Рет қаралды 46,721
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kikristo dhehebu la Sabato wameiomba Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na mhe, Rais Samia kuanzishwe ukaguzi huru dhidi ya baadhi ya Watumishi wa dhehebu la Sabato wanaohusika na matumizi mabaya ya fedha na mengineyo ndani ya kanisa.
Hayo yamebainishwa leo na Mchungaji Mstaafu wa makanisa ya Wasabato Kenan A. Mwasomola wakati wa mkutano na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akisema lengo ni kuondoa changamoto na mikwaruzano katika makanisa ya Sabato na kuongeza amani na furaha.
" Kupitia malalamiko mbalimbali tuliyowahi, Kwa sasa tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani na Serikali yake sikivu, Kupitia Mamlaka zake kuanzishwe ukaguzi huru dhidi ya wabadhirifu wote na wachukuliwe hatua kali" Amesema Mwasomola.
Aidha Mchungaji Mstaafu Mwasomola amewasihi Waumini wa Dini, Watanzania kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu kwani ndio silaha kubwa ya kupata maendeleo katika nchi yetu na kuachana na tamaa hiyo itasababisha kuvunja amani na utulivu nchini.