Рет қаралды 7,031
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeweka hatua tano za kisera ili kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza viwango vya riba ikiwemo kuondoa sharti la uzoefu wa kufanya biashara kwa angalau miezi 18 kwa waombaji wa biashara ya wakala wa benki. Hiyo ina maana kuwa sasa muombaji wa biashara ya wakala wa benki atatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa au namba ya Nida. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne Julai 27, jijini Dodoma, Gavana wa BoT, Prof. Florens Luoga amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha sehemu ya amana za mabenki kinachotakiwa kuwekwa benki kuu