Рет қаралды 2,650
KANYE WEST na MKEWE BIANCA WACHAFUA HALI HEWA GRAMMY AWARDS WATIMULIWA BEYONCE AMTAJA MUNGU SANA..
Kanye West na mke wake, Bianca Censori, ambaye inadaiwa walifunga ndoa ya siri baada ya kutengana na Kim Kardashian mwaka 2021, walitimuliwa kutoka katika ukumbi wa Tuzo za Grammy 2025 usiku wa kuamkia leo, Jumatatu, Januari 3, 2025. Hii ni baada ya kuripotiwa kuhudhuria hafla hiyo bila mwaliko rasmi na kutokana na mavazi ya nusu uchi aliyovaa Bianca kwenye zulia jekundu, jambo lililoibua mshangao mkubwa ulimwenguni kupitia mitandao ya kijamii na televisheni.
Bianca, mwanamitindo machachari mwenye umri wa miaka 30, ambaye mara kadhaa ameibua mjadala kwa mitindo yake tata ya mavazi, alivalia vazi la rangi ya ngozi lenye matundu makubwa, ambalo liliacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi. Aidha, aliripotiwa kutovaa nguo za ndani, hali iliyowashangaza mashuhuda waliokuwa katika Red Carpet ya tuzo hizo maarufu duniani, zilizofanyika katika ukumbi wa Crypto.com Arena, Los Angeles, Marekani, jana Jumapili, Februari 2, 2025.
============================================================
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 739 750910), ( +255 783453136)
⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_y...
⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globa...
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusiv...
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/gl...
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx