Рет қаралды 51,348
QURAN NI SHIFAA
Quran ni muujiza Allah alimuonyesha Mtume wake Muhammad (S.A.W.) na ni baraka kwa ubinadamu. Quran sio muongozo tu kwa wanadamu bali Allah (Subhanna wa taallah) ameifanya kuwa njia na tiba ya kimwili, kiroho na ya kisaikolojia ya aina zote. Mola wetu alituumba amesema wazi kwamba maneno yaliyoopo ndani ta Quran ni “Shifaa” (tiba) kwa wote; tiba aina hii inaweza kusababisha muujiza kwa matatizo aina yote. Na hii imetajwa katika vitabu vingi vya sunna cya kiislamu .
Na katika imani ya muislamu, Quran ni nia ya tiba na mente kuria ni Allah (Subhanna wa taallah) pekee. Hata unapokwenda kwa daktari au mtaalam wa afya, yeye atakupa dawa ama anafanya upasuaji, lakini anayetibu ni Allah (Subhanna wa taallah) pekee.
Kuisoma Quran ama kusikiliza tu, itakupa utulivu. Katika hadith ya Abu Huraira (Radhi Allahu Anhu) inasema, wanapokusanyika watu katika nyumba ya Allah (Subhanna wa taallah) kuisoma katibu chake, basi utulivu huwateremkia, na rehema huwazunguka, na malaika pia huwazunguka, na Allah (Subhanna wa taallah) huwataja kama wale walio miongoni mwake.
Tukizungumzia aina zengine za tiba, Uislamu hauja zuia matumizi ya tiba zinazopatikana kupitia dawa na sayansi. Na tiba aina hizi zina ziliungwa mono katika masomo ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W.) ambaye pia yeye alizitumia kwa karachi tofauti na kuwashauri wafuasi wake kufanya hivo. kwa hiyo pia kutukia tiba za kiasili pia tipo fatica uislamu.