Рет қаралды 3,924
Mathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Yesu alimwita awe mwanafunzi wake mwanzoni kabisa wa huduma yake ya hadharani. Kwa hiyo mambo mengi anayoyaelezea aliyashuhudia kwa macho yake mwenyewe. Anaanza kwa kueleza kwa kirefu kuhusu kuzaliwa kwa Yesu na Bikira Maria, kubatizwa kwake na kujaribiwa kwake nyikani. Yesu alikuja akihubiri juu ya Ufalme wa Mungu ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika Ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Yesu. Mathayo ameyagawa mafundisho ya Yesu katika sehemu kubwa tano: Maadili, Kueneza Habari Njema, Mifano, Ushirika na kuja kwa Ufalme wa Mungu. Sehemu ya Mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza juu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, na agizo alilotoa kwa wote wanaomwamini kueneza Habari Njema ulimwenguni kote.