KILIMO CHA AZOLLA |Jua jinsi ya kupanda,kuvuna na kulisha AZOLLA|

  Рет қаралды 4,620

MKULIMA SMART TV

MKULIMA SMART TV

Күн бұрын

JINSI YA KUZALISHA AZOLLA KWA CHAKULA CHA KUKU
Kilimo cha Azora; Jinsi ya kuandaa AZOLLA, huongeza Protin na Vitamin kwa mifugo yako
Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji/Chotara na Kilimo cha Azolla
JINSI YA KUZALISHA AZOLLA KWA CHAKULA CHA KUKU. Habari Ndugu Mfugaji popote pale ulipo, jifunze jinsi ya kuzalisha azolla kwa chakula
MMEA WA AZOLA. Azolla ni aina ya magugu(green argae) yanayostawi juu ya maji.Na ufanana na mmea kama ukoka wa majini.Huu ni mmea ambao
JINSI YA KUZALISHA AZOLLA KWA CHAKULA CHA KUKU
kilimo cha azolla tanzania
AZOLLA
Azolla ni aina ya blue green algae ambayo huweza kulimwa na kustawi vizuri katika mabwawa,mito, madimbwi na mitaro inayotuhamisha maji kwa muda mrefu kazi yake kubwa hufyonza nitrogen kutoka kwenye hewa pia hukua haraka sana katika maji yaliyotuama.
Faida za Azolla
1. Hutumika kuongeza nitrogen kwenye udongo kwa kutumika katika utengenezaji wa mbolea vunde au kuyafanya kama matandazo shambani
2. Hutumika kama chakula cha mifugo kwasababu ina kiwango kikubwa cha protein 25%-30% hutumiwa na ng'ombe, mbuzi, kuku, nguruwe
3. Huongeza uzalishaji wa maziwa kwa ng'ombe asilimia 15-20
4. Pia hutumika kama tiba ya maji kwani huweza kuyafanya yaweze kutumika kwa muda mrefu inawafaa wale wenye mabwawa ya umwagiliaji
5. Huwasaidia wakulima na wafugaji kupunguza gharama za mbolea na chakula cha mifugo yao
5.Huongeza kipato/faida kwa wafugaji na wakulima
Kilimo cha AZOLLA katika eneo dogo la square mita 18 kina futi 1.5 ambapo unaweza kuvuna AZOLLA ya kula Kuku 100 kila siku.
MAHITAJI
1. Mbolea ya ng'ombe kilo 27-30
2. Maji
3. Udongo
4. Mbegu ya AZOLLA (culture) kilo 3
5. Mbolea ya kiwandani (single/tripple super phosphate) gram 90-100.
HATUA ZA KUFUATA KTK UPANDAJI
1. Andaa bwawa lenye ukubwa wa square mita 18 kina futi 1.5
2. Jaza udongo kwenye bwawa lako kwa kina cha 10cm
3. Weka Mbolea ya ng'ombe kwa kuisambaza juu ya udongo kilo 27-30
4. Weka Mbolea ya super phosphate kwakuirusharusha bwawani ili isambae juu ya Mbolea na udongo.
Walishe Kuku wako Chakula cha Azolla
5. Jaza maji kwenye bwawa lako kufikia kina cha 10-15cm kutoka juu ya udongo,samadi na Mbolea
6. Ondoa leya itakayokuwa imetanda juu baada ya kumimina maji, kisha acha bwawa litulie kwa muda wa masaa 12-24.
7. Panda AZOLLA yako kwa kumimina bwawani(3kg).
8. Weka kivuli juu ya bwawa lako ili kuzuia mionzi ya jua kupiga moja kwa moja bwawani(direct sunlight).
9. Subiri kuvuna baada ya siku 15 kwa Mara ya kwanza baada ya hapo utakuwa ukivuna kila baada ya siku 2-3 kwa zaidi ya mwaka.
UTUNZAJI WA BWAWA
1. Ongeza Mbolea ya super phosphate kila wiki gm 90
2. Hakikisha bwawa lako haliishiwi maji
3. Kivuli kisipungue kwenye bwawa lako.
Asanteni kwakusoma maandishi haya, ELIMU HAINA MWISHO penye mapungufu karibu tuboreshe ili tuweze kupunguza gharama za chakula cha mifugo yetu.
ZINGATIA: Si kila AZOLLA inafaa kulishia mifugo zipo zilizofanyiwa utafiti.
NAMNA YA ULISHAJI
Chakula cha Azolla unaweza ukawapatia mifugo kwa namna mbili.
1. unaweza ukawapatia kwa kuchanganya na vyakula vingine kwa kuweka azolla kilo 50, pumba kilo 25, na kilo 25 za chakula cha madukani/ ulichochanganya mwenyewe ili kupata kilo 100
2: unaweza ukawapatia Chakula cha Azolla tu bila chakula kingine, na hii hufanyika kwa Kuku wanauchunga hasa wa kienyeji.
SUGECO Tanzania
#mkulimasmart
#shambadarasa

Пікірлер: 5
@uzungupoint
@uzungupoint Жыл бұрын
Niliwauliza kuhusu uchanganyaji wa Azolla,pumba na chakula cha dukani kama mmevyoelekeza kwenye description. Majibu yenu ikawa hakuna ufanisi na matokeo mazuri kwa ukuaji wa kuku(kuongezeka uzito) kwa kutumia formula hiyo ya 50%(Azolla),25%(Pumba)&25(Commercial feeds). Naombeni formula sahihi ndugu zanguni, Ahsante.
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART Жыл бұрын
Kwasababu haya ni majani hayana uzito.Unaweka Kama kirutubisho
@uzungupoint
@uzungupoint Жыл бұрын
@@MKULIMASMART Ahsante sana kwa majibu, kwahiyo formula ipi yafaa kutumia hapo?
@mwanatz5980
@mwanatz5980 Жыл бұрын
Asanteni
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART Жыл бұрын
Karibu
AZOLLA NI NINI? FAIDA ZAKE KWA MIFUGO NI ZIPI?
10:06
AGRI SMART TV
Рет қаралды 506
Incredible Dog Rescues Kittens from Bus - Inspiring Story #shorts
00:18
Fabiosa Best Lifehacks
Рет қаралды 35 МЛН
Angry Sigma Dog 🤣🤣 Aayush #momson #memes #funny #comedy
00:16
ASquare Crew
Рет қаралды 48 МЛН
拉了好大一坨#斗罗大陆#唐三小舞#小丑
00:11
超凡蜘蛛
Рет қаралды 16 МЛН
Upandaji wa Azolla Kwaajili ya Chakula cha Kuku
8:19
Changamkia Fursa
Рет қаралды 14 М.
UZALISHAKI WA VITUNGUU
10:08
TAHA ONLINE TV
Рет қаралды 7 М.
Jinsi ya Kutunza Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji
8:19
Changamkia Fursa
Рет қаралды 254 М.
How to plant azolla / easy way to cultivate azolla
4:29
Creative Junior
Рет қаралды 81 М.
KILIMO CHA AZOLLA |mbegu ya azolla na jinsi ya kulisha mifugo azolla|
3:07
Azolla Farming / Azolla Cultivation | How to grow Azolla in HDPE Pond
4:26
Discover Agriculture
Рет қаралды 217 М.
How To Make Compost | IN 10 DAYS
13:49
Urban Gardening
Рет қаралды 1,8 МЛН
Incredible Dog Rescues Kittens from Bus - Inspiring Story #shorts
00:18
Fabiosa Best Lifehacks
Рет қаралды 35 МЛН