Nahitaji ushauri kwa walokuwepo njee ya nchi na kutaka kufanya biashara tz
@maishamax11 ай бұрын
Hii itategemea kama ushawahi kufanya biashara kabla au laah, lakini niruhusu nijikite zaidi kwenye haujawahi kufanya kabla. Kwanza kabisa, biashara inaweza kuwa ya bidhaa au ya huduma lakini ya bidhaa ndio bora zaidi kwa jamii yetu. Somo la biashara ama ujasiriamali ni gumu kufundishika kwa sababu linahitaji vitendo zaidi, lakini kuna mambo ya msingi kuzingatia; 1. Tenga mtaji kulingana na kiwango cha hatari unachoweza kukimudu ili kama mambo yataenda tofauti na matarajio, usipoteze kila kitu na uwe na sehemu ya kuanza imara zaidi kutokana na mafunzo uliyoyapata. 2. Fanya utafiti kujua soko linahitaji bidhaa gani, hii ni hatua muhimu sana na utapataje taarifa hizi. Tembelea mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, JAMII FORUMS ambapo kuna makala nyingi sana za watu wanazoshare kuhusu karibia kila biashara utakayoweza kufikiria (wewe sio wa kwanza) 3. Subira ni muhimu, lakini kasi ni muhimu zaidi kwenye biashara kwa sababu itakupa maoni juu ya njia gani zinafanya kazi kwenye kukuza biashara yako na utafanya marekebisho mapema. 4. Fanya kazi na watu wazuri, hii inajumuisha jamaa zako ambao umeamua kuwashirikisha, lakini pia supplier wa bidhaa zako, yani kiufupi watu wote ambao wanahusiana na biashara yako UMAKINI MKUBWA UNAHITAJIKA. 5. Biashara ni matangazo, hakikisha unabobea au unatafuta mtu aliyebobea kwenye sekta hii, biashara katika zama hizi inahamia mtandaoni ni muhimu kuwa imara hapa. Ninatumaini nimekujibu walau kwa uchache, lakini ungana nasi hapa kuna masomo mengi yanakuja kuhusu mafanikio katika biashara. Ahsante.
@Abdulrahmanhassan1811 ай бұрын
Mtu mmoja aliwaikusema kwamba, tunaweza kumla tembo na kummaliza ikiwa tutamkatakata vipande vipande. Ahsante sana kwa elimu
@maishamax11 ай бұрын
😄 hakika, umeweka summary vyema sana.
@Abdulrahmanhassan1811 ай бұрын
@@maishamax hahaha pamoja sana
@Valentinekainy10 ай бұрын
Good
@maishamax10 ай бұрын
Thanks 👍
@iddyjm256011 ай бұрын
Nakubal brother umetish ww ni mwalim mzur san
@maishamax11 ай бұрын
Shukran sana Kaka mkubwa 🎊🤝
@hemedimuna140011 ай бұрын
Brother nakuelewa 🎉 nikitimiza ninachokifanya nitakutafuta nikulipe hata Asante
@maishamax11 ай бұрын
Karibu sana Kaka, tuendelee kupambana hatua kwa hatua.