Рет қаралды 249,203
ILAHI KARIMU TAKABALI DUA | KHADIJA AKTHAM
🖋 QASWIDA IMETUNGWA NA ALHABIB HASSAN BADAWY JAMALULEIL (ALLAH AMRAHAMU)
🎬 PRODUCTUON - ALIHSAAN RECORDS
1) Wewe ni mwenye tabia adhwimi
Ilahi amemwambia mtumi
Katika qur'anil karimi
Inna kala3laa khulukin adhimi
2) Illahi alimu sote watuyuwa
Na yetu muhimu yote waelewa
Wewe ni karimu mwingi wa zipowa
Ilahi karimu takabali dua
3) Twakuomba wewe usiomethali
Sisi utokoe kwa tumwa na ali
Dhiki zitatue zote fil hali
Ilahi karimu takabali dua
4) Kwa wako rasuli ulomtauwa
Tunatawasali dua tukitowa
Zitengeze hali utupe afuwa
Ilahi karimu takabali dua
5) Yalo tutatiza ndiwe mtatuzi
Kiondoshe kiza ambacho huuzi
Tupe muangaza upesi na 3ezi
Ilahi karimu takabali dua
6) Utupe umri utupe afiya
Na mambo mazuri ukitufanyia
Tuishi kwa kheri pasina udhiya
Ilahi karimu takabali dua
7) Sisi na zijana furaha pamoya
Kulla la maana tukiwatendeya
Wao kulingana nasi kuwayeya
Ilahi karimu takabali dua
8) Kwa zetu juhudi na niaze njema
Ni hatuna budi ww kukwegema
Umetuahidi tupe kula mema
Ilahi karimu takabali dua
9) Rwabi tufungue hizi pingu zako
Rwabi zitatue kwa rehema zako
Sote tutongoe shukurani zako
Ilahi karimu takabali dua
10) Nazituvumie pepo za baraka
Na utukifie kula heka heka
Tuyasikilie mema tulotaka
Ilahi karimu takabali dua
11) Utufutahie futaha za kheri
Utukusanyie kula lilozuri
Sote tulivae taji lenye kheri
Ilahi karimu takabali dua
12) Rejesha furaha twalokua nazo
Na njema buraha kula tutakazo
Tue tuna raha hatuna mikazo
Ilahi karimu takabali dua
13) Na majumba yetu yahifadhi yote
Na heshima zetu uzitunge kote
Tupe zema zitu rwabi situate
Ilahi karimu takabali dua
14) Na hawa zijana wetu twakwambia
Rwabi ni amana tumekuatia
Wape kulingana na kuongokea
Ilahi karimu takabali dua
15) Kwa wako sayyidi tunatawasali
Wako muhammadi swahaba na ali
Saada suudi tupe filhali
Ilahi karimu takabali dua
16) Zetu ajisadi utuhifadhie
Na yetu miradi ututengezee
Muovu hasidi asikurubie
Ilahi karimu takabali dua
17) Badiru ing'are ya mwezi kamili
Tuteze tuture kwa mema mithali
Naisitukere hali wala mali
Ilahi karimu takabali dua
18) Wewe ni mueza ilahi wayee
Rwabi wapee enzi nao watengee
Kulala lakuudhi uwaondoshee
Ilahi karimu takabali dua
19) Yafute matata nadhiki zapuke
Mtu kitukuta tuna taambaki
Mitaji tukita yote iitike
Ilahi karimu takabali dua
20) Yapoe maradhi haya tulonayo
Kula lakuudhi utokoe nayo
Yote sibaadhi uyondoshe hayo
Ilahi karimu takabali dua
21) Rwabi wanusuru wasiungulike
Kula lakudhuri ya rwabi lepuke
Wote wape nuru hata watosheke
Ilahi karimu takabali dua
22) Na yako salamu ikifuatia
Madamu hamamu ametughania
Ladha ya ilimu tukiisikia
Ilahi karimu takabali dua
23) Rwabi wasamehe walotangulia
Uwape na raha waliposhukia
Ziwe kula nuru zikiwang'aria
Ilahi karimu takabali dua
24) Na sote jumla tulohudhuria
Tupe kula mema yakitushukia
Tuondoke hapa yote kutimia
Ilahi karimu takabali dua
25) Nasi tulingane kwa sote pamoya
tuafikiane kwa moyo mmoya
matunda tuvune furaha afiya
Ilahi karimu takabali dua
26) Sisi twajuhudi tupe taufiki
dua twaradidi nasi hatuchoki
wewe ni wadudi tupe njema haki
Ilahi karimu takabali dua
27) Wanafundi rwabi nao waokoe
Kwa masomo yao rwabi watatue
Na walimu wao watuze watue
Ilahi karimu takabali dua
28) Na hawa walimu tusikizanao
Yatoshe yatimu matilaba yao
Wewe ni karimu tuza nyoyo zao
Ilahi karimu takabali dua
29) Na umswalie wako mukhutari
Na ala wangie swahaba wa kheri
Utungarishie yake jauhari
Ilahi karimu takabali dua