MKANDARASI SIHOTECH ENGINEERING COMPANY LTD NA AMJ GLOBAL MULTI CONTRACTORS CO LTD WAKABIDHIWA MRADI

  Рет қаралды 351

NJB TV NEWS

NJB TV NEWS

20 күн бұрын

MKANDARASI SIHOTECH ENGINEERING COMPANY LIMITED NA AMJ GLOBAL MULTI CONTRACTORS CO LTD WAMEKABIDHIWA RASMI KAZI YA KUJENGA MRADI WA MAJI WA THAMANI YA ZAIDI YA BIL 5.2 KIJIJI CHA ITIPINGI NJOMBE
MKANDARASI AKABIDHIWA KUJENGA MRADI WA UMWAGILIAJI WA BILIONI 5.2 ITIPINGI NJOMBE
Tume ya taifa ya umwagiliaji imemkabidhi mkandarasi kazi ya ujenzi mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Itipingi halmashauri ya wilaya ya Njombe ambao utagharimu zaidi ya shingi za kitanzania bilioni 5.2 ambao awali ulijengwa kwa gharama ya shilingi milioni 400.
Akizungumza kijijini hapo na wananchi mbele ya viongozi wa serikali wa mkoa wa Njombe wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Antony mtaka mhandisi wa umwagiliji mkoa wa njombe Machage Mwema amesema baada ya usanifu wa pili wa mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa baina ya serikali na mkandarasi kutoka kampuni ya Sihotech Engeneering Company ltd na Amj Global Multi contractor co ltd hapo June 24 mwaka 2024 jijini Dodoma.
Ameeleza shughuli ambazo mkandarasi huyo atafanya kwa kipindi cha miezi 14 ya ujenzi wa mradi kuwa ni Pamoja na kukarabati miundombinu iliyojengwa kwenye ujenzi wa awali iliyochakaa , kundeleza na kujenga mfereji mkuu, kujenga mifereji ya umwagiliaji,kujenga Barabara za kuzunguka mashamba,ujenzi wa madaraja ,vivusha maji , kujenga Barabara kutoka eneo la mradi mpaka kijijini kwaajili ya kusafirisha pembejeo na mazao na kujenga ofisi ya mhandisi wa umwagiliaji.
Amesema pia kutokana na ukubwa wa mradi serikali itanunua gari moja kwajili ya kuhudumia mradi Ampapo pia amesema kazi ya ujenzi huo inaanza baada ya siku 14 baada ya mkandarasi kukabidhiwa kazi na kuwa mradi huo unatraji kuwahudumia wakulima 417 idadi ambayo inaongezeka kutoka 77 ya mradi wa awali wanufaika wakiwa kutoka vijiji vya Itipingi, Kiumba na Malombwe kutoka halmashauri za makambako na Njombe.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Njombe kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima wa vijiji vinavyozunguka mradi ikiwa ni Pamoja na kupima mashamba na viwanja,kuandaa teknolijia za kisasa za kilimo Pamoja na kuandaa masoko ya uhakika wa mazao yatakayo zalishwa kutoka eneo la mradi.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha itipingi Mtaka amewaasa wananchi kuutunza mradi huo kwa kuacha kupeleka mifugo katika eneo la mradi huku akionya vijana kuacha wizi wa vifaa na uvivu kwa vija wanaojihusisha na michezo ya kamali.
Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha itipingi wakiongozwa diwani wa kata hiyo ya Igongolo Isaya Myamba wameishukuru serikali kwa kutoa fedha za kujenga mradi huo kwa mara ya pili na wameeleza kiu yao ya kunufaika na mradi kwa kuzalisha mazao ya mbogamboga kwa wingi.

Пікірлер
Опасность фирменной зарядки Apple
00:57
SuperCrastan
Рет қаралды 8 МЛН
ODM Leadership in Kenya Kwanza Government.
43:38
SpiceFM
Рет қаралды 87 М.
MCHIMBA VISIMA ATOBOA SIRI  UPATIKANAJI WA MAJI KWA HARAKA
10:16
🔴HAPA NA PALE KUTOKA ARUSHA, 28 Julai, 2024.
ITV Tanzania
Рет қаралды 3
DAY BREAK | Ruto picks Raila's Men [Part 2]
1:11:05
Citizen TV Kenya
Рет қаралды 135 М.
WANANCHI KATA YA UTALINGOLO WAPATIWA ELIMU YA UKATILI MTANDAONI
21:18
DEREVA AKUTWA  AMEFARIKI KWENYE GARI AKIWA NA  JIKO LA MKAA
11:38
NJB TV NEWS
Рет қаралды 2,1 М.
DAY BREAK | Ruto picks Raila's Men [Part 1]
19:16
Citizen TV Kenya
Рет қаралды 137 М.