Рет қаралды 3,450
Swala la unywaji pombe haramu limekuwa changamoto kubwa humu nchini huku serikali kupitia maafisa wa usalama ikijitahidi kupambana nalo. Lawrence Rop mzee mwenye umri wa miaka 65 na ambaye alinusurika kifo baada ya marafiki wake watano kufariki dunia baada ya kushiriki pombe haramu katika kaunti ya Nandi basi amejitosa katika kuwahimiza watu katika kaunti hiyo kuacha pombe haramu na kuokoka. Katika mwezi wa Julai watu zaidi ya 12 waliaga dunia baada ya kushiriki pombe haramu katika kaunti hiyo. Mwanahabari wetu Gatete Njoroge ametuandalia taarifa hiyo