Salama Na NAPE NNAUYE SE6 EP15 |ASKARI WA BRIGEDIA PART 1|SendTip MPESA LIPA NO 5578460

  Рет қаралды 26,956

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
ASKARI WA BRIGEDIA
Mbele ya macho ya wengi Nape Mosses Nnauye ni kama SIMBA, anatisha, amejaa, anajiweza na anajitambua na kutambua kile akifanyacho na yake yote anayoyasema na kuyafuatilia. Na kwenye macho ya wale wa karibu yake Nape ni yote hayo na zaidi ni mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa wale wa karibu na moyo wake, mcheshi, anapenda watu na ni rafiki wa kweli, yule rafiki mmoja ambaye haijalishi kukoje ila yeye ndiye ambaye atabaki na wewe mpaka mwisho, na atakuambia ukweli pale panapohitajika.
Mimi na yeye ni mtu na mdogo wale ambao wamepishana kama miaka minne hivi, huwa tunawasiliana na kuongea tunapokutana, tunaheshimiana na kuaminiana pia. Ila kwa respect ili tuweze kumpata kwenye mazungumzo haya tuliamua kumtumia mdogo wake Kipenzi anayeenda kwa jina la Bimdo ili hata kama alikua na mambo mengi kiasi gani, au ratiba yake imebana ki vipi, basi kwa wawili sisi angefanya linalowezekana ilimradi atufurahishe, na tulifanikiwa 😄.
Baba na mume na Kaka na Kiongozi kwa watu wake wa Mtama, Nape ni moja ya nguzo imara za Chama Cha Mapinduzi, naamini mpaka leo bado iko hivyo, kipindi cha uchaguzi wa Mwaka 2015 ndo tulimuona zaidi, wakati Chama chake pendwa kilipokua kinakabiliwa na upinzani wa mkubwa kutoka kwa vyama vyengine vya Siasa. Nape yeye ndo alikua mstari wa mbele wa kupanga mashambulizi na mipango sahihi ya kuweza kupata mgombea sahihi ambaye Chama kingemsimamisha na kuweza kupata dhamana kutoka kwa wa Tanzania zaidi ya milioni 55 ambao kwa hamu tulikua tukingojea kutambua jina na mtu ambaye Chama kingempa dhamana. Haikua mechi ndogo Ila kama tunavyofahamu sasa imebaki story tu. CCM walimsimamisha Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli na mambo mengine mengi yakaanzia hapo.
Sasa hayo mambo mengine mengi yaloanzia hapo ndo moja ya sababu nyingi zilizotufanya sisi tutake kuongea na Nape, akiwa imara na alojaa tabasamu yeye hakua na hiyana kujibu maswali yetu mengi ya kutaka kujua mawazo yake juu ya mambo mengi ambayo kama Taifa na yeye kama mwanasiasa tulipitia. Kuanzia jinsi CCM ilivyoshinda uchaguzi, teuzi, kutumbuliwa, issue ya aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kipindi hicho, mambo ya kutolewa silaha hadharani, issue ya yeye kwenda Ikulu kuomba msamaha, miaka 6 ya JPM na Tanzania kama taifa na mueleko wake, niamini nikisema humu yote tuligusia na yeye alitujibu.
Nape ni mmoja ya watoto wa Marehemu Brigedia Mosses Nnauye, mmoja wa watu imara sana wa nchi hii, pia tulitaka atuambie mahusiano yake na Marehemu Mzee wake, kama kuna lolote amejifunza kutoka kwake na kama yeye ndo alikua chachu ya yeye kuwa anafanya ayafanyayo sasa (kutumikia wananchi wake wa Mtama) na alituelezea kwa kirefu tu juu ya wasifu wa Mzee wake.
Kuna mahusiano yake pia na Marehemu Ruge Mutahaba, ukaribu wake na January Makamba na Zitto Kabwe, events za miaka minne mitano iliyopita zimemfunza nini hasa? Majibu yote ya maswali tele tulokua nayo, Nape alitupatia. Yangu matumaini nawe uta enjoy mazungumzo haya kama sisi tulivyo enjoy.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪KZbin Link bit.ly/KZbinS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 32
@Boaz22
@Boaz22 2 жыл бұрын
Wakwanza ku comment hapa, naomba likes 👍
@thomsanga7956
@thomsanga7956 2 жыл бұрын
so upo hapa kucomment ili upate likes!! 😳😳!!!!????? mzima kweli wewe!!?
@pastorteddywaziri5754
@pastorteddywaziri5754 2 жыл бұрын
Mimi nampendaga huyu baba mheshimiwa Waziri wetu wa habari wa sasa kwa jinsi alivyo very charming.Nilianza kumpenda kupitia video moja hivi alikuwa anaimba wimbo Fulani hivi wa maudhui ya kizamani kwenye events ya wasafi. Ooh yes nimekumbuka ilikuwa ni siku ya mahaba ndindindi ya wasafi.Alikuwa yaani naimba bila maringo kwa unyenyekevu halafu ana sauti natural yaani sauti ilikuwa inatoka TU yenyewe bila kuilazimisha 🔥🔥🔥.Nafikiri alikuwa anaimba Ili kuwaunga mkono vijana na kuwatia moyo Ili waendeleze Sanaa zao. Alinifurahisha Sana kwakweli.Huyu baba namkubali Sana kwakweli 👏👏👏🔥🔥🔥
@kelvinbanoth2161
@kelvinbanoth2161 2 жыл бұрын
Huyu jamaa anaufasaha wa kuzungumza sana na anaufanisi mzuri wa kujib maswali....best interview
@tonymasy8872
@tonymasy8872 2 жыл бұрын
Nsumba secondary schools kumbe we nape ni school mate wangu, duuh it's very joyful
@shebbyhadithi5559
@shebbyhadithi5559 2 жыл бұрын
Salama Demo zinawai, lakini video zinatake long long time kuwa uploaded🙏
@luizabahati5198
@luizabahati5198 2 жыл бұрын
Nice one!..All the best Mhesh Nape ..Baba Jay..kweli leadership ni kazi .Mungu akujalie ukatende kwa utukufu wa Bwana daima
@uwezomabava3949
@uwezomabava3949 2 жыл бұрын
Nakukubali bro
@yusufmohamed8874
@yusufmohamed8874 2 жыл бұрын
I like this guy
@nsajigwamwanjati5119
@nsajigwamwanjati5119 2 жыл бұрын
Salama tuletee Gwajima
@kmnetworktz3473
@kmnetworktz3473 2 жыл бұрын
Imekaa sawa sana hii
@Aidansimwanza
@Aidansimwanza 2 жыл бұрын
Salama ww ni🔥🔥
@zuwenaabdallah7748
@zuwenaabdallah7748 2 жыл бұрын
Huwa nampenda sana huyu kaka yaan niliumiaga kipindi alivyotolewa bastola😪
@halimamasai2234
@halimamasai2234 2 жыл бұрын
Hata mimi nilisikitika sana
@jackhans7708
@jackhans7708 2 жыл бұрын
Kwanza haiitwi luga ni lugha, kiswahili
@mussakhamis2377
@mussakhamis2377 2 жыл бұрын
Big up salama unajua
@sassboy9360
@sassboy9360 2 жыл бұрын
Ndugu Nape 😂😂
@rrchidy6208
@rrchidy6208 2 жыл бұрын
Ya stone town
@valentinetesha8536
@valentinetesha8536 2 жыл бұрын
WABUNGE kumbe wana tabu kweli
@shaiduna
@shaiduna 2 жыл бұрын
Hey momma how are you
@rommelmauma8081
@rommelmauma8081 2 жыл бұрын
Punguzeni matumizi ya Kiingereza, kwa vitendo!
@nicolastitus568
@nicolastitus568 2 жыл бұрын
Sio luga ni rugha kiswahili ni rugha yetu
@abubakarothman2521
@abubakarothman2521 2 жыл бұрын
Lugha na si rugha kama ulivyokosea wewe!
@aminanamoyo83
@aminanamoyo83 2 жыл бұрын
Lugha mpendwa
@japhetkasewa9372
@japhetkasewa9372 2 жыл бұрын
Na sio rugha ni "lugha"
@alexjacobndagile8708
@alexjacobndagile8708 2 жыл бұрын
Wewe umekosea au nawe hujui? Sio rugha Ni lugha nadhani amekosea au ameathirika na matamshi.
@saidnoumani7244
@saidnoumani7244 2 жыл бұрын
Focus zaidi kwenye contents not single work kama lugha au luga
@jackhans7708
@jackhans7708 2 жыл бұрын
Storia yako imeshaandikwa,wewe ni mwizi 2 kama wengine.😡
@alfredmhana235
@alfredmhana235 2 жыл бұрын
Wivu huna point kwa nini usiwe muugwana kakukosea nini
@jackhans7708
@jackhans7708 2 жыл бұрын
@@alfredmhana235 kwa sisi tuliozaliwa kitambo tuwafahamu wezi wa nchi hii.
@lameckmahona2058
@lameckmahona2058 2 жыл бұрын
Ckupend nape mnafk sana,nadhan ulisoma chuo Cha unafki
The FASTEST way to PASS SNACKS! #shorts #mingweirocks
00:36
mingweirocks
Рет қаралды 13 МЛН
ПРИКОЛЫ НАД БРАТОМ #shorts
00:23
Паша Осадчий
Рет қаралды 2,8 МЛН
Mkasi | SO9E16 With Gadna : Extended Version
42:50
MkasiTV
Рет қаралды 61 М.
MSANII |1| mkojani,samofi,chandim,kamugisha
11:08
MKOJANI GANG
Рет қаралды 79 М.
Dr.Samwel Malecela- Maisha Yangu | Maisha Magic Bongo
3:36
Maisha Magic Bongo
Рет қаралды 16 М.
The FASTEST way to PASS SNACKS! #shorts #mingweirocks
00:36
mingweirocks
Рет қаралды 13 МЛН