The best and most redpilled rapper in african 🔥🔥🔥 A Gem this one
@deograsiasnada88853 жыл бұрын
hizi tungo zitumike zitumike rasmi kwenye fasihi huko mashulen na swali lake liwe la lazima kwa wnafunzi wote.. content ipo mkao ur genius bro
@nikompemba36553 жыл бұрын
Kabisa kaka
@dizastavina3 жыл бұрын
Lyrics Dear boys dear… men Ni sisi wasichana kina dada, mabinti na mama zenu, Tunaongea kutoka upande wa chini, upande mbali upande kutoka usawa wenu Upande nilipo msichana kuna hitilafu ‘So’ sikio lako thabiti ni ushindi kwangu Ninayotaka kusema hapa sio siri katu Ili ujue nina vingi vya ku-offer kabla ya mwili wangu Kwa miaka mingi nimeishi gizani Gizani kwenye baridi na miba mingi nyikani Eneo uliotaka niishi ni eneo kandamizi Na bahati mbaya we’ ndo’ mchoraji wa hii ramani Ramani inamwonyesha binti kama chombo cha mapenzi Msindikizaji mtoto tegemezi Ramani isiyojua vituo, Isiyojua tunaweza kuwa marafiki bila kuvuana nguo Dear boys, dear men Mngeelewa mngeiweka fikra sahihi Kama sanaa jinsi inavyozalisha fasihi Mi’ ni mlezi ukinivika mi’ umeivika jamii U-gentlemen sio kulipa mgahawani Umeshapitwa na wakati, Hainisaidii kunifungulia mlango nikifika kwenye gari Nifungulie fikra nitafakari Dear boys, dear men Tumekuwa tegemezi maana mmeficha mbegu Nani wa kuipigana vita yetu Umbali kati yetu utakuwa mkubwa milele Maana si ni wahanga wa mifumo mliyoiunda wenyewe Nikijaribu kusoma nabaki bure Maana unajali mwili wangu, ndo’ maana sitaki shule Kila nikienda popote wanaomba ngono Labda niwe changudoa to the fullest At least I’ll get paid Hata sisi tuna life too And the world doesn’t revolve around you Nipo tofauti sikupenda, na tena Unaponichezea fahamu kuwa ninazeeka mapema Shujaa unakumbukwa mzazi sikumbukwi Na kwanini kuwa msafi sio haja kwako Au kutembea kifua wazi ni kujiamini nikitembea mimi ni nusu uchi I wish ungejua pride yako nayo sumu I wish ungejua kuwa uanaume sio nguvu I wish ungejua kuwa binadamu hajakamilika Mwanaume aliyekamilika anatimiza majukumu I wish ungejua kuwa na mimba sio haya I wish ungejua mwanamke kuwa kichwa si vibaya I wish ungejua kuwa upendo nao una nguvu kwahiyo mwanamke akitongoza mwanaume si malaya I wish ungejua kuonyesha fear sometimes, it’s okay It’s okay kulia sometimes I wish ungejua uongozi hauoni jinsia si Tatizo mwanamke kuongoza njia sometimes Mifumo mliyoianzisha ina maisha Na chenye maisha kinazikwa Kwahiyo ipo siku mwanamke atasimama Na vita tunayopigana tutashinda Inasikitisha hamkui kihisia, japo mnakua kiakili Natamani … natamani mngejua kuwa inauma sana kuwa namba mbili kwenye kila nyanja, Ego ni power ila iogope Maana ni upanga unaokata pande zote Ngoma nzuri ngoma nzuri haitavuma milele Ukitumia ubabe vibaya utakuvunja mwenyewe Hadithi ya mwanamke alimshawishi Adam kula tunda Iliandikwa na wewe, Sijui Delilah alichukua nguvu za mumewe akaziuza Iliandikwa na wewe Upande wangu wa hadithi haujasikilizwa Pengine hautasikilizwa hasirani Maana ulianzisha shule akasoma mwanaume Mwanamke nikabaki nyumbani Dear boys, dear men Hamtakaa kwenye kilele Maana kilele ni kuwa mama Mi’ ni kichwa sio wewe ungekuwa kichwa Mtaani kusingekuwa na single mothers Lini mtaacha kutuita mademu Au labda mwite demu mama’ako Ukiona hauwezi naomba niheshimu kwa maana heshima inaanza kwako Na haja ya maelewano iko hapo I mean… ipi salama ya kichwa cha familia bila Mkono wa kuosha macho? Najua tupo tofauti Na tofauti yetu itabaki, itabakia hivyo milele Ila naomba usinichukie nielewe Dear boys, dear men Ni sisi wasichana, kina dada, mabinti na mama zenu Tunawasilisha kutoka upande wa chini upande wa pili Upande mbali kutoka usawa wenu Dear girls, dear Women Ni sisi kina kaka, kina baba, wanaume machizi wenu Tunaongea kutoka upande wa juu, upande wa mbali Upande uliowekwa na asili yetu Upande wenye mafungu yenye ulanguzi Upande wenye uthubutu na maamuzi Upande wenye machozi jasho na damu Uongozi upako ufahamu, upande usio na uhuru na uchaguzi Upande uliofanya wanaume tutengwe na tunu Tutengwe na tunu, Upande ambao pengine kuishi wewe ni ngumu Upande ambao asali yake ni kilele cha sumu Upande ambao haushabikii tija ya upendo au furaha au amani Kama hauangalii pima utagundua upande niliosimama mimi ni ngao ya jamii nzima Uanaume sio ushindi ni jukumu Uanaume sio rizki ni hukumu Ungejua kwanini wanaume wana msongo wa mawazo pengine ungefurahia udogo wako Dear women , dear girls Mmekuwa chombo cha ngono Maana mmetufanya chombo cha fedha Kama nguo hazitabadili mishono Hatuwezi kuwa marafiki bila ngono nawaeleza Mnapoona padogo pana taswira ndefu Kiasi haujui si ndio tuliopigana vita yenu Hata mkiamka mmekuwa wanaume leo Mtagundua kuwa jinsia sio cheo Wapendwa tukishindana mtashindwa Hata mkishinda ushindi wenu hautalindwa Kama ambavyo kila mmoja anatumia choo chake Kila mmoja a-play role yake na awe bingwa Dear women Ndoa sio mafanikio Kuna wengi wanakonda maana ndoa zao sio Ndoa ni mwiba usijivune Ukiipata niamini unaweza kukamilika bila mume Dada baki shule bila elimu utateseka Ukitegemea urembo ipo siku utazeeka Kama ukiweka mwili wako hisani Ukizeeka tutajali ulichonacho kichwani ‘Skiza’ hata wanaume tuna doubts too And this world doesn’t revolve around you Tuna stress zinatufunga na tena Kazi zetu ni ngumu ndo’ maana tunakufa mapema Kama unahisi upo huru umepotoka Hauwezi kuwa huru wakati umelipiwa posa Dear women It’s okay kuwa namba mbili Majukumu sio mashindano acha kukalili It’s okay kumlea mwanaume asiye na kazi Ukaendelea kumuheshimu bila kumshusha hadhi Mbona sisi tunalea wanawake masikini wamekata ringi na bado mtaani hatutatangazi Mwanaume ana jukumu la kujenga msingi? No, msingi unajengwa na elimu Kwa mfano nani anayekubali kucheza uchi kwenye videos? Jiheshimu nikuheshimu Urembo pia ni power, ila ni power na iogope Maana ni upanga unaokata pande zote Ngoma ya uzuri haitovuma milele Ukiutumia urembo vibaya utakuvunja mwenyewe I wish ungejua unachowaza ni muhimu, ukifanyia kazi na kuwa wa kwanza si’ majibu I wish ungejua kwamba asili imenipa umwamba Nikulee, kukulea wewe ni msaada si’ wajibu I wish ungejua tuko tofauti hata utunge dini hauwi mwamba kwa kumweka mwanaume chini I wish ungejua kuwa kichwa ni hukumu Maana hakuna kinachotisha kama jukumu Wangapi tumelelewa na hao single mothers Maskini and we turned out just fine Maybe idea ya kuacha kujali mtoto sababu Baba mjinga ingeachwa far behind Tunasubiria uhalisi ubadilike Labda uhalisia haubadiliki huu Labda ni wakati wa kukubali ili yaishe kwamba Mtoto ni wa mama na baba ni rafiki tu Lini mtaacha kutuita madanga ma-sponsors? Ndio, niheshimu nikuheshimu nitaacha wewe Ukiona imetosha, au sio? Najua tuko tofauti Na tofauti itabaki hivyo milele Usinichukie nielewe Dear girls, dear women Ni sisi kina kaka kina baba, wanaume machizi wenu Tunawasilisha kutoka upande wa juu, upande mbali uliowekwa na asili yetu
@snashbwaii1703 жыл бұрын
Daaah we mzee una andikaga saa ngapi🙆♂️ au una andikia baharini
@shabaniadolph73673 жыл бұрын
Dear.....,.
@anoldjulius93523 жыл бұрын
Dah, af tuzo bora ya hip hop anapewa flan, maaaaaninaaa
@shariphidrissa47963 жыл бұрын
Hii IQ level nyingine kbs
@ahmedsdk67363 жыл бұрын
Dizasta Vina
@rolandkingia29753 жыл бұрын
Huyu masta Ndio the Best Hiphop story telling in East Africa
@karimchindema98233 жыл бұрын
Kazi nzuri,,, at least nimepata kitu Cha kufundishia wanafunzi wangu wa literature
@ahmednuhu2386 Жыл бұрын
ningekua raisi ninge shinikiza hii ngoma itumike kama mashairi mashuleni kwaajili ya kujibia mitihani angalau tungepata watoto wanao jitambua.......hili shairi kwangu halichuji kila siku naona jipya
@beatbyrich2891 Жыл бұрын
Imeachiwa mwaka mmoja uliopita lakini Vyombo vyetu na wanahabari Hawana muda wa kuzungumzia tungo hii!!!!! Nasikitika kuona vipaji kama hivi Vikiwa underrated 😢. Hii simulizi ungetengenezea na kitabu. Salute kaka wachache tunajua
Hii ndo maana ya hiphop kuzungumzia changamoto na maisha ya kila siku kwenye jamii yetu dizasta vina👏👏👏🙌
@29WavesTV3 жыл бұрын
Kazi nzuri inahitaji vichwa timamu kuelewa jamaa anamaanisha nini. Pia watu tufanye kusupport kazi nzuri ka hizi utunzi murua!👏🏻👏🏻💥🔥
@razackyahaya77983 жыл бұрын
Uwezo... Muandiko... Dizasta OG nakubali kaka
@patrickmartinmsuya3673 жыл бұрын
Inauma sana kuona Mziki wa maana kama huu haupewi promo mtaani tumejawa na singeli
@micochazi91533 жыл бұрын
Si tatizo mwanamke kuongoza njia sometimes
@rafeageefilan55443 жыл бұрын
DIZASTA nusu mtu nusu rap mashine UWEZO WAKO MKUBWA MNOO😇👏👏👏🙌
@yusuphnassoro88363 жыл бұрын
Dizasta Aandike kunyoosha hii Tz. Alipoachia Ndoano nikadhani kabahatisha, niliposikia Hatia1-4 nikawa fan, alipoachia wimbo usio bora nikawa AC kabisaa now this guy is becoming my role model in writting ✍✍✍.
@nickman44353 жыл бұрын
Siku utasikiliza tatuu ya asili na The lost one utachanganyishwa na akili za huyu shujaa bro
@yusuphnassoro88363 жыл бұрын
@@nickman4435 Agreed, jamaa ni Genius alaf no matusi no wanawake walikaa uchi yani chikichiki rap na elimu
@gabrielflavianus50333 жыл бұрын
Umechora sana mzee! Umebalance vyema kabisa ,big up!!
@yuzhoshaban53673 жыл бұрын
Kuanzia sasa we ndio best rappper, best lyricist, best emcee, best artist, best best best....
@Mina-mr3ol3 жыл бұрын
Hujawah kukosea tunaokufaham na kufatilia kaz zako tunajua ila unatutesa sana hit kama hz unachukua muda kutoa unatufanya tuwe bored jitahd kuleta kaz kaka naamin uwezo wako
@johnjenks95193 жыл бұрын
Yean natama ngoma zako zote zingekua zinafika angalau views m1 had m10 sema ndo ivo wabongo tuanafkilia vitu kwa ulahisi ila mungu yupo vina d zasta
@topranking0133 жыл бұрын
Pande zote mbili zimeguswa vilivyo Big up
@LugomboMaKaNTa3 жыл бұрын
Uandishi na ghani za ulimwengu wa juu sana ✊🏿💪🏿
@jodyntilayoungpapo91893 жыл бұрын
Ninayotaka kusema hapa sio siri katu....d hustle✊
@athumanihamadi66193 жыл бұрын
What a talent. Uyu jamaa ni best story teller angekuwa mambele huyu angeimbwa kila uchao
@deogracious84742 жыл бұрын
👊👊
@immanuelmwaipopo16053 жыл бұрын
My favorite artist in the planet
@Essau-r8f3 жыл бұрын
DIZASTA VINA Nusu mtu Nusu Rap Machine. We proud of U Homie
@kelvinkeita3192 жыл бұрын
Moja ya binadam wachache kabsa dunian ambawo huwa wanaletwa ili kuwafundisha watu jisi ya kuishi Big up sana br dizasta heshima kwako daah nmejiona mwenye dhambi kubwa sana kwa kuwadharau mabiti kubeza uwezo wawo na kuamin wawo ni chombo cha stareh tu hi fkira au mitazamo ya namna hi kwenye jamii inabidi iishe kabsa hongera sana br mungu akubariki ww na uzawo wako
@isl71133 жыл бұрын
Atleast in the midst of all these bubble gum artists bado kuna mwamba bado amestick kuspread knowledge tena bila kuwa biased na jinsia ....well balanced content ....much love Ninja
@snashbwaii1703 жыл бұрын
Hapa bongo hakuna kama wewe mzee we ni hatari zaidi ya dangerous
@kaminyogediallo73383 жыл бұрын
Tunatumia vitabu vya kina Wole Soyinka wakati hii ni fasihi tosha toka nchini kwetu, Disasta we ni zaidi ya kawaida.
@alexselias94203 жыл бұрын
Pengo la King Zilla limezibwa kikamilifu kabisa na huyu mwamba
@johannesjoseph74963 жыл бұрын
Bongo hajatokea lyrical mcee ka dizasta..
@alexselias94203 жыл бұрын
@@johannesjoseph7496 huyu mzee baba wa moto kinoma noma ni ile anakata mawimbi balaa
@pasimillinga2623 жыл бұрын
Ipo siku tu dunian itakuelewaa wee jamaa🙌🏾
@Ogtydan3 жыл бұрын
Naahidi kuja KU comment Tena hapa 2025 🎶🎵
@winfredykahwili15133 жыл бұрын
Hivi dizasta huu unyama Huwa unauchimbua wapi🤸🏼♂️🤸🏼♂️🔥🔥🔥🔥
@giftelia55353 жыл бұрын
Mwimbaji si mtu huyu, huyu ni mtume zawadi ya Mungu kwa jamii..
@twamanjatwasini42003 жыл бұрын
Ukiskiliza hizi ngoma unatamani ata siku moja usije kufa daah! Unavyo🗣 nichezea tambua kuwa nazeeka mapema
@nyikumbarasylvester85053 жыл бұрын
Huyu jamaa hua anakula nn?kiukwel dizasta vina ni extra odinary👐💪
@Mr.Kibabu3 жыл бұрын
Hakika Hip Hop ipo kwenye Mikono salama ya Dizasta
@HidayaSwai7 ай бұрын
Napenda kusoma haduthi mba limbali dizasta umetoa uwelevu wangu kupiia macho sasa natambua kwa kusikiliza asante d napenda busala zako katika utunzu wako mfano ulipo sema muite dem mama yako vijana wengi huwathalau wana wake mara nyingi mwana ume akishindwa kufanya jambo fulani huitwa mwanamke hii inathihirisha wanaume walio wengi huwa thihaki au kuwatharau wanawake daaaaaa
@BUSHASHASWITCH3 жыл бұрын
Love from bushashacomedian ubabe ukiutumia vibaya utakuangusha chini mwenyewe thanks very massage
@isakakipalule9749 Жыл бұрын
Ngoma mbili kwenye ngoma moja
@godwillmawere55333 жыл бұрын
Mwanaharakati katikati katika kusemea suruali na sketi Uwe na maisha marefu saana
@dickmlawa88433 жыл бұрын
Nishasikiliza mala 20 nabado napenda ngoma isiishe fungua shule dizasta
@OMYUUN3 жыл бұрын
Dahhh hatari sana kila mstari umeandikwa ukasimama. Dizasta
@zolomwashinga90743 жыл бұрын
Ngoma kali haujawi feli broo kuandika unajua sana ila sikutegemea kuwa naweww utakuwa ni yule mtu asiye jibu dm za mashibiki wake
@alphamartin99473 жыл бұрын
Kaka nakukubali adi naumwa. ''kukulea wewe ni msaada sio wajibu'' kunahisia umeziamsha apa 👊👊👊
@Miatv_tz3 жыл бұрын
Du du du du huyu ndio msanii pekee anaepaswa kukabidhiwa bendela ya nchi.
@maschalqaalqadivu63933 жыл бұрын
Jamaa unajua sana ngoma Kali hatarii oya mwamba we nimshindi
@philimonambilikile66453 жыл бұрын
Dizasta my brother jah bless you walio juu yanajifanya hawajuhi umuhimu wako kwa game letu leo na kesho nakukubali
@saidijuma93863 жыл бұрын
Kazi nzuri brother hii zaid ya wimbo usio bora
@Alegria_doPovo3 жыл бұрын
Dizasta Vinaaaaa the vertelaaa🔥🔥🔥🔥 Tatizo ngoma za hivi hazipewi promo
@geraldyona55973 жыл бұрын
Best rapper in Tz💫....... unaandika snaa brz kudos kwako
@omkamasamson90503 жыл бұрын
hii kazi kubwa ....ubongo ulifanya kazi sana big up sana
@cobwaafri Жыл бұрын
hii ngoma naisikiliza alafu naisikiliza tena madini ni mengi sana humu
@el-hajjel-shabbaz80783 жыл бұрын
Nerd, we jamaa ni hatari sana asee👏👏👏👏👏
@johannesjoseph74963 жыл бұрын
Uliposema nikiwaka naweza mgeuza fid akawa sajina sikuelewaga.. Ila adi leo nimegundua bongo hakuna mwandishi mkali zaidi yako. Salute bro.. Stay real.. Kitu kizuri ujitaftia njia yake chenyewe.. Soon raia wote wa tz na east africa watakupa heshima na 💰zako
@kurudimzizima79953 жыл бұрын
Inafikirisha sana hii. Kwa hiyo cha msingi kwa pande zote mbili ni kujiheshimu na kutimiza wajibu. Wanawake na wanaume tuko tofauti na daima hatutakua na usawa, huo ndo ujumbe wako?
@jumaibrahim42973 жыл бұрын
Dah sijui hata niandike nini..! Ila Dizasta ni mtu na nusu 🔥🔥
@col.mayungamayunga20393 жыл бұрын
Sina neno kubwa Zaid ya Asante kwa burudani
@chipdady903 жыл бұрын
My brother mwenyezi MUNGU akupe umri mrefu...uzid kutupa vitu vzuri nakukubali San.shabiki yako kindaki ndaki hap.
@juliasmariki71583 жыл бұрын
Kwann awakup heshima yako wakati wew ni mungu..
@viceboirapper11213 жыл бұрын
Namkubali hilii jamaaa had so powaa
@zascotz36623 жыл бұрын
broh yaan unajua mpaka unaboa una ngoma mbaya ata moja
@flolafaustine37913 жыл бұрын
Umetutendea haki Sana kina dada na kina mama Kazi kwenu wanaume msikilize na mchukue Hatua Dizasta ni Shule
@TanzaniaTaiji Жыл бұрын
No one like you brother... ni wewe unayeifanya HipHop.. kwa Africa wewe ni Namba 1... SIJUI UNA ELIMU GANI.
@GoodPeopleOfBiafra3 жыл бұрын
Wewe jamaa makini sana kiuhalisia na kiifupi mwanamke ndiyo akili yenyewe kabisa kimaisha hapa na huko tunako tokea sisi wanaume tukiwanao kwa makini hakuna kitakacho kushinda hata kuunda ndege na gari utaweza tu
@albanitarimo97213 жыл бұрын
Genius of this generation ma main man Dizasta vina much respect broo
@EYVMedia2 жыл бұрын
Wasanii wengi tunaowaskia hawatupatii haya Mafunzo😭😭😭😳😳😳 very deeeep content and messege!!! Keep on pushing and change our society!!! Mama ndiyo mzazi wakweli Baba ni rafiki tuu😂😂😂😂😂 i just saw my son Alvin.
@thelivingwelltv63993 жыл бұрын
Hivi huyu jamaa mbona ana balaa la kijini kabisa,inamaana kweli hawaoni uwezo huu wa hatari alionao!!?Man i love hip hop na hii ndio hip hop,Dizasta yo genius bro
@ussiussi34133 жыл бұрын
Hongera bro kwa uandishi mkubwa kama huu.
@Regnard999 Жыл бұрын
Women as second class citizens!! Asante kwa kunikumbusha kozi niliyoisoma chuo kikuu katika Literature i.e "Feminism"- UDSM😍😍
@jumannefaustin60363 жыл бұрын
Kwa huu utunzi,, Ni wazi inaonesha ulkuwa unawakimbiza sana darasan wakat unasoma..
@brownbreezzy41363 жыл бұрын
Dizasta Vina we jamaa una madini sana..
@johnjenks95193 жыл бұрын
Dah naumiaa sana jins unavofanya kazi nzur afu baazi ya watu wanashindwa kukuelewa nakubali sana kaz zako broh
@aboumogrey65533 жыл бұрын
MC mwenye mabalaa 🔥🔥🔥
@anthonymgogo26513 жыл бұрын
Uliletwa kwa sababu man keep on grinding!
@josephmmbando28994 ай бұрын
Vina hatari sana we jamaa! Unaandika babuu…. my son should come and see this verses! 🔥
@selemaniselemani5912 жыл бұрын
daahh bro popote ulipo leo ndio mara yangu ya kwanza kusikiliza ngoma ya hip hop mpaka machozi yananitoka daahh broo unajua sanaaaa
@priscaonesmo1416 Жыл бұрын
Rafk yangu kanitumia huu wimbo siku wa woman's day ,imebidi niutafute niuskilize vzur ,mbali na kuburudisha huu wimbo unatufunza pia
@vianneysospeter22353 жыл бұрын
Dizasta vinaaa the story teller mtu makina watu timamu hawapewi airtime tupe shule mwamba
@udambwi61762 жыл бұрын
Masta nakubali Sana kila idala upo ,,,kama kuna mtu anandugu yake ni mlokole au anasali Sana mwambie akasikilize KANISA Ya huyu jamaaa 🙏🙏🙏
@dinocastico84952 жыл бұрын
Una fikra pana sana zisizo kadirika kwa kipimo ila mzani wa mtu mwenye fikra pia. Hakika wewe ni muandishi ambae uandishi wako waweza tumika katika fasihi mashuleni . Kiufupi una fikra pana sana
@twamanjatwasini42003 жыл бұрын
IPO SK mziki wa hip hphop utatawala kama uko duniani kwamaana saiv viongoz waliopo hawaupi promo lakn one dy hatuach kuskiliza
@jelitochale43103 жыл бұрын
Cjawai jutaaa kusikiliza ngoma zakoo
@joachimjohn64443 жыл бұрын
Sema huyu Jamaa aisee.. 🔥🔥 haya bana, tuache watu waendelee na hizo za nifinyie kwa ndani badala ya kufungua masikio upande huu, Dizasta ni Shule ya bure ada ni masikio yako tuu
@stiffmenake47003 жыл бұрын
Lifetime music .. ni historia kwa vizazi 🔥🔥🔥
@bryanabwaku71873 жыл бұрын
This is ART in its purest FORM. Damn!!
@neko98693 жыл бұрын
Muscular feminist# 👊🏿✌🏿💪🏿# THE VERTELLER 🔥🔥🔥🔥
@KennyGaudence7 ай бұрын
Olaaa hii Ngoma nishaisikiliza 100times kiukweli kinachotuua wanaume ni hii kauli mbinu haki sawa
@salimkigarimbwe49117 ай бұрын
This is my best song from dizasta apa mzee kaumiza kichwa sanaa😮 🇰🇪🇰🇪
@Bk_melodyTz3 жыл бұрын
mzee umeua sana 🙌🏾🙌🏾
@davidmwandumusya1293 жыл бұрын
Ngoma kali.... Ila wabongo tuko bize na bia tamu... Sijui tumelogwa nanani?
@OVMiNG3 жыл бұрын
The Verteller, endelea kuokoa hiki kizazi chenye fikra potofu✊✊ wewe sio rapper tu bali ni GENIUS
@promramson14783 жыл бұрын
Sijawahi juta ku subscribe account yako ...man nashindwa nisemeje.. ila .. you so gifted in short words
@jundabyabdul14783 жыл бұрын
Sanaa ndani ya akili yenye mantiki👍👍👍
@diofpinto75202 жыл бұрын
brother disasta sina mengi ya kusema,nakukubali mno.hakika mungu amekuchagua kutetea na kuelimisha jamii
@Katapa-jr3 жыл бұрын
KING of story teller DIZASTA VINA 🙌
@rockerz5043 жыл бұрын
Hizi ngoma ziingizwe kwenye Syllabus ya upande wa Fasihi 💉
@dullyboyka59183 жыл бұрын
Dizasta Vina.. Mtunzi bora..we ni fundi brother
@kibonahenry71393 жыл бұрын
Mwamba unajua na unajua sana
@saidgawawa85192 жыл бұрын
Huyu rapa mbona naanza kumkubali..hivi! Disasta ww ni msani hatari Tena tishio kwa Kwa hii hip-hop game.bro uko sawa vinoma zaidi ya kamusi tunayoisoma.big congrats 👏