Рет қаралды 35,738
Wafilipi 2
5Kwa hiyo iweni na nia iyo hiyo ndani yenu kama ilivyokuwa ndani ya Kristo Yesu. 6Ambaye alikuwa yuna namna ya Mungu, hakuona kuwa sawa na Mungu ni unyang'anyi. 7Lakini alijiangamiza mwenyewe, akitwaa namna ya mtumwa, aliyefanywa kwa sura ya wanadamu; 8Naye alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila Jina; 10Ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la walio mbinguni, na walio duniani, na walio chini ya nchi, 11na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.