Рет қаралды 3,077
Washington. Watu wote 67 wanahofiwa kuwa huenda wamefariki katika na ajali iliyohusisha ndege ya Shirika la Marekani namba 5342 iliyogongana Helkopta ya Jeshi la Marekani kisha kutumbukia ndani ya Mto Potomac jijini Washington nchini humo.
Shirika la Habari la CNN, limeripoti leo Alhamisi Januari 30,2025, kuwa hadi sasa zaidi ya miili 30 imeopolewa kutoka ndani ya Mto Potomac, ambao hata hivyo sehemu kubwa ya maji yake yameganda na kuwa barafu kutokana na hali ya hewa inayolikumba taifa hilo.
Helkopta hiyo aina ya ‘Sikorsky H-60 Black Hawk’ inadaiwa ilikuwa inaendeshwa na wanajeshi watatu waliokuwa kwenye mafunzo ya kijeshi kwenye kambi iliyoko karibu na eneo hilo.
Maseneta wa Majimbo ya Kansas ni miongoni mwa viongozi wa Serikali waliofika eneo ilipotokea ajali hiyo karibia na Uwanja wa Kitaifa wa Reagan nchini humo huku wakieleza kuwa kinachoonekana eneo hilo kinatisha.
Kwa mujibu wa Maseneta wa Jimbo la Kansas, Jerry Moran, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Usafirishaji wa Anga, Sayansi na Usafirishaji Ardhini katika Jimbo hilo amesema jitihada za kuopoa miili zinaendelea huku akidai zinarudishwa nyuma kutokana na kuganda kwa maji ya mto huo.
Seneta mwenzake, Roger Marshall, amesema hadi sasa takriban watu zaidi ya 60 wanahofiwa kuwa huenda wakawa tayari wameshafariki huku miili zaidi ikiendelea kuopolewa.