Nuhu hakuwa anakarabati safina, bali alikuwa anajenga chombo kipya kisichokuwepo. Yesu katika kujenga Safina alibomoa neno la uongo na kuweka neno la kweli la Mungu ili ajiletee kanisa safi lisilo na mawaa. Kanisa hilo sio lile lililokataa ukweli, bali wanafunzi wapya wa Yesu waliokubali ukweli. Watengenezaji hawakufanya marekebisho ya mafundisho yaliyopotoshwa na kanisa, bali walilikemea kanisa upotofu wake, na kanisa lilipokataa kuondoa mapotofu ndipo watengenezaji walifanya umoja na wale waliokubali ukweli na hivyo likawa kanisa la Mungu kama vile Yesu alivyofanya kuchukua wanafunzi wapya. Kanisa si suala la jina la dhehebu linalokataa ukweli, bali linaloukubali ukweli wa neno la Mungu, ndilo Yesu alisema wawili watatu wanaokusanyika kwa ajili ya neno lake (jina) na yeye Yesu anakuwa kati yao. Kanisa ni jukwaa la ukweli wa neno, sio jengo au jina fulani tukufu. Nyakati zote kanisa likipotoka huwa halikubali kukosolewa, na huwafukuza na hata kuwaua wanaolikemea upotofu wake. Ndipo baba wa uongo huwaweka viongozi wa kutetea mafundisho yake potofu ili kuyalinda yasing’olewe na mtengenezaji yeyote. Viongozi huwa watumishi wakali wa kulinda kiti cha ibilisi kanisani humo na huku wakilinda vyeo vyao wakitetea mapotofu na kupinga ukweli maana wakiukubali ukweli wataondolewa zao - Matendo 7.45 Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. 47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? 48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? Kanisa likikataa ukweli ndipo Mungu huupeleka ukweli kwa wengine watakaukubali ndio huwa ndio kanisa la Mungu lililojitenga mbali na wale wakaidi -- Matendo 13:45-52; 19:8,9 45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. 46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. 47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. 48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. 50 Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. 51 Nao wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio. 52 Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu. 19.8 Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu. 9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi,akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tirano. Kanisa lolote hata lingeoza kiasi gani lazima litabakiwa na waaminfu wanaoamini kanisa hilo badala ya kuwa waaminifu kwenye ukweli wa neno la Mungu, watakuwa wana wivu sana kwa kanisa, wala si kwa neno la kweli la Mungu.
@jacksule7557Ай бұрын
Mbwana alistahili nafas ya makam
@jacobmalase10604 жыл бұрын
Mungu awe nasi na akutie nguvu PR nime barikiwa
@pmpgospeltv68824 жыл бұрын
Amina Jacob Malase
@josephkirimi54532 жыл бұрын
Kanisa la Mungu halijapoteza mwelekeo wala halitapoteza kamwe. Watu hukonfuse kanisa la Mungu na ndini za watu. Kanisa la Mungu haliwezi kuitwa jina lingine SDA. SDA ni SDA na kanisa la Mungu ni kanisa la Mungu.
@gabrielsaelie8091Ай бұрын
Unabii unasema hivi miaka inavyosogea mbele, dini zote zitarudi kuwa na imani moja ya ukatoliki wa roma . Kwamba Mungu (Uungu) ni, UTATU MTAKATIFU wa mungu baba, mungu mwana na mungu roho mtakatifu. Huu ni uongo mkubwa wa Lusfer wa kujiiniu yeye aabudiwe kama Mungu. Soma Isaya 14: 13 Anayestahili kuabudiwa ni Mungu Baba na Yesu Kristo peke yake. Uongozi wa SDA kupitia GC una naendelea kuvutwa zaidi kueleke RC na miaka inavyosonga tutakuwa hatuna ujajiri wa kukemea opotofu wa RC juu ya ukweli wa Mungu wa Mbinguni. Soma Daniel 7: 1-19
@josephkirimi5453Ай бұрын
@@gabrielsaelie8091 Unataka kuniambia hata ndini yako itakuwa kwa huo muungano wa imani moja.
@precieuxwalina85332 жыл бұрын
Mungu atufunze zaidi 🙏
@evaristussirocha74373 жыл бұрын
tujifunze tabia ya Yesu kirsto
@kusakabuga2824 жыл бұрын
Somo limeniponya Amina
@janemokaya9353 Жыл бұрын
Excellent
@rebeccaomondi4914 жыл бұрын
Mungu atusaidie
@stephaniecelestine79902 жыл бұрын
Que Dieu vous bénisse abondamment . j'aime ❤️❤️❤️❤️😋😋