Рет қаралды 34
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu Kanda ya Geita Kelvin Mhina amesema mashauri zaidi ya elf 8 sawa na asimilia 94.2 yamesikilizwa na kukamilishwa kwa mwaka 2024 ikiwa ni moja ya malengo waliyojiwekea ya kumaliza kesi zote kwa wakati na kwa viwango vya juu zaidi.
Jaji Mhina ametoa kauli hiyi katika Kilele cha maadhimisho ya wiki ya mahakama Nchini ambapo katika mkoa wa Geita yamefanyika katika viwanja wa Mama Samia mjini Geita huku akisema ahadi waliyojiwekea kwa mwaka jana lilikuwa kuwafikia wateja wote kwa wakati.
Kwa uapande wake Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka waandishi wa habari kuandika habari za kesi za madai kwa uwazi bila kuogopa, kwani atahakikisha analinda usalama wao.
Leo Februari 3, 2025 ni kilele cha maadhimisho ya wiki ya mahakama Nchini, ikienda na kaulimbiu isemayo, “Tanzania Ya 2050: Nafasi Ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu Ya Dira Ya Taifa Ya Maendeleo”.