Рет қаралды 384,699
(Mataifa yote ya ulimwengu
Yatakusujudia ee Mungu (Mungu Baba) *2
Mema uliyonitendea Mungu wangu ninashukuru
Jana leo nimeamka kesho sijui itakuwa vipi
Ninashukuru Mungu wangu leo
Na nyimbo nzuri ninaimba ili kesho nayo niwe salama
Nazo sifa zako, nitangaze pote } *2
1. Uamkapo asubuhi ndugu yangu, umshukuru Mungu,
Kwa jinsi alivyokulinda usiku wenye giza tororo,
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha.
2. Ufikapo safari yako ndugu yangu, umshukuru Mungu,
Kwa jinsi alivyokulinda kwa ajali za barabarani,
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha.
3. Shikaneni mikono sasa yote muinyanyue juu,
Semeni kwa shangwe na mbwebwe maneno haya kwa furaha,
Ameweza, Bwana Mungu kweli ameweza, ameweza.