zaidi amemuacha mjukuu wangu akaenda kuoa mwanamke mwingine wa mjini" "Hivi ndugu zangu ,hamuoni Kama hii ni dharau kwa familia ya Bibi Zahara?au mnataka tumuache aendelee kutamba ndani ya kijiji chetu?" Wachawi wote saba wakamuunga mkono Bibi Zahara kwa kuitikia "Hii ni dharau kubwa mkuu" "Hahahah...sasa basi ,inatakiwa tumuoneshe Kama sisi ni kilinge cha Manjunju,hahahah" Wachawi wote wakacheka "Hahahah" Bibi Zahara akanyoosha mkono juu kuwataka wakae kimya "Mchezo wetu ni uleule,kabla hawajafunga ndoa itabidi sisi tufanye yetu" "Sawa mkuu" "Kikao cha Leo kinaishia hapa,au kuna swali?" Mchawi mmoja wa kiume akanyoosha mkono. Bibi Zahara akamuona "Baba Otieno unataka kusema nini?" Baba otieno ana umri wa miaka arobaini, ni miongoni Mwa wachawi saba waliopo chini ya Bibi Zahara. Baba otieno akasema "Mkuu,naomba hiyo kazi ya kumuua huyo Kijana nipatiwe Mimi,haiwezekani atudhalilishe" "Haina shida Baba otieno,siku ya kesho tutakusanyika tena hapa kwa ajili ya kuweka mambo sawa,..jambo la mwisho ni wale wote waliopo zamu ya kuwanga usiku wa Leo,itawabidi muendelee kuwanga mpaka muda wetu utakapoisha" "Sawa mkuu" (waliitikia wachawi wanne,hawa wachawi walioitikia ndio watakaobaki kuwanga kwenye nyumba za wanakijiji cha Mashene) Bibi Zahara akacheka Sana kisha akapokea kichawi,katikati ya uwanja wakabaki wachawi saba wakiwa wanamalizia kucheka ngoma za kichawi,baada ya dakika tano kupita tangu Bibi Zahara apotee kichawi,wale wachawi ambao hawapo zamu ya kuwanga usiku wa Leo wakaanza kupotea mmoja mmoja akiwa na msukule wake. Wanakijiji wa Mashene huwa wanapitia mateso makubwa kutoka kwa wachawi,kila siku lazima wafanyishwe mazoezi ya kila aina, raha ya mchawi ni kuona unatesekea,anaweza ingia chumbani kwako na asitoke hata na Mia yako,ila furaha yake akiwa anakuchezea na kukugeuza geuza mfano wa chapati. Wachawi wakaendelea kupita nyumba moja baada ya nyingine, walikuwa wanapita pasipo pingamizi kwa sababu wanakijiji hawakuwa na nguvu za kuwalinda,utaratibu huu wa kupita nyumba kwa nyumba ni utaratibu ambao umezoeleka kwa wachawi. Wakiwa wanapita nyumba moja baada ya nyingine huwa wanatafuta nyama za binadamu.Wachawi walifika nyumba moja iliyojengwa kwa tope na kuezekwa kwa nyasi,wakamkuta mama mmoja mjamzito akiwa amelala na mume wake. Wachawi wakaanza kukizunguka kitanda huku wakicheza ,walizunguka kwa dakika kadhaa kisha kiongozi wa msafara wa wachawi waliopo zamu akasema. "Huyu mama ni mjamzito,inatakiwa tukipate hicho kitoto alichobeba tumboni kikatusaidie kuongeza nguvu" Wachawi wakanyoosha mikono yao kuelekea kwa mama mjamzito aliyelala kitandani,wakatoa miale yenye rangi nyeupe machoni mwao,miale ile ikaelekea tumboni kwa mama mjamzito. Wakakivuta kitoto tumboni pasipo mama mjamzito kufahamu.Wachawi huwa wanatumia mbinu hii kukitoa kitoto tumboni Mwa mama yake pasipo wao kujua,siku ya kesho ataona damu zinamtoka kwenye via vya uzazi na atahisi mimba imeporomoka kumbe wachawi wamemchukua mtoto wake. Wachawi wakamchukua mtoto kisha wakapotea kichawi na kumuacha mama mjamzito akiwa amelala kitandani,hakuwa anajua alichofanyiwa na wachawi,hata tumbo lake lilibaki vilevile ila akienda kufanya vipimo ataambiwa hana ujauzito Wachawi wamepanga siku ya kesho mama mjamzito aone damu nyingi zinatoka ukeni,akiona vile atahisi ujauzito umetoka.Vilevile huduma za afya hazikuwa karibu na kijiji cha Mashene, iwe isiwe lazima mama mjamzito atakubaliana na hali ya kumpoteza mtoto. Itaendelea..... 😈HUU NI MWANZO TU. 😈BIBI ZAHARA NA GENGE LAKE LA WACHAWI HAWATAKI NDOA IFUNGWE,NDOA HIYO YA NANI?NA HUYO MJUKUU WA BI ZAHARA NI NANI?
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji) SEHEMU YA PILI(02) MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA MAWASILIANO: 0748862999 ** Siku iliyofuata majira ya saa tatu asubuhi, nje ya nyumba moja inayoonekana kuezekwa kwa bati ,wanaonekana wanakijiji mbalimbali wa kijiji cha Mashene wakiandaa Mazingira kwa ajili ya sherehe, wamama walikuwa wanachota maji ,wengine walikuwa wanaosha vyombo na wakati huo wanaume walikuwa wanachimbia miti itakayotumika kufungia turubai. Shamrashamra zilikuwa zinaendelea katika familia hii,ndani ya nyumba ya udongo iliyokuwa imepakana na nyumba yenye bati,alionekana Kijana mmoja wa makamo ya umri wa miaka ishirini na nane,Kijana huyu alivalia Mavazi tofauti na wanakijiji wa hapa,bila Shaka ameishi Sana maisha ya mjini tofauti na wanakijiji wengine. Hassan Onyango ndilo jina la Kijana huyu,alikuwa anachezea Simu yake ya smatifoni huku amejilaza juu ya kitanda cha kamba,tabasamu mwanana halikuacha kuchanua kwa Hassan. Hassan alikuwa anachati na mwanamke mrembo ambaye anatarajia kumuoa siku ya kesho,kuna ujumbe akauandika. "Kipenzi changu sipati picha siku ya kesho utakavyokuwa unashangaa kuona mila za kikwetu" Ujumbe ukajibiwa "Nishaanza kuzoea,hapa nipo na wadada wawili wananiandaa andaa" "vipi Mazingira umeyazoea ?nahofu Sana juu yako hasa kulala katika kitanda cha miti na kamba" "Ondoa Shaka ,Leo ni siku ya pili tangu tufike kijijini kwenu ,nitazoea taratibu kipenzi changu japo Usiku wa Jana nilikuwa nasikia sauti za ajabu" "itabidi uzoee kipenzi changu,hiyo ndio sababu kubwa sikutaka ndoa yetu ifungiwe huku ila kwakuwa uliniomba tuje kwa wazazi wangu nikakubali" "Mume wangu hapa ni kwenu,unapoishi nilipaswa kupafahamu kuliko kufunga ndoa mjini bila kuona ndugu zako,kwa Sasa nina amani na Furaha ,Dada zako nipo nao wananifundisha mengi nisiyoyajua" "OK mrembo,Mimi nipo kitandani nimepumzika" "Poa baadae" Hasani na mke wake mtarajiwa wakaishia hapo kuchati,Hassan akajipumzisha kitandani kwa Furaha maana siku ya kesho anaenda kufunga ndoa na mwanamke wa ndoto zake,hakuwa anajua Kama Bi Zahara na kundi lake la Wachawi wanapanga mikakati ya kumdondosha. ** Nyumba nyingi za kijiji cha mashane zimejengwa kwa tope na kuezekwa nyasi ama makuti,ni nyumba chache Sana ambazo zimejengwa kwa tofali za kuchoma na kuezekwa bati,ukiiona nyumba ya bati basi hapo ni kwa mwenyekiti ama mkulima mkubwa. Kulikuwa na nyumba moja ya udongo iliyojengwa pembeni kidogo na kijiji cha Mashene, nyumba hii ilikuwa imejitenga peke yake bila ya kuwa na majirani wa karibu,nyuma ya nyumba kulikuwa na makaburi mengi. Mlango wa nyumba ukaonekana kufunguliwa na aliyekuwa anatoka ni Bibi Zahara. Bibi Zahara alikuwa amechoka choka,akatoka nje huku akijinyoosha nyoosha. "Dah,nimechelewa kuamka" Katikati ya uwanja wa Bibi Zahara kulikuwa na nyuma ndogo iliyochakaa,haikuwa inafahamika ni stoo ama nyumba ya kufugia wanyama. Bibi Zahara akasogea mpaka ilipo nyumba ambayo imechakaa,akaufungua mlango kisha akaingia ndani. Kwa macho ya nyama hauwezi ona chochote ndani ya hii nyumba,Bibi zahara akapuliza mluzi mithili ya mfugaji akimtuma mbwa wake mkali kwenda kuwafukuza mbuzi wanaokula mahindi yake. Sekunde kumi zilitosha kuonesha vitu gani vipo ndani ya nyumba iliyochakaa.Kulikuwa na misukule wapatao ishirini,misukule hawa walikuwa wanatokwa na udenda mdomoni ,wengine wamejikunja mikono n wengine macho yao yamebadilishwa kutoka kuwa ya binadamu mpaka ya fisi. Misukule walipomuona Bi Zahara wakaanza kuunguruma,njaa ilikuwa inawasumbua ndio maana walipomuona Bi Zahara wakaanza kupiga makelele. "Hebu nyamazeni ,Leo sijawaletea Chakula,subirini mjukuu wangu na wenzenu warudi kutoka mashambani na mihogo" Misukule huwa wanalishwa mihogo kila siku,mara moja moja ndio bi Zahara huwa anawakorogea uji wa mahindi.Misukule hawa ni watu waliokufa,kila msukule uliopo nyumbani kwa Bi Zahara chanzo cha kifo chake kilisababishwa na Bibi Zahara. Furaha ya Bibi Zahara ni kuwaona watu wakiteseka,huwa anachukua kwa nguvu za Giza kisha anaanza kuwafuga.Misukule wanamsaidia bi Zahara katika shughuli nyingi za kiuchumi,ijapokuwa anaishi yeye na mjukuu wake lakini amelima hekali kumi za mahindi ,mihogo na viazi. Kazi ya kulima,palizi mpaka kuvuna huwa anawatuma misukule wake. Bi Zahara akamsogelea msukule mmoja ambaye anaonekana kuwa na kitambi. "We Omondi punguza uroho,ulikuja hapa hauna kitambi sahivi tumbo kubwa,sipendi li mtu li roho Mimi alaa"(Bibi Zahara hakufurahishwa na kitambi cha omondi) ** Baba Otieno alikuwa ni mmoja wa wanaume waliohudhuria katika maandalizi ya ndoa inayotarajiwa kufungwa siku ya kesho. Kazi aliyokuwa ametumwa Baba otineo ni kuhakikisha hakuna zindiko lolote linafanyika sehemu hii. Baba otieno ni mchawi kutoka katika kundi la Bi Zahara,amejichanganya na watu wengine pasipo kujulikana Kama ni mtu mbaya.Macho ya Baba otieno yalikuwa yanapepesa kila kona,alitazama mlango wa kuingilia ndani ya nyumba aliyopo Hasan. Baba otieno akawatoroka wanaume wenzake ,anazunguka nyuma ya nyumba ya akina Hasan pasipo kuonekana na mtu yeyote,alipofika nyuma akatazama kushoto na kulia kisha akatoa hirizi iliyokuwa imefungwa ndani ya mfuko mdogo mweusi. Baba otieno akachimba shimo haraka haraka halafu akazindika hirizi yake ya kichawi,alipofukia akatamka maneno kadhaa ya kichawi ambayo hayakuwa yanaeleweka. Baba otieno akaachia tabasamu la kinafiki "Muda wako Hasan umefika" Akasimama huku akitabasamu,akarudi kwa wanaume wenzake alipowaacha. Hasan akiwa ndani peke yake,akajikuta akipata usingizi mzito usio wa kawaida,usingizi huu ulimfanya Hasan atowe na jasho mithili ya mwanariadha aliyefika mwisho wa mbio zake. Hali ya Hasan ikaanza kubadilika,jasho lilimtapakaa mwilini,hakuwa na nguvu za kuamka kitandani maana usingizi wa kichawi umemchukua,Bwana harusi mtarajiwa hali yake ni mbaya,wanakijiji hawakuwa wanajua kinachoendelea chumbani kwa Hasan,wao walikuwa 'bize' kuandaa Mazingira mazuri kwa ajili ya siku ya kesho. ** Bibi Zahara alikuwa anawapiga misukule waliopo nyumbani kwake,aliwafanya anavyotaka. Bi Zahara akamsogelea msukule mmoja "Leo Usiku nitakupeleka kwa mkeo ukafanye naye Mapenzi,au haujamkumbuka mke wako?" Msukule alikuwa anacheka Cheka huku anatokwa na udenda, "Unanisikia?" (Bi Zahara akampiga Kofi msukule) Bi Zahara anampango wa kumpeleka msukule kwa mke wake akafanye naye Mapenzi,kwa uchawi alionao bi Zahara huwezi fahamu Kama ameingia nyumbani kwako,aina hiyo ya uchawi ndio huwa anautumia kuwapeleka misukule wake wakawaingilie wanawake wa kijiji cha Mashene. ** Hali ya Hasan ilizidi kuwa mbaya,endapo hatopata msaada ndani ya dakika tano basi atapoteza maisha,uchawi uliotumika na Baba otieno unaitwa 'Ungusu',huu ni aina ya uchawi ambao hutumika kumuua mtu kwa usingizi,yaani mtu anapata usingizi mzito unaomnyima nguvu hadi kifo. Hasani ametupiwa uchawi na Baba otieno ndiyo maana amepitiwa na usingizi mzito,jasho likaendelea kumtoka Hasan ,mapigo yake ya moyo yakazidi kumwenda mbio mithili ya mpira wa kona. Wakati Hassan amebakiza muda mchache apoteze maisha,upande wa pili kwa mke wake alikuwa anasukwa nywele na wadada wawili ambao ni Dada zake na Hasan. Angel ndilo jina la mke mtarajiwa wa Hasan,rangi yake ya ngozi ni maji ya kunde,ana sura nzuri ya kuvutia,umbo lake namba nane ndilo linakamilisha asilimia tisini na tisa za uzuri aliojaliwa. Angel alikuwa ndani ya nyumba ya udongo akiwa anasukwa nywele na Dada zake na Hasan. Mara ghafla kuna hali ya ajabu ikatokea,wasusi wote wawili pamoja na angel wakaganda,wasusi waliokuwa wanamsuka angel wakaganda,vilevile angel na yeye akaganda vilevile.. Upepo ukavuma ndani ya nyumba kisha wachawi wanne wanaotoka katika kundi la Bi Zahara wakatokea.Wachawi hawa ndio wamewagandisha Dada zake na Hassan pamoja na angel Wachawi wakaanza kuruka ruka Kama ndege,wakachukua tunguli zao walizozifunga kwa kamba nyeusi shingoni,wachawi wakatazamana kwa macho yaliyotoka nje. Wakainua mikono juu kwa pamoja, wakatamka maneno ya kichawi kwa awamu tatu,papo hapo kikashuka kisu kikali pamoja na chungu kidogo. Mchawi mmoja wa kike aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wote akasema kwa sauti ya chini. "Huyu Bibi harusi damu yake tutaiweka ndani ya hiki chungu" Wachawi wenzie wakajibu kwa kuunguruma Kama simba "Ngruuuuu" Wachawi wanaotoka kwa Bi Zahara wanataka kumchinja Angel kama kuku. Angel na Dada zake na Hassan wamegandishwa kichawi,upande wa Hassan na yeye amebakiza dakika tatu apoteze maisha, matukio mawili yanatokea kwa mpigo na yote yanawahusu wapendanao wanaotarajiwa kufunga pingu za maisha siku ya kesho. Itaendelea.....
@SummyStories
@SummyStories 7 ай бұрын
Safii mno ❤❤❤❤
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Tuendelee kupambana
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji) SEHEMU YA TATU(03) MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA MAWASILIANO: 0748862999 ** Hassan akaendelea kupambania roho yake,hakuwa na nguvu za kuamka kitandani,akawa anatokwa na mapovu mdomoni mithili ya Yale yatokanayo na sabuni wakati wa kufua. Hassan akawa anajitahidi kuamka lakini hakuweza,kila alipojitahidi walau kupiga kelele za kuomba msaada alishindwa,Hassan akaanza kupoteza nuru taratibu. Akiwa anakaribia kukata roho,mlango wa chumba alichopo ukafunguliwa,aliyeingia ni mshenga wake anayeitwa Mwita.Mshenga Mwita alivalia mavazi yanayofanana na Hassan kwa sababu hawa ni marafiki wa tangu utotoni. Mwita alipomuona hasana anatokwa na mapovu akapiga kelele za kuomba msaada "Uwiii...msaada...msaada" Kelele za Mwita zikapenya kwenye ngoma za masikio ya wageni waalikwa,wakakimbia kuelekea walipoisikia sauti ya kuomba msaada. Wanaume wakaingia ndani kuangalia nini kinachoendelea, wakamkuta Mwita akiwa amepiga magoti mbele ya kitanda alicholala Hassan. Hassan hakuwa amepoteza maisha bali hali yake ni mbaya,anatokwa na povu jingi mdomoni mwake. Miongoni Mwa wanaume walioingia chumbani alikuwepo Baba Hassan,umri wa baba Hassan ni miaka arobaini na sita,kitendo cha kumuona mwanae akiwa amelala kitandani akajikuta akianza kutokwa na machozi bila mpangilio maalumu. Wanawake walikusanyika nje ya mlango huku kila mmoja akisema lake,wengine walikuwa wanalia ,wengine walianza kunong'ona kwa kutupiana mpira nani atakuwa anahusika na hili. Mama yake na Hassan alikuwa ndani ya nyumba nyingine, alipopewa taarifa za mwanae kuugua ghafla na yeye pale pale akapoteza fahamu. Baadhi ya wanawake wakaanza kumpepelea Mama Hassan, wakati mama hassan anapatiwa tiba ndiyo wakati ambao Hassan anapatiwa huduma ya kwanza. "Jamani pungueni ndani apate hewa" ilikuwa ni sauti ya Baba otieno, yaani baba otieno ndio chanzo cha haya yote lakini anajidai ni mtu mwema na mwenye kujali.Baba otieno akawaomba watu wapungue ndani,wanaume tisa wakabaki ndani ya chumba kwa ajili ya matibabu ya hassan. Walijaribu kila namna wawezayo na wasiweze,Hassan alikuwa Kama aliyepatwa na kifafa,alianza kujirusha rusha huku akitokwa na povu mdomoni,baada ya dakika tatu kupita hassana akatulia kimya. Ukimya ukatawala ndani ya chumba ,kila mmoja akawa anamtazama mwenzie,utulivu wa hassan ni dalili mbaya kuwa huenda amepoteza maisha. Baba Hassan akaanza kulia "Mwanangu?mwanangu usiniache mwanangu, nakuomba mwanangu usiniache" (Baba Hassan alilia Sana). ** Upande wa pili kwa angel na Dada zake Hassan, walikuwa bado wamegandishwa na wachawi ambao wanataka kumuua angel. Wachawi wakaandaa kisu Chao ambacho huwa wanakitumia kuchukulia damu za watu wanaohitaji kuwala nyama,kisu hiki cha maajabu wakimchoma angel ataugua ugonjwa wa muda mrefu mpaka kifo. Mchawi aliyeshika kisu akamsogelea angel,akakiinua kisu ili akishushe kifuani mwa angel,kabla hajakishusha akasita baada ya tundu za pua zao kunusa harufu ya ujio wa binadamu. Mchawi mwenye kisu akasimama "Kuna watu wanakuja,tena inaonekana wamefika karibu" (akawa ananusa nusa) "Twendeni haraka wasitukute" wachawi wakapiga magoti na kupotea kichawi,hiyo ndio ikawa pona pona ya angel. Wachawi walipotoka tu,angel na mawifi zake wakaendelea na shughuli zao za kusukana,hawakuwa wanajua Kama walikuwa wamegandishwa kwa dakika kadhaa,wao walijiona wapo kawaida. Angel akaendelea kusukwa na mawifi zake huku wakisindikiza stori za hapa na pale,angel hakuwa anajua Kama mume wake amepoteza maisha kwa sababu nyumba ya bibi harusi ilikuwa mbali na Bwana harusi. Mama na Dada yake na angel wakaingia ndani alipo angel bila ya kupiga hodi,walionekana kujawa na hasira Sana. "Mama Kuna nini tena?mbona mmeingia ndani bila kupiga hodi?" Mama yake na angel ni mama wa makamo,sura yake inafanana na ya angel,tofauti yake na watoto wake ni unene,yeye ni mnene kuliko angel na Dada yake. Dada yake na angel anaitwa Patricia,umri wake ni sawa na angel kwa kuwa ni mapacha wanaofanana. Angel akawauliza tena "Kuna nini?" Mama angel akasema "Mwanangu hapa ndoa haipo,kusanya kila kilicho Chako tuondoke" "Mama sijakuelewa ,unasema kwamba..?" Patricia akadakia "Dada hapa hakuna ndoa,utafungaje ndoa peke yako bila Bwana harusi?" "Bila bwana harusi? Mbona siwaelewi?" (Angel alibaki njia panda) "Mwanangu, mume wako ame..." (Mama angel akainamisha kichwa chini) Dada zake na hasan kwa pamoja wakajikuta wakiuliza swali linalofanana "Kaka kafanya nini?" (Waliuliza wakiwa wameyatoa macho kwa mshangao) Patricia akapiga moyo konde,akasema "Amefariki" "Amefariki?mama anachosema da Patricia ni kweli?eti mama hebu nijibu,ama mmeamua kunifanyia sapraizi,hee?mama sema hajafa,mama?" (Angel hakuwa ana amini kusikia hassan amepoteza maisha) "Mwanangu anachokisema Dada yako ni kweli,mumeo amekutwa akiwa amekufa ndani ya nyumba aliyokuwepo" "Mama haiwezekani, nimeongea na mume wangu muda mchache uliopita,eti wifi zangu si nimeongea na kaka yenu?" Angel akaanza kulia. "Mwanangu inavyoonekana ni mambo ya kishirikina, naomba ujiandae turudi mjini,hiki kijiji kinaendekeza mambo ya kichawi" "Hapana mama,siwezi kuondoka" angel alikuwa mbishi. Dada zake na Hassan wakatoka nje huku wakilia,mbio mbio wakaanza kurudi nyumbani ambapo kuna msiba. "Mama niache nikamuone mume wangu mama,tumahidiana mambo mengi,tena alisema mtoto wetu wa kike ataitwa jina lako,mama niache" (Angel alilia mpaka akakaa chini) Patricia na mama yake wakamkumbatia angel kwa kumfariji,kifo cha Hassan kimemuumiza angel ukizingatia kimetokea siku moja kabla ya siku ya harusi, angel amejiandaa kufunga ndoa siku ya kesho lakini anapata taarifa mbaya za kumpoteza mume wake. "Mdogo wangu angel najua ni maumivu kiasi gani unapigia,ila naomba usikilize ushauri wa mama,twende turudi mjini ,hapa hapafai tena,haiwezekani mtu afe ghafla"(Patricia alizidi kumfariji pacha yake). " mama Mimi nina mkosi gani Mimi,ndoa ilikuwa kesho halafu mume wangu amefariki, mama uwiii"(angel alilia kwa uchungu) ** Vilio vilitawala nyumbani kwa akina hassan,hata Baba otieno alidondosha chozi la kinafiki,kutoka kuwa sherehe mpaka kuwa msiba,watu hawakuwa wana amini wanachokiona na kukisikia. Zile nyimbo walizoandaa kwa ajili ya siku ya kesho wakazitupilia mbali,na sasa wimbo utakaoimbwa siku ya kesho ni 'parapanda,Italia parapanda'. Baba Hassan alishindwa kumtazama mwanae, akatoka nje kwa majonzi makubwa.Huwezi amini Baba otieno ni rafiki wa karibu na familia hii. Baba otieno alipomuona Baba Hassan ametoka nje,na yeye akamfuata. "Pole sana rafiki yangu" (Baba otieno alimpatia pole rafiki yake) Dada zake na Hassan walifika nyumbani mbio mbio,wakakutana na hali iliyowafanya waamini maneno waliyoyasikia kutoka kwa mama na Dada yake angel. Kwanza walipigwa na butwaa kukuta vilio vimetawala,wakaanza kutembea kwa kuburuza miguu,hawakuwa wana amini Kama kaka yao Hassan amepoteza maisha. Watu wote wakatoka ndani ya chumba na kuuacha mwili wa marehemu Hassan ukiwa umelala kitandani,waliufunika shuka wakisubiri sanda ya kufanyia mazishi,lakini pia masikio na pua waliziziba kwa pamba. Bwana harusi mtarajiwa amepoteza maisha ikiwa ni masaa machache kufikia siku maalumu ya kufunga pingu za maisha. ** Ugeni wa wachawi ukatua nyumbani kwa bibi Zahara,hawa ni wale wachawi waliokuwa wanataka kumchoma kisu angel. Walifika wakamkuta Bibi Zahara akiwa ndani ya nyumba ya misukule, bibi Zahara akatoka nje baada ya kuhisi hali ya tofauti. "Nipeni taarifa" Mchawi mmoja akasema "Mkuu,kuna watu walitokea tukashindwa kumuua Bibi harusi" "Mmeshindwa kumuua?hivi mpo kweli na hii kazi?au mnataka niwageuze misukule sasahivi?" (Wakajibu kwa pamoja)"tusamehe mkuu" Bibi Zahara akakasirika mpaka macho yake yakabadilika rangi kuwa mekundu,akaachama mdomo na kutoa ulimi mrefu ,ulimi ule ulikuwa na kichwa cha Nyoka kwa mbele. Ulimi wa Bibi Zahara hubadilika na kuwa Kama Nyoka endapo akiwa na hasira ama akiwa anataka kumpatia mtu adhabu,Bi Zahara ana nguvu kuliko wachawi wote wa kijiji cha Mashene na wale wanapatikana vijiji jirani na hapa. Ulimi nyoka wa Bibi Zahara ukaanza kumnusa mmoja baada ya mwingine,wachawi wote wakajikuta wakitetemeka maana wanajua balaa zito litokanalo na ulimu wa bi Zahara. Itaendelea........
@kombomvungi730
@kombomvungi730 7 ай бұрын
Kazi nzuri sana
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
@@kombomvungi730 asante Sana ndugu yangu kombomvungi
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
BIBI ZAHARA (Mchawi wa kijiji) SEHEMU YA NNE(04) MTUNZI&MWANDISHI; JODA WA KISSANA MAWASILIANO: 0748862999 ** TULIPOISHIA..... Bibi Zahara akakasirika mpaka macho yake yakabadilika rangi kuwa mekundu,akaachama mdomo na kutoa ulimi mrefu ,ulimi ule ulikuwa na kichwa cha Nyoka kwa mbele. Ulimi wa Bibi Zahara hubadilika na kuwa Kama Nyoka endapo akiwa na hasira ama akiwa anataka kumpatia mtu adhabu,Bi Zahara ana nguvu kuliko wachawi wote wa kijiji cha Mashene na wale wanapatikana vijiji jirani na hapa. Ulimi nyoka wa Bibi Zahara ukaanza kumnusa mmoja baada ya mwingine,wachawi wote wakajikuta wakitetemeka maana wanajua balaa zito litokanalo na ulimu wa bi Zahara. SONGA NAYO..... Bibi Zahara alijawa na hasira isiyo kifani,akajiandaa kuwatemea mate wachawi wake,lakini kabla hajafanya vile kuna sauti ikamzuia. "Bibi acha" (sauti hii ilikuwa inatoka kwa Mjukuu wake Zahara) Zahara alikuwa amevalia mavazi ya asili yaliyoshonwa kwa ngozi ya ng'ombe,ingawaje anaishi kijijini lakini ni mzuri Sana.nyuma ya Binti Zahara kulikuwa na misukule watatu ,mmoja wa kike na wawili wa kiume,misukule walikuwa wamebeba mifuko iliyojaa mihogo mibichi. Kwa macho ya nyama hauwezi iona misukule,mtu ambaye utamuona ni Zahara pekee ,misukule unaweza iona ukiwa na nguvu ya ziada. Zahara akapiga hatua mpaka kwa Bibi yake na wachawi aliokuwa anataka kuwaua "Bibi kuna nini?" Bibi Zahara akaurudisha ulimi nyoka ndani ya mdomo wake,akamtazama mjukuu wake Zahara. "Hawa wameshindwa kuifanya kazi niliyowaagiza" "Kazi gani?" "Niliwaambia wamuue Binti aliyekuwa anatarajiwa kufunga ndoa na Hassan ila wao wameshindwa" Zahara alikuwa na moyo wa huruma dhidi ya wachawi wenzake, akamwambia Bibi yake. "Naomba uwasamehe Bibi,halafu Mimi sioni haja ya kuwaua wote wawili kwa mpigo,hebu tuwapatie muda walau kwa siku tatu ndipo tumuue huyo binti" (Zahara akamtazama Bibi yake) Bibi Zahara anampenda Sana mjukuu wake,kila anachokiongea Zahara mbele ya Bibi yake lazima kitekelezwe,hata uchawi alionao Zahara kwa sasa aliurithi kutoka kaa Bibi Zahara tangu akiwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kumi. "Sawa mjukuu wangu" (akawatazama wachawi)"Haya tokeni hapa"(Wachawi wakapotea). Zahara akawaita wale misukule aliokuwa ameenda nao kuchimba mihogo. "Letene hapa hiyo mihogo" Misukule wakaleta furushi tatu zilizojaa mihogo mibichi. "Leo mmechukua shamba la nani.?(lilikuwa swali la Bi Zahara) Zahara akatabasamu " Leo tumeenda kwa mwenyekiti wa kijiji, si unajua shamba lake lina mihogo mitamu" "Safi Sana mjukuu wangu,hii ndio faida ya uchawi,unawatuma misukule wanachimba mihogo halafu unaileta,uzuri hakuna mwana kijiji anayeweza kuiona misukule yangu" (Bibi zahata akawa anajigamba). Misukule wakaiweka mihogo chini. "Haya nendeni kwa wenzenu nitawaita" (Zahara akawa amru misukule wake waingie ndani ya nyumba mbovu iliyojengwa nje) Misukule wakaenda kujumuika na wenzao,Bi Zahara na mjukuu wake wakaendelea kupiga soga. "Vipi Bibi umefikia wapi kuhusu mpango wetu?" "Mpango wetu unaenda vizuri,na mpaka sasa tunavyoongea Hassan ameshapoteza maisha, hapo vipi mjukuu wangu?" Bi Zahara akaachia tabasamu ila Upande wa zahara mambo yalikuwa tofauti, hakufurahishwa na kifo cha Hassan. "Vipi mjukuu wangu kuna tatizo?" Zahara hakumjibu Bibi yake,akaanza kuingia ndani huku akiwa ameuvuta mdomo mbele mithili ya mtu anayejiandaa kupuliza mluzi. ** Nyimbo za msibani ndio zilitaradadi kwenye familia ya Baba na Mama Hassan.Mpaka sasa Mama hassan bado amepoteza fahamu ijapokuwa wanawake wenzie wanampatia huduma ya kwanza kikamilifu. Baba Hassan alikuwa na Baba otieno wakiwa wamejitenga na wanaume wengine. "Pole Sana rafiki yangu" Baba hassan hakuacha kulia,ingawaje ni mwanaume lakini msiba hauna komando,kila alipokumbuka uwepo wa mwanae akazidi kudondosha machozi. "Mungu nimekukosea nini?" "Baba Hassan usimkufuru Mungu,yeye ndiye aliyeiumba mbingu na nchi na sisi tukiwemo,alituumba kwa udongo ni lazima tutarudi mavumbini,hebu vumilia rafiki yangu" (Baba otieno alizidi kumpatia maneno ya kumtia moyo Baba hassan) Baba Hassan akasema kwa sauti iliyojaa ujasiri. "Hawa ni wachawi wamefanya hivi,najua lazima watakuwa hapa, lazima wapo hapa hapa" Baba otieno akabaki mdomo wazi "kuna wachawi hapa?umejuaje?" "Mimi ni mzaliwa wa hichi kijiji,nawajua vizuri wana nzengo wa hapa,nakuambia hivi,wamrejeshe mwanangu ama na wao watatangulia mbele za haki" Baba Hassan hakuwa amekosea ,ni kweli kifo cha mtoto wake chanzo ni wachawi wa kijiji,Bab Hassan anatamba mbele za Baba otieno kwamba muda si mrefu atawatambua wachawi wote waliohusika na kifo Cha mwanae,hakuwa anajua Kama Baba otieno ni miongoni mwa wachawi wanaounda kundi la Bi Zahara. ** Zahara akaingia ndani kwa hasira, akakaa juu ya mkeka ulikokuwa umetandikwa ndani,akavuta pumzi na kuishusha. Bi Zahara akaingia ndani,yeye akawa amesimama huku Zahara akiwa ameketi juu ya mkeka. "Mjukuu wangu kuna jambo gani unawaza?" (Bi Zahara aliuliza kwa sauti iliyojaa upole ndani yake). "Bibi,kwanini mmemuua hassan?" Bibi Zahara akaketi juu ya mkeka ulioisha. "Nisikilize mjukuu wangu,tusipofanya hivyo hauwezi olewa na hassan" "Sasa Bibi nitaolewa vipi na wakati ameshakufa?itakuwaje Bibi?" "Hahahah...kumbe ni hicho tu,tambua Bibi yako anauwezo wa kufanya jambo lolote na likafanikiwa,kifo cha Hassan ndicho kitakufanya uheshimike kijijini,ni amini Mimi mjukuu wangu" "Sawa Bibi nakuamini,ila sijajua mpango wako wa kumuua hassan ni upi" "Hii ni saparayizi mjukuu wangu" Zahara akacheka. "Bibi siyo saparayizi ni sapraizi" Bibi Zahara akarudia tena kutamka neno 'sapraizi' matokeo yake akajikuta akikosea tena. "Saparayazi..saparayizi" Zahara akaangua kicheko mpaka machozi ya Furaha yakawa yanamtiririka,Zahara akatoka nje huku akicheka. ** Angel aling'ang'ania kwenda kumuona Hassan. "Mama naomba mniache nikamuone Hassan,suala la kurudi nyumbani tutalijadili baadae" Angel akaanza kutoka nje,Patricia na mama yake hawakuwa na namna ya kumzuia angel,ikabidi wamsindike kuelekea nyumba ambayo kumetokea kifo cha Hassan. Angel,Patricia na mama yao ,wakaianza safari kwa miguu kuelekea nyumbani kwa akina Hassan,ikumbukwe nyumba aliyokuwa amepelekwa angel kuna umbali kidogo na sehemu aliyokuwa hassan,kwa mila na desturi za huko hauruhusiwi kulala ama kuonana na mke wako kabla ya ndoa kufungwa,ndio maana angel alipelekwa nyumba nyingine na hassan. Wakiwa njiani wanaelekea ulipo msiba,mara ghafla kuna kimbunga kikajikusanya nyuma yao,kimbunga kile kikaanza kuwakimbiza,kila walipoongeza 'spidi' ndivyo kimbunga cha maajabu kiliwakimbiza. Mama mzazi wa Angel na Patricia alipata tabu Sana kuzidi wanae,unene wake ndio unaomfanya achoke wakati wa kukimbia,upepo wa kimbunga ukaendelea kuwafuata nyuma kwa kasi,kila waliposimama na kimbunga kilisimama,wakipunguza 'spidi' na kimbunga kinapunguza. Zahara alionekana akiwa amekaa juu ya mgongo wa msukule mmoja huku anapuliza mchanga aliouweka mkononi,ilikiwa kila akipuliza mchanga kimbunga kinazidi kuwakimbiza angel ,Patricia na Mama yao. Zahara ndio anawachezea ,Furaha yake ni kuwaona wakiteseka wakati wote wataokuwa kijijini Mashene.Binti Zahara akaendelea kuwachezea akina angel,wao walikuwa wanakimbia mbio mbio kuepukana na kimbunga. Kila Zahara anapopuliza mchanga ndivyo kimbunga kilijikusanya zaidi na kuongeza spidi.Leo Mama angel amelazimishwa kufanya mazoezi bila kupenda,ukiwaona wanavyokimbia unaweza dhani wanafanya mashindano ya riadha,mbele alikuwa ametangulia angel,katikati alikuwepo Patricia na nyuma alikuwepo Mama angel. ** Upande wa pili kwa Baba Hassan na Baba otieno. "Rafiki yangu hebu niambie una mpango gani?" Baba hassan akamtazama Baba otieno "Kuna jambo la msingi natakiwa kulifanya,ila utanisamehe ,kwa sasa siwezi kukushirikisha,nitakuambia baadae" (Baba Hassan akaelekea ndani ya nyumba ambayo analala yeye na mke wake) Baba otieno akabaki akiwa anamtazama rafiki yake "Sijui anataka kufanya nini!" (Baba otieno aliongea peke yake) Baba otieno akaelekea kwa wazee wenzake walipokaa. ** Zahara akaendelea kuwachezea akina angel,kimbunga kikaendelea kuwafuata kwa kasi zaidi ya mwanzo.Zahara akatazama macho juu,macho yake yakabadilika rangi na kuwa mekundu,akautazama udongo aliouweka juu ya kiganja cha mkono wake kisha akaanza kuunenea maneno ya kichawi. Maneno anayoyatamka Zahara yana maana kubwa katika ulimwengu wa Giza,maneno haya huwa yanatumika wakati ambao wanataka kutoa kafara, mchawi akiyatamka maneno haya basi mtu atakayemtaja jina atakufa papo hapo,vilevile huwa wanayataja wakati wanataka kumuua mtu ili wanywe damu na kula nyama yake. Zahara amedhamilia kuwatoa kafara Angel,Patricia na mama yao kwa kutumia kimbunga,Zahara anataka kimbunga kiwameze wote wapotelee humo. Zahara hakuwa na huruma hata kidogo, akaendelea kufanya ibaada ya kichawi huku akiwa amekaa juu ya mgongo wa msukule. Itaendelea..... 😈BI ZAHARA NA BABA HASSAN WANA MIPANGO GANI? 😈ZAHARA AMETUMA KIMBUNGA CHA KICHAWI.
@MusNus-bc2rf
@MusNus-bc2rf 7 ай бұрын
👊
@THEDONSIMULIZI
@THEDONSIMULIZI 7 ай бұрын
Imetulia simulizi
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Asante Sana the done sauti ya Radi
@sophiebanga9533
@sophiebanga9533 7 ай бұрын
Nice story
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Thanks,please subscribe🙏
@MariaPatrick-u3p
@MariaPatrick-u3p 7 ай бұрын
❤❤
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
@mariamomran6144
@mariamomran6144 7 ай бұрын
Good
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Shukurani Mariam,endelea kuwa karibu na hii channel mengi mazuri yanakuja,usiache Ku subscribe
@JjjNs-xw5tq
@JjjNs-xw5tq 7 ай бұрын
Moto
@JodaKissana
@JodaKissana 7 ай бұрын
🙏
@NURUABDALLAH-r1k
@NURUABDALLAH-r1k 7 ай бұрын
Mbna sasa mwisho nne😢
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
Mwendelezo utakuwa unatoka hapahapa ,kuanzia ijayo utaipata mwendelezo hadi kumi, endelea kubaki hapa,na Kama bado hauja subscribe ,subscribe ili uwe wa kwanza kuipata
@FatherMadereck
@FatherMadereck 6 ай бұрын
Hii tamthilia imetulia, na mtunzi naye ametulia kwa kweli, naomba iwepo nafasi ya ku download ili ilahisishe kuisikiliza baadaye hata usipokua na mega
@jodastories
@jodastories 6 ай бұрын
OK,option naiweka sasahivi,lakini pia unaweza download kwa kufuata hatua hizi. 1..copy link ya hii simulizi ,nenda ilipoandikwa share kisha copy. 2...ingia vidmate weka hiyo video kisha download. Ukishindwa nichek kwa namba 0748862999(wasap).Ntakuelekeza vyema
@FatumaJumanne-p4d
@FatumaJumanne-p4d 7 ай бұрын
❤❤❤
@jodastories
@jodastories 7 ай бұрын
More❤
@MusNus-bc2rf
@MusNus-bc2rf 7 ай бұрын
👊
@Mellissabahati137
@Mellissabahati137 6 ай бұрын
❤❤
BI ZAHARA (WAONE MISUKULE WAO) PART 2
1:00:05
GO-GO STUDIOS
Рет қаралды 2,7 М.
BI ZAHARA PART 5 {DAWA YA MCHAWI NI HII}
34:41
GO-GO STUDIOS
Рет қаралды 1,4 М.
Lazy days…
00:24
Anwar Jibawi
Рет қаралды 6 МЛН
THE DEVIL WORSHIPER (SIRI YA FREEMASONs)
1:57:47
SIMULIZI FUPI by Simulizi Mix
Рет қаралды 36 М.
SINA CHAGUO ZAIDI YA HILI 10/12 SIMULIZI ZA MAPENZI.
50:36
D Oen Simulizi Fupi
Рет қаралды 1,2 М.
CHUNGU CHA BIBI
2:58:47
SIMULIZI FUPI by Simulizi Mix
Рет қаралды 3,6 М.
BI ZAHARA PART 4(siri ya kwanini unaamka asubuhi umechoka)
27:53
GO-GO STUDIOS
Рет қаралды 1,5 М.
FUPI YA KUSISIMUA: SAFARI YA MVUVI; SIMULIZI
4:43:41
SIMULIZI FUPI by Simulizi Mix
Рет қаралды 204 М.