Рет қаралды 4,239
Barabara tisa jijini Dar es Salaam, zitakuwa zinafungwa kwa muda ndani ya siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 wakati ambao misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika itakapokuwa inapita.
Pia, bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.
Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema kutokana na ugeni huo, barabara hizo zitafungwa kuanzia leo.
Amezitaja barabara zitakazofungwa kuwa ni Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi.