Dizasta Vina - A father figure (Official Album Intro)

  Рет қаралды 39,454

Dizasta Vina

Dizasta Vina

Күн бұрын

Stream/Download #AFF Intro
Audiomack - audiomack.com/...
Mdundo - mdundo.com/son...
Other Musical contents
Audiomack - audiomack.com/...
Boom play - www.boomplay.c...
KZbin - / dizastavina
Mdundo - mdundo.com/a/2263
Spotify - open.spotify.c...
Apple music - / dizasta-vina
Deezer - www.deezer.com...
Spotify Playlist - open.spotify.c...
Genius - genius.com/Diz...
Connect with Dizasta Vina on social medias
Instagram - / dizastavina
X/Twitter - x.com/dizastavina
Facebook - / dizastavina07
Business: Pan.authentik@yahoo.com
Website - bio.link/dizas...
Lyrics
Natazamwa kama mgongo
Wa kuegewa kama chombo
Nikitegemewa na watoto
Lakini kwa ndani mi' ni mtoto pia
Mtoto wa katikati
Njiapanda kati ya
Ukweli na uongo
Ukubwa na udogo ama
Upofu na uchongo
Ama pumbazo na mwongozo
Katikati ya uhalisia
Na mategemeo
Karibu na jitihada
Mbali na egemeo
Sina hesabu ya mafanikio
Kila kitu ni jukumu na uwepo wangu
Ndio hukumu yangu ya leo
Sina cha thamani nilichorithi
Ila nilichonacho ni kumbukumbu ya simulizi
Na picha nilizokuwa nazo
Nilizopewa na wavuja jasho
Wasakatonge wa mwanzo kwahiyo
Nigawie masikio yako
Macho yalinipa tishio lenye manufaa kwangu
Maana nilishuhudia kufanikiwa na
Kushindwa kwa mashujaa wangu
Lakini shuhuda zilinifunza
Zilinifunza kuhusu Mashujaa
Wa karibu na mbali
Wenye nasibu za ghali
Au watabibu wa kuponya hali
Na nguvu ya kufukuza shali
Za wadhalimu na waharibifu
Wenye visu vikali
Mashujaa walisisimua sana
Lakini wapo kadhaa waliokufa
Na hawakuacha alama
Nilifunzwa kuhusu hawa
Hawa mashujaa walipanda maua
Wakilea vyema yakachipua
Na wengine usingizi ulipowachukua
Wadudu wala mizizi wakafukua
Machache yaliyofanikiwa kukua
Ndege waliyachukua
Na mengine hayakuwa mahala pema
Kwahiyo yalichomwa na jua na kuungua
Oooh hujui walimwengu walisema nini
Kuhusu hawa shujaa wangu walioshindwa
Walisema Kaharibuu
Kwakuwa shujaa kwa walimwengu
Ni yule anayeweza wakati akifanya
Lakini sio anayeshindwa wakati akijaribu
Kwa walimwengu shujaa
Ni yule mwenye nguvu
Asiyetoa chozi wakati wa uchungu
Asiyekosa au anayeonekana mtukufu
Kwa walimwengu ushujaa ni
Kuweza na sio kuthubutu
Kwahiyo wakati sherehe za mashujaa
wao zikipikwa kuchochea
Hadithi za mashujaa wangu
Zilizikwa na kupotea
Kwakuwa mashujaa wangu
Hawakuvaa suti zenye nakshi na kuita
Hawakuwa na viatu vya kung'ara hivyo
Hawakupendeza kwenye jarida
Ni kama walipima ushupavu wa mashujaa
Kwa kuangalia afya za maua
Bila kujua afya za maua sio ubora
Wa anayeyajua pekee
Lakini kuna jua na mvua na ni
Ubashiri wa kujua lini vinakuja
Uhakika ni kesho, kesho yenye giza
Na hakuna anayeitambua
Shujaa wangu alileta mlo mmoja
Kuhakikisha siku haipiti, na aliweka
Tofali Moja wakati wa kujenga msingi
Alifagia barabara alipambana na
Uraibu kama kamali, ulevi na madawa
Ila hadithi yake haikuvutia gazeti
Sio sawa
Ni vile nimeanza kuwa kama shujaa
Wangu nimegundua kuwa sijamaliza kujua
Ni kama nimeanza kulea wakati sikumaliza kukua
Natamani kuwa shujaa mzuri
Lakini nipo hapa kujifunza
Na pa kuanzia sipajui
Sipajui maana maelekezo ni mengi saa hii
Mara jikaze wewe, baba halii
Mara utapoteza nafasi, watu hawatanii
Mara kwanini usifanye kama nanihii
Ona watoto wake wamenanihii
Bahari ya elimu ni pana kuushinda upeo
Kulia matarajio, kushoto mategemeo
Bado najifunza sipo mbali
Ila sijui lini nitakuwa tayari
Inaniwia kuweka kipimo
cha kujua kipimo kiundani
Kupima usahihi wa wito
Ninaposema hadharani
Unawaandaaje watoto kwenda mitaani
Kwa sababu kuliko kuwa mkata maua vitani
Ni bora kuwa mwanajeshi kwenye bustani
Nini maana ya kuwa baba
Ikiwa bado najifunza
Kutosherehekewa nikishinda
Ila kusakamwa nikianguka
Hata nikipendwa au nikichukiwa
Ni sawa ila si vyema nikapuuzwa
Labda ninachelewa ila ni vyema
Nimejua kuwa baba hazaliwi
anaundwa

Пікірлер: 451
@WakujaTech
@WakujaTech 8 ай бұрын
THE STORY BEHIND THIS VOICE👇🏾 There’s a back story kwenye sauti ya intro. Mzee wangu alifariki nikiwa mdogo sana. Mama aliwahi kuniuliza mara moja wakati tunaangalia picha za marehemu mzee wangu, akasema “unahisi mzee angeongea leo na wewe angesema nini?” It was an interesting question. Niliandaa hii intro with that Idea kwamba, kama mzee angepata nafasi ya kuongea na mimi angesema nini kunishauri. Wazo la kuweka sauti tofauti na yangu likaja. Ile sauti inawakilisha umbali wa mzungumzaji na anayesikiliza, inawakilisha utofauti wa dimension kwa mmoja yupo hapa na mwingine yupo mahala pengine. It doesn’t really have to make sense to you. It is personal @DizastaVina
@bensonoloo1388
@bensonoloo1388 8 ай бұрын
This deep connection with life events and putting them on paper, then on sound for us to listen to is why i love your songs bro. Keep giving us more of this ~ legend 👊🏿
@volcanoland9526
@volcanoland9526 8 ай бұрын
SIJAWAHI kuona kwenye comment mtu ana mDiss vina,,,aya like apoooooooo
@manbebo4460
@manbebo4460 8 ай бұрын
😂😂😂😂sawaa tunalike
@msafirifabian2143
@msafirifabian2143 8 ай бұрын
Huyu kashindikana
@volcanoland9526
@volcanoland9526 8 ай бұрын
@@msafirifabian2143 Yan huyu kila wimbo ake naouskliza ad sisimka
@volcanoland9526
@volcanoland9526 8 ай бұрын
@@manbebo4460 unajua bwan me masuala ya kulike comment za watu huwaga sikumbuki ila mtu akiniambia ni like ya dizasta hua sijiulizi mara 2 me ni kulike tu hahahaja
@yoseanjiku6263
@yoseanjiku6263 8 ай бұрын
hakuna kazi mbovu Toka kwa vina ,,,,,,
@nillyjos1203
@nillyjos1203 8 ай бұрын
Song ya dizasita vina kabla sijaisikiliza hua na like kwanza Kisha ndo na comment 🎉
@selemaniselemani591
@selemaniselemani591 8 ай бұрын
Baba kweli hazaliwi anaundwa but nimependa ile line ya kupambana na urahibu wa madawa , kamali na pombe iko poa na vile mashujaa wetu historia zao zinavyo puuzwa na kutupa za kwako ni good thing na nimependa inspiration kuwa yatupasa tupambane na sio kufananishwa na watoto na fulani
@jollityjorgan5920
@jollityjorgan5920 8 ай бұрын
Dizasta hakuna maneno mazuri ya kukusifia ila hii Dunia uliopo binadamu wa kawaida mwenye uelewa wa kawaida n rahisi kukuona wew kawaida, nakugawia masikio yangu Tena na Tena bila ukomo Hadi pale ntakapozima nisipumue Tena.
@user-vm9fz1eg7z
@user-vm9fz1eg7z 8 ай бұрын
Ila uyu jamaa cjui kwnn watu hawamzingatii ila nibonge la kichwa🎉
@alfredkobonga3535
@alfredkobonga3535 8 ай бұрын
Ay 0:29 a wa kwanza mimi leo like zangu sasa
@wakalitz3959
@wakalitz3959 8 ай бұрын
Kama hujalipa pre Oder ya hii albam, unasubiri nini????? Hakikisha tuna support hii talent aisee
@hilaliustheophil1952
@hilaliustheophil1952 8 ай бұрын
Kwa wale wapambanaji kitaa huyu ndo msemaji na mfariji wetu. We need this hard thinking with a lot of teaching sms. Simple things wengi wanafanya. Broo .....
@user-gn5uy8up2w
@user-gn5uy8up2w 8 ай бұрын
Oyaaaah wanangu baba hazaliwi anaumbwa plz kama kuna watu wanamkubali huyu mwamba kushinda mimi agonge like hapa nahitaji nijueh wanaomkubali kaka mkubwa vinaah❤❤❤🎉🎉🎉🎉 upewe maua yako kabla ya mwaka kuisha
@georgeburchard4872
@georgeburchard4872 8 ай бұрын
Kaka maarifa unayotumia Ni makubwa Sana! Sina uhakika hiki kizazi Cha amapino Kama kinakuelewa!
@rajabushedafa6397
@rajabushedafa6397 8 ай бұрын
Kwenye hip hop hatunaga wakwanza Mimi show love Kwa dizasta Kwa kutoa 👍 za kutosha
@Sheckwes092
@Sheckwes092 8 ай бұрын
Hii si ya kuitwa nyombo hii Hini gene pool ci yakutoka chimbo hii This one is legendary….. Will go down to the histOry❤
@yussufkhasim9021
@yussufkhasim9021 8 ай бұрын
I am a father 👨 🎉🎉 kwa ma Baba wote never give up bro 🙏 💪 🙌 we nishuja..😊
@AleckLoina-xb4qc
@AleckLoina-xb4qc 8 ай бұрын
Kuliko Kuwa Mkata Maua Vitani, Ni Bora Kuwa Mwanjeshi Kwenye Bustani👊👊👊
@piussungwa5386
@piussungwa5386 8 ай бұрын
Kuliko kuwa mkata maua vitani, ni bora kuwa Mwanajeshi kwenye bustani 🔥🫡
@Njokaa
@Njokaa 8 ай бұрын
Ningekuwa na kituo cha Radio ningepiga ngoma za dizasta pekee miaka yote
@jolamboi8842
@jolamboi8842 8 ай бұрын
Dizasta vina wapi like jaman 🎉🎉🎉🎉
@gervasscofield
@gervasscofield 8 ай бұрын
Hip-hop is supposed to uplift and create, to educate people on a larger level and to make a change. Hip-hop saved my life, man. It's the only thing I've ever been even decent at. I don't know how to do anything else.
@stevemwachi254
@stevemwachi254 8 ай бұрын
Vina ni shule vina ni profesa..sioni haja yakusoma vitabu vya riwaya nyimbo zako zinatosha kunipa elimu ❤❤❤🔥🔥🔥🔥
@eddiedonald7483
@eddiedonald7483 8 ай бұрын
Nipeni likes zangu comment ya kwanza leo 🔥🔥🔥
@user-xg6gp4ht4g
@user-xg6gp4ht4g 8 ай бұрын
You made it brooo natamani siku mojaa Jamiii ikuelewe more than more na tukakupime iQ yako so mtuu wa kawaidaaa wewe 😂😂greatestiiiiii vina
@asamouramos7391
@asamouramos7391 8 ай бұрын
Ahsante kwa kutoa funga mwaka bro, mpaka saiv nlkuwa nawaza mwakani naenda na goma gn jpya, bro @dizasta-Vina
@twahirsaidi7943
@twahirsaidi7943 8 ай бұрын
Hv watoa tunzo huaga wanaangaliaga vigezo gan ,kama miuziki mwamba alitakiwa awe amebeba tunzo zao zote kwakwel mwamba anaua sana Kila Ngoma.
@Deejay_plannet255
@Deejay_plannet255 8 ай бұрын
Huyu mwamba ni bonge la storyteller wa muda wote anajua sana🔥🔥🔥🔥🔥
@k_voicetv
@k_voicetv 8 ай бұрын
Nimekosa cha ku comment ila bora ni comment tu bro wewe ni more 🔥🔥💫🎤
@albertayubu3377
@albertayubu3377 8 ай бұрын
Akili kubwa Sana imetumika, Hijaniangusha Kwa watu niliowaamisha kuwa wewe ni Bora kuliko Ubora wenyewe. ONYO: INAHITAJI UTULIVU SANA KUMUELEWA HUYU MWAMBA
@Suleiman99
@Suleiman99 8 ай бұрын
Unaniimba mm vinna nahusika kabisa na hii poem
@danielkihombo488
@danielkihombo488 8 ай бұрын
Km mm npo mbeya huku nafaidi madini ya hiki kichwa vzuri hv adi najioonea wivu ,je rafiki wa karbu wa huyu jamaa itakwaje??.,Kiufupi namwonea wivu yeyote ata mweny namba ya huyu mwamba.......More appreciation kamada
@najar825
@najar825 8 ай бұрын
sjui kenya niko mm peke yangu ila nakubali kila unachokifanya BLACK MARADONA💪👊❤
@ajsmainde5138
@ajsmainde5138 8 ай бұрын
ukimsikiliza huyu jamaa, km ni msanii unaweza usiimbe tena😄
@oldskuladimuzabongo8873
@oldskuladimuzabongo8873 8 ай бұрын
😂
@mohamedissa9228
@mohamedissa9228 8 ай бұрын
Nawaona boot camp click(BCC), jed mind tricks( JMT) na Capone and noreaga(CNN). Kwenye ngoma zako DV❤❤❤🔥🔥🔥🔥
@RazaQy
@RazaQy 8 ай бұрын
.....nimegundua kua, sijamaliza kujua, nikama nimeanza kulea, sijamaliza kukua. The king of vina, much respect to you bro
@kilalakaila9762
@kilalakaila9762 8 ай бұрын
Vina inabidi afungue chuo cha rap bongo coz hii nizaidi ya kujua🙌🏿
@josephpeter833
@josephpeter833 8 ай бұрын
Kuliko kuwa mkata maua vitani ni boraa kuwa mwanajeshi bustanini.
@allyntepatz
@allyntepatz 8 ай бұрын
Baba azaliwi anaundwa❤, sisi tuliosoma art tunaweza toa maana hata 100 kwenye msemo huo tu
@timothykaiza327
@timothykaiza327 8 ай бұрын
Vina unaishi mbele ya muda mwanetu.
@paticotz2513
@paticotz2513 8 ай бұрын
Kwann uyu jamaa asijengewe sanamu pale posta aisee
@alikominga6310
@alikominga6310 8 ай бұрын
kwaiyo posta ni sehemu yakuwekaweka vitu visivyo vya msingi ety eeh
@gagalinodenatrick1652
@gagalinodenatrick1652 8 ай бұрын
😮
@mohamedissa9228
@mohamedissa9228 8 ай бұрын
Nilianza kuona ubunifu wako kwenye uandishi wa ngoma zako nikaendelea kuona kwenye dakika 5 za maangamizi nikaja kuona pia ubunifu kwenye dis tracks zako kwa rapcha ila pia nikaendelea kuona ubunifu wako kwenye kolabo ya underrated. Na hapa nipo naendelea kuona ubunifu wako kwenye intro ya hiyo album ya tarehe 6. DV kwenye Kaya. ❤❤❤❤
@user-iv8hn6of7r
@user-iv8hn6of7r 8 ай бұрын
Broda cjawahi ku comment kweny nyimbo zako ila Kwa hili cwez kujizuiia wew ni hadhina Kwa hip hop ya Tanzania 😢
@carlospaul1032
@carlospaul1032 8 ай бұрын
Dizasta tafadhali naomba ulike comment yangu Wewe ni kiumbe kingine kwenye rap arena
@user-yv7dg9or9d
@user-yv7dg9or9d 8 ай бұрын
U are the one in this world 4 my lovely rap style
@kisalaurence6177
@kisalaurence6177 8 ай бұрын
Dah akili nyingi always FATHER FIGURE .. USHAURI ULIOTUKUKA ASANTE DIZASTA VINA 👑
@anoldkivuyohiphopmc1957
@anoldkivuyohiphopmc1957 8 ай бұрын
Men your the head of this game,nawaelewa wengi lakini from now on I respect your work's cause every single you release teach in each line ,broo you're the head of this game and you own ur crown ✌️✌️☑️☑️☑️☑️☑️💯💯💯💯🔥🔥🔥🔥🔥🙅🙅🙅🙅
@user-tu8tb3zq8t
@user-tu8tb3zq8t 8 ай бұрын
Nakubaliana na uwezo wako kaka unajua haipingw
@macumianitha3638
@macumianitha3638 8 ай бұрын
Mmi maskini lakini kuna zawadi yako bro😢😢😢😢😢utaipokea hivohivo
@cellestinelucas165
@cellestinelucas165 2 ай бұрын
we mshenzi me nyoko mbili umetisha😂😂
@mtaaruma
@mtaaruma 8 ай бұрын
Another stone from prof Tungo hujawah tuletea tishu kama wengine kila ukiachia kitu kina heavy weight
@onesjulius3870
@onesjulius3870 8 ай бұрын
Ni muda sasa basata wampe Tuzo ya heshima hata kama vinna yeye hataki ashikishwe tu Street verified ❤
@Dyram_dee
@Dyram_dee 8 ай бұрын
Embu nii_dedicate hii nyimbo kwa vijana wote wanaopambana kwa familia zao za sasa na zijazo. 🙌🔥✊
@nickyvanich6214
@nickyvanich6214 8 ай бұрын
Ngoja kwanza niyasikilize mashauri kutoka kwa nguli huyu makini, suala la comment ntacoment tar.6 hyo 2024. Maana uhh
@fundi_nyata
@fundi_nyata 8 ай бұрын
Elimu isiyofunzwa shuleni! Baba hazaliwi, anaundwa!
@kassioothemiracle1688
@kassioothemiracle1688 2 ай бұрын
Broo big up xana tunajivunia ww kuzaliwa Tziii
@josephrespigi9454
@josephrespigi9454 8 ай бұрын
The greatest rapper 🔥🔥🔥🔥
@juliuschipanha6625
@juliuschipanha6625 7 ай бұрын
The best story teller from panorama authentic
@MaazMunir-hv7xw
@MaazMunir-hv7xw 8 ай бұрын
Umenishinda tabia vina umenifanya leo nimejua kuwa kweli bahari ikichafuka inampima nahodha wa meli kama atakubali kufa au ataongoza kweli . Your are da best in Tz brother
@frankjoseph2984
@frankjoseph2984 8 ай бұрын
Heavyweight mindset, Crinical message to the universe. Extraordinarily literature Homey. .. We need ur sound tone of speech we used to know.
@valencepaul4604
@valencepaul4604 8 ай бұрын
Hili ni darasa tunaendelea kujuzwa ambavyo hatukufunzwa shuleni,,,ni bahati sana kuwa MFUASI wa DIZASTA
@Bongo_gossip
@Bongo_gossip 8 ай бұрын
Kama haujaelewa kitu..nenda kawasikilize wakina Gnako upande juu ya mezaa
@volcanoland9526
@volcanoland9526 8 ай бұрын
Hahahaha jamaa msenge ww😂😂😂😂😂
@Bongo_gossip
@Bongo_gossip 8 ай бұрын
@@volcanoland9526 🙌🏽😂
@XxhamxyyxShha
@XxhamxyyxShha 8 ай бұрын
Nimeanza kulea wakati bado sijamaliza kukua.💪
@Smartkichizi
@Smartkichizi 8 ай бұрын
Oya father iko kichwa shikamoo "kuliko kuwa mkata maua vitani bora kuwa mwanajesh kwa bustan"🙌
@mohamedshabani619
@mohamedshabani619 8 ай бұрын
Nimeanza kulea kabla sijamaliza kukua 😢
@Deadskytz
@Deadskytz 8 ай бұрын
Real hip-hop pillar 🔥🔥
@sportsbiotz
@sportsbiotz 8 ай бұрын
Vina is key to our mind doors...his bars open our mind to new way of thinking
@MosesMwanyema-vq7kq
@MosesMwanyema-vq7kq 8 ай бұрын
Album Bora 2024
@aishaobo6186
@aishaobo6186 8 ай бұрын
Mr vina mm nangoja vidio ya wachezaji wa timu broo
@VeeTechnologies22
@VeeTechnologies22 8 ай бұрын
Nimedownload kwanza kabla ya kuanza kusikiliza, saiv ndo nasikiliza sasa😊
@kingcole60
@kingcole60 8 ай бұрын
Artist with no hater, Vina 🔥
@BenjaminJosephat-js7dd
@BenjaminJosephat-js7dd 8 ай бұрын
Nakubali mwamba
@victorburser1717
@victorburser1717 8 ай бұрын
Huu ubongo sijui unaukubwa kiasi gani jamaa akili kubwa sana
@Stopper_wa_pili
@Stopper_wa_pili 8 ай бұрын
Elimu ya bure na yenye kuleta positivity katika jamii inatoka kwako kaka 🙌🙌tunajifunza vingi kupitia wewe 🔥🔥🔥
@ayubukaduma1017
@ayubukaduma1017 8 ай бұрын
vina tambo liko vema limesimama hakika , lina leta hisia flaniii haielezeki .nasubili mwendelezo
@godblessluvanda9808
@godblessluvanda9808 8 ай бұрын
🎤🎤🎤🎤🎤👑👑👑👑Hip hop of Africa 🌍
@user-wy5sl9ki9m
@user-wy5sl9ki9m 8 ай бұрын
Huna mpinzani kuhusu vina number one Tz
@tabora_boy
@tabora_boy 8 ай бұрын
Aisee akili kubwa Sana🤔
@yusuphisack285
@yusuphisack285 8 ай бұрын
Unaishi kwenye moyo wa mtaa.... unaishi centre... hata ukifa leo hii itaishi kesho Tukutane tarehe 6 🔥🔥🔥🔥🔥
@user-pu4di3sz5z
@user-pu4di3sz5z 3 ай бұрын
Asante d sichoki ndo nazidi kujifunza usiache d tunaishi na wewe mwana kwetu
@JuliusLeskar-js2ot
@JuliusLeskar-js2ot 8 ай бұрын
Kwa walimwengu shujaa ni yule mwenye nguvu
@Chimgege
@Chimgege 8 ай бұрын
Waelewa kuna vina mnaelewa jamaa nini anamaanisha ila Tutafika tu natamani awe raisi ila madaraka yana levya kaka endelea tu kutupa ngoma
@wizzallyxxtentacion2877
@wizzallyxxtentacion2877 8 ай бұрын
D kam D heshima kak hukosei ni za moto kila zikitoka dizasta 👊🏿🌋🌋
@mohamedissa9228
@mohamedissa9228 8 ай бұрын
Dingi kwenye hii Kaya ya hip hop bongo i respect you brother always ❤❤❤🔥🔥🔥
@yusuphnassoro8836
@yusuphnassoro8836 8 ай бұрын
Nina utabiri dizasta stories will be the future of amazing bongo movies that will sell African culture to the world. I see the Art the true Art. I WANT THIS ALBUM IN MY LIBRARY
@user-ei8vm3we2p
@user-ei8vm3we2p 8 ай бұрын
Kuliko kuwa mkata maua vitani , bora kuwa mwanajeshi kwenye bustanii...💪🏿
@erickyemtee5664
@erickyemtee5664 8 ай бұрын
Ukifuatilia hizo tungo na picha utaelewa anachomaanisha vina🎉 Tungo zako ni kali bro
@mohamedissa9228
@mohamedissa9228 8 ай бұрын
Daaah ila vina ni mbunifu Sanaa aseee
@noelfanuel9496
@noelfanuel9496 8 ай бұрын
Hii ktu inafny tareh6 iwe mbal mzee
@Big.JMjaribu34
@Big.JMjaribu34 8 ай бұрын
Haya Tukannuee sasa Jama iii 10k tyu
@sabrenamputa2894
@sabrenamputa2894 8 ай бұрын
Mmenunua album kwa kuanzia tsh 10000 ebu tuchukue jaman
@EnockKyejo-ej4lc
@EnockKyejo-ej4lc 8 ай бұрын
Bg up sana bro kwamana sikuzote hata nguo nzuri hununuliwa kwa wanao kua na hela tu nahata mistali yako tunasikiliza wenye akili mingi tu kamanda
@legawayz6093
@legawayz6093 8 ай бұрын
The music lives forever 🎧 ☺️ Utunzi umelala humu, usipokuwa makini utaona nikitu Cha kawaida ila hii ndo sanaa sasa KWANGU NAIONA AS "POEM" 👏👏👏👏👏 DIZASTA VINA
@user-dz1cq9cl8d
@user-dz1cq9cl8d 8 ай бұрын
Dah nilichojifunza "Bado Nina mengi ya kujifunza" xo unique blood,,,❤
@giftelia5535
@giftelia5535 7 ай бұрын
Sanaa inachosha Kwa sababu wasanii wanajaribu kuficha mambo, wanatufanya tupige puchu kifikra. Vina anaweza kuweka mambo hayana, unaweza kuwajihiana na uhalisia wa mambo Kwa tungo zake chache tu.
@captainb.o.b568
@captainb.o.b568 8 ай бұрын
Another hit mpaka wataelewa tuu kuwa wewe ndiye professor tungo lyrics on🔥🙌
@mesharkctz2374
@mesharkctz2374 8 ай бұрын
Nime miss kuskia distrack kutoka kwa vina
@user-jh3ly6sn1s
@user-jh3ly6sn1s 8 ай бұрын
Unyama kama wote
@EnockKyejo-ej4lc
@EnockKyejo-ej4lc 8 ай бұрын
Afu bro wote tunajua kila kilema kinamwendo wake kwa mtazamo wangu Ni hizi tungo za kimafia ndo zimefana utumie sauti hiyo tunakukubali sana
@khloevibe7569
@khloevibe7569 8 ай бұрын
We jamaa me nikutie moyo usibadilike maana hichi nnachokiona ni kikubwa mnooo MUNGU kakupa endelea kutufunza🙌hakuna kama ww kwa sasa
@gabrielmiatus3886
@gabrielmiatus3886 8 ай бұрын
Hujawahii niangusha mwalimu 🔥🔥🔥✊✊✊
@BAD5IVE
@BAD5IVE 8 ай бұрын
À Father Figure 💥💥💥💥💥💥💥
@nelsonmushi4413
@nelsonmushi4413 8 ай бұрын
Vina rap ya bongo ipo mikononi mwako
Dizasta Vina - Wachezaji wa timu
7:25
Dizasta Vina
Рет қаралды 81 М.
Dizasta Vina - Muscular Feminist
9:05
Dizasta Vina
Рет қаралды 103 М.
when you have plan B 😂
00:11
Andrey Grechka
Рет қаралды 27 МЛН
مسبح السرير #قصير
00:19
سكتشات وحركات
Рет қаралды 11 МЛН
escape in roblox in real life
00:13
Kan Andrey
Рет қаралды 10 МЛН
When Adam Mchomvu discovered Dizasta Vina
2:49
The Diary of Dizasta Vina
Рет қаралды 10 М.
Tribulation
11:27
Dizasta Vina - Topic
Рет қаралды 26 М.
KINYA MISTARI - SINA FT DIZASTA VINA & BOSHOO NINJA
3:08
kinya mistari
Рет қаралды 13 М.
Oka Martin REACTION / Dizasta Vina - Top Shelf
14:26
Oka Martin
Рет қаралды 9 М.
Dizasta Vina - Almasi (Feat Tk Nendeze)
4:39
Dizasta Vina
Рет қаралды 69 М.
Dakika 10 Za Maangamizi-  Dizasta Vina | Planet Bongo I
12:06
EastAfricaRadio
Рет қаралды 724 М.
Dizasta Vina - Chupa moja ya ziada
5:04
Dizasta Vina
Рет қаралды 41 М.
Dizasta Vina - Hatia V
8:16
Dizasta Vina
Рет қаралды 116 М.
when you have plan B 😂
00:11
Andrey Grechka
Рет қаралды 27 МЛН