Salama Na Shilole Ep 5 | MAMA Part 1

  Рет қаралды 235,090

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast #SalamaNaShilole
Listen our Podcast on
Boomplay Link boomplay.lnk.t...
‪Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcasts Link apple.co/2Ou1bru‬
‪KZbin Link bit.ly/KZbinS...
Mama
Zuwena Yusuf Mohammed ndo jina alopewa na wazazi wake na siko hapa kuwakosoa kwa chaguo lao hilo ila mi nadhani Shilole ndo limekaa mahala pake zaidi. Anaongea kama Shilole, anacheka kama Shilole, ni shujaa kama Shilole, REAL kama Shilole, anapenda kama Shilole na sisi tunampenda kama Shilole. Ally Rehmtullah alikua anaadhimisha miaka kumi ya kazi yake. So alifanya auditions kwa ajili ya kuchagua models kuelekea kwenye adhimisho lenyewe, Shilole aka Shishi alikua mmoja wa ma judge wa skuihiyo, picha likaanza hakuwepo popote pa kuweza kuonekana, shuguli ambayo ilichelewa kuanza kutokana na mambo mengine ilibidi pia iendelee bila yeye. Akatokea wakati tunakaribia kabisa kumaliza ila alipofika kila mtu alijua kama Shishi KAWASILI. Vicheko na matani vilitawala na kila mtu akasahau kama hata Shishi alichelewa kufika. Shishi ni ‘special’. Kuanzia muonekano mpaka tabia, jinsi anavyoishi maisha yake na jinsi anavyotafuta na kujiongeza kila siku ni mfano tosha kwetu sote ya kwamba ‘mwenda bure si mkaa bure’
Anaweza pia akawa kafanya yote ili kuweza kutumiza ndoto yake au zake. Kaigiza, kaimba, kaishi kwenye mahusiano ambayo hajivunii kama alishawahi kuishi hivyo, kafanya biashara, kapigana na mengine mengi kapitia ambayo yanaweza kumaliza kurasa, yote kwa yote... Ni mfano wa kuigwa kwa watafutaji na wanaoanza wengi.
Kwenye meza yetu pia alikuja kachelewa, huku akiwa kavurugwa na baadhi ya watu lakini tulipokaa tu kwenye viti yote yalisahaulika na tukajikita zaidi kwenye mazunguzo yetu ambayo yalijaa vicheko, masikitiko, simulizi za kuacha midomo wazi na faraja tele.
Tafadhali enjoy, na chukua mawili matatu ambayo yatakufunza jambo katika safari yako na kukufanya uwe bora zaidi.
Love,
Salama.
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown

Пікірлер: 288
@esterdanford5563
@esterdanford5563 4 жыл бұрын
Shishi....charming soul...nimependa ulivyojisifia na kukuhimiza wasanii wa kike upande wa mziki wajitunze. Hii ni kwa wadada wote ,muhimu kujitunza na kuweka mipaka.Last but one...You are truly beautiful dadaa🤩
@sidval-el5816
@sidval-el5816 4 жыл бұрын
"Mtu mwenye shida unaeza mfanya unavotaka". Bonge la point, "Maskini haaminiki". Show moja nzuri Dada Sally.
@jacquelinesasiyo7915
@jacquelinesasiyo7915 4 жыл бұрын
Kama unapenda kipindi hiki ngonga like twende sawa
@Wanairobi
@Wanairobi 4 жыл бұрын
Inaumiza sana kuona anavyoteswa na mume wake. I love you Shishi and wish you all the best! We need you and your kids need you more.
@lavenderCWTCHEEKS
@lavenderCWTCHEEKS 4 жыл бұрын
"it's okay I am a woman let me do it" words of the great shishi baby! what a strong woman
@neemacharles5135
@neemacharles5135 4 жыл бұрын
Salama hongera sna kwakutuandalia kipindi kizuri mambo yako huwa 🔥🔥💯 kila cku mwenyeze Mungu azidi kukuzidishia uombacho.mwambie shishi tunampenda pia
@latriciah01augustino67
@latriciah01augustino67 4 жыл бұрын
Natamani kungekuwa na voice note ili niwaeleweshe nyie mnaosema shishi nae alimrekodi yule dada wa machungwa aliyemsaidia, ni kweli ndio alimrekodi sio uongo, lakini mnasahau kitu kimoja yule muuza machungwa hakwenda kwa shishi kuomba msaada, hapo ndo ilipo tofauti ya alichoongea shishi na alichofanya shishi kwa dada wa machungwa....! Shishi alimuinua yule Dada pale alipo na kwenda sehemu nyingine (kwa kumuongezea mtaji) Na alifanya kama kushawishi wengine ambao kiukweli wengi wetu tunawalalia sana wale wamama kwa kuomba punguzo wakati hatujui mikiki wanayopitia kupata hiyo 15000 ya beseni moja la matunda,......! hao anaosema shishi ni wale ambae anafatwa na mtu mwenye shida then anamsadia kwa kumrekodi uko ni kudhalilishwa, HIVI MNAELEWA?
@yunaisamir2099
@yunaisamir2099 4 жыл бұрын
Hv una bishana na mbongo haja sikiliza kitu akaki elewa kasha comments anavo jua hata uwa eleweshe vep hawaelew mwengine ndo kaamka hata mswak haja piga ana wenge la usingiz ata elewa wap mada yan me wanan kera kama nn sema ndo uswahili tena
@veronicadaniel1122
@veronicadaniel1122 4 жыл бұрын
Latriciah01 Augustino Asante kunielewesha
@chinamilenas3375
@chinamilenas3375 4 жыл бұрын
Yn bora umejitahidi kuelewesha, mana mi nilishindwa haa, big up
@haimahaima9135
@haimahaima9135 4 жыл бұрын
Waoooo bora umesem ww wengne hawaelew jmn
@Bintimrembo-y1v
@Bintimrembo-y1v 4 жыл бұрын
Haijalishi point ni kwamba unapotoa msaada hutangazi, ni siri yako na Mungu wako.
@alexshallom3094
@alexshallom3094 4 жыл бұрын
SITOCHOKA KUWA SHABIKI WA KIPINDI HIKI, NAENJOY
@azzamahamdu7039
@azzamahamdu7039 4 жыл бұрын
Shishi ni OG comedian.salama umecheka kulko interview zote.
@G.S985
@G.S985 4 жыл бұрын
Strong woman you are Shishi,sipendi zalau ya wanaume!
@brendaa.5222
@brendaa.5222 4 жыл бұрын
My best loved people based in TZ, nawapenda from +254🇰🇪🇰🇪🥰
@luhanyamipawantobi6888
@luhanyamipawantobi6888 4 жыл бұрын
SALAMA mtafute Zuhura yunus kabla hajaenda London Basi!!!
@jessydaktari5209
@jessydaktari5209 4 жыл бұрын
Nice observation🤝🏽🤝🏽
@hawamtambwa402
@hawamtambwa402 4 жыл бұрын
Kabisa
@aimanabbas8542
@aimanabbas8542 4 жыл бұрын
Luhanya Mipawa Ntobi cc’d Es ccccfrfgtty
@leslienakara9890
@leslienakara9890 4 жыл бұрын
una vipindi vya ki LEGEND SANA MTU MZIMA. NAKUFUATILIAGA SANA KITAMBO. una maswali ya kikubwa sana........ big up salama jabiri
@naimamwambe8083
@naimamwambe8083 4 жыл бұрын
Salama hepu naomba siku moja uwe na huyu Dada Sheri mwenye story nzuri kuhusu kazi za ndani Oman wataelemika wengi
@queenseptember4640
@queenseptember4640 4 жыл бұрын
Shishi pole sana kwa tukio la kubakwa, miaka 14 ulikua bado mdogo sana, i can imagine maumivu uliyoyapata, ila nimefurahi kua ulisamehe na maisha yakaenda, inaonesha na wewe ulikua unamkubali, lol.
@asmaahramadhan629
@asmaahramadhan629 4 жыл бұрын
Au altoa ushrikiano cku hiyo
@ibrahimdea2659
@ibrahimdea2659 4 жыл бұрын
Katika interview zote ulizofanya hii bhana ni noma coz dada shishi kafunguka mpaka raha! i realy preciate that
@harounamahoro3436
@harounamahoro3436 4 жыл бұрын
Mi ni mshabiki mkubwa sana wa kipindi hiki from Rwanda...na sitachoka kamwe!
@gradelinemedia6453
@gradelinemedia6453 4 жыл бұрын
U know what i love from u Salama? Unaishi wewe unatenda wewe haufake. Naamini una vitu vingi vikubwa mbeleni. Tuombe tuishi
@zuleikhakhamis3303
@zuleikhakhamis3303 4 жыл бұрын
Salama leo umeishiwa pozi mana ata masuali yamekuishia chezea Shishi baby wewe ana story mpk bac unacheka unahizunika maisha yanaenda na maisha ni kupambana wanawake hakuna kukata tamaa
@tedymwandara5480
@tedymwandara5480 4 жыл бұрын
Yani sisi wanawake tuna akili sana.
@adbellar338
@adbellar338 4 жыл бұрын
@@tedymwandara5480 sanaa. Sisi jembe!!
@infinityfreak6561
@infinityfreak6561 4 жыл бұрын
She is so real.. best interview so far ingekua hata siku nzima haichoshi
@IlhaamMarshed
@IlhaamMarshed 4 жыл бұрын
Halima Rk kzbin.info/www/bejne/fHjLg6yfpNeKZ7s
@rodgernambuta7502
@rodgernambuta7502 4 жыл бұрын
Sijapenda hiyo style ya mike kufunika vitambaa inaonekana kama mnatambika hivi kaah
@beatricetenywa4367
@beatricetenywa4367 4 жыл бұрын
Mdada aliye real asiyefeki,mama ntilie wa Taifa👌💃❣
@IlhaamMarshed
@IlhaamMarshed 4 жыл бұрын
Beatrice Tenywa firigisi za kuku rosti kzbin.info/www/bejne/ppvUgKiobriApJY naomba subscribe tafadhal
@chobydibibi8115
@chobydibibi8115 4 жыл бұрын
Shishi naomba soma comet mm Niko kama ww nawachukia zaidi yako
@kentychristine8539
@kentychristine8539 4 жыл бұрын
She is right though.. Imagine you at the lowest point of your life.. And then someone comes to help u with a camera.. People keep ur cameras at home when helping the need....
@theresiandasuya1849
@theresiandasuya1849 4 жыл бұрын
Sikuwa najua historia yako kabla, pole na hongera sana kwa hatua uliyofikia shishi, nakupenda sana, Mungu ni mkubwa
@musamwambindo2929
@musamwambindo2929 2 жыл бұрын
Very inspiring story.story imenigusa sana.hatufai kukata tamaa wakati Bado tunaishi.
@happinessmagesa3704
@happinessmagesa3704 4 жыл бұрын
Zuena nakupenda sana napenda nyenendo zako San nataman SKU moja tukutane tuongee jambo
@swaumabdi4213
@swaumabdi4213 3 жыл бұрын
Salama ubana nywele umependeza kweli mashallah
@halimaaasaeed8785
@halimaaasaeed8785 4 жыл бұрын
Shi shi nacheka ka mazur unanifurahish we we mchesh mashaallah
@jamilaathumani9004
@jamilaathumani9004 4 жыл бұрын
Story ya shishi inafanana nayakwangu nampaka sasa mwanangu anamiaka 14 Yupo form one
@preciouspeter6126
@preciouspeter6126 4 жыл бұрын
She has a big heart... hongera Shilole
@mtanzaniahalisimungunimwem673
@mtanzaniahalisimungunimwem673 4 жыл бұрын
Salama hongera kwa kazi nzr sana.Nakupenda Sana na Mungu akubariki mno
@leslienakara9890
@leslienakara9890 4 жыл бұрын
umekuwa legend sana mtu mzima....... NEXT LEVEL
@shedrackelia687
@shedrackelia687 4 жыл бұрын
Shishi hii interview imenichelesha kazin
@ibrahimzuberi1029
@ibrahimzuberi1029 4 жыл бұрын
Bonge ya interview, plz tuletee idris,bigbrain pfunk na dj fetty plzplz
@khdigahk4246
@khdigahk4246 4 жыл бұрын
Hii stoli imenigusa mm miezi 7 ndo najua km mjamzito na siku aliotoa bikra na mimba 😭
@dokasalim943
@dokasalim943 4 жыл бұрын
Salama nafatilia sana na nakupenda Sana dadangu udumu katika hii sanaa nakufatilia Sana toka kipindi kile cha nyuma sijaipitwa ata na interview moja.😍😍🇰🇪🇰🇪🇰🇪😍😍
@estermakasi6246
@estermakasi6246 4 жыл бұрын
Nakupenda sana Shilole, mpambanaji superwoman
@said306nyatu9
@said306nyatu9 4 жыл бұрын
Kweli. Shishi. Mzuri. Sana. Mashaallah
@munirasalim148
@munirasalim148 4 жыл бұрын
Shishi bhana mara nyingine usipende ongea huku unakula... Hii hali inakua inaboa flan kuongea huku unatafuta... Yaan mpaka mzuka unakata wa kukusikiliza
@shemsaabdallah3898
@shemsaabdallah3898 4 жыл бұрын
Salama uko juuuuuu unatuwakilisa wa Zanzibar yahstone Towan
@pendohumphrey7588
@pendohumphrey7588 4 жыл бұрын
The story is so touchable😭😭😭
@lindaadhola4514
@lindaadhola4514 4 жыл бұрын
So touching.....sio touchable bro
@Emmy22655
@Emmy22655 4 жыл бұрын
Love u so much my Salama u so beautiful 💞😍💞💞😍really. and vry strong. Joo sauza one day💞💞💞 please Salama
@ashuraomar4935
@ashuraomar4935 4 жыл бұрын
Nakupenda sana Shilole ila japokuwa kweny INTERVIEW kama hizo jaribu sana unapo karibishwa kula ,weka fork chini then zungumza huo ndio ustaarab wa kula ,Salama anatamani amwambie lakini NASHINDWA kukueleza ukweli. Ila mimi nakupenda sanaa Shilole but will tell you what you suppose to know
@lilyjuma2265
@lilyjuma2265 4 жыл бұрын
Mhhhmhhhh da shishi nakupenda lkn kwa hilo hpn ,,heb kumbuk we yule muuza machungwa ulimrekodi ili iwe nn mxeeew kwel muongo hn kumb kumb..
@veronicadaniel1122
@veronicadaniel1122 4 жыл бұрын
Lily Juma Alafu tena yuko siliazi hapo kama cyeye wa machungwa
@kazkaz1943
@kazkaz1943 4 жыл бұрын
ahahaha bongo movie wanasahu harakaaa yan kakauka kama sio yeye alotoa elfu 50
@lilyjuma2265
@lilyjuma2265 4 жыл бұрын
@@veronicadaniel1122 hahahahah
@mariamsiraju5612
@mariamsiraju5612 4 жыл бұрын
@@veronicadaniel1122 jamn mbon yule dada wa machungwa hakutak msaada ila shilole alichokifanya ni kumuunga mkono tuu
@zenamadhan2517
@zenamadhan2517 4 жыл бұрын
Ndio wasanii baadhi yao hujiropokea tuu
@halimasoyomar7289
@halimasoyomar7289 4 жыл бұрын
Shishi nakupenda ukiongea staki. Ata umalize
@huktyasnaty4023
@huktyasnaty4023 4 жыл бұрын
Nampenda shishiii kiukweli napenda mpk maisha yake afek life uyuuu Dada
@vailethamin8439
@vailethamin8439 4 жыл бұрын
leo ww haupo kesho upo😀😀😀
@aliabraj688
@aliabraj688 4 жыл бұрын
Salama jaribu kuwaambia wageni wako wasiongee huwa wanakula huwa wanatukirihisha.
@halimaaasaeed8785
@halimaaasaeed8785 4 жыл бұрын
Shi shi mtam we we nakupend sn ila pole kwa mitihani iyo sio yamoja mm pia imenikuta ila Allah atusaheh
@dianafesto4240
@dianafesto4240 2 жыл бұрын
She's so good mwanamke mpambanaj ❤️❤️❤️
@jumanina446
@jumanina446 4 жыл бұрын
We mwanamke badilisha neno lako la kusema Mungu alivo mbaya
@monicamsemo7577
@monicamsemo7577 4 жыл бұрын
Waooo yani nmejifunzaa sana kupitia shishi good interview nakipenda hichi kipindii mnoo
@hawamtambwa402
@hawamtambwa402 4 жыл бұрын
Nilikuwa nataman sana interview Na huyu Dada Nakupenda Shishi mm nataman siku Moja nikutane Na ww
@hatamimnimempendabulejaman1596
@hatamimnimempendabulejaman1596 4 жыл бұрын
Shishi wengi tunampenda
@hatamimnimempendabulejaman1596
@hatamimnimempendabulejaman1596 4 жыл бұрын
Piko hotel ndo alifanya shangazi yangu
@hatamimnimempendabulejaman1596
@hatamimnimempendabulejaman1596 4 жыл бұрын
Alipata na kazi kabisa. Hata mimi nilisomea hotel walimu walikuwa wananipenda kwel kwasababu nilikuwa naelewa
@hatamimnimempendabulejaman1596
@hatamimnimempendabulejaman1596 4 жыл бұрын
Ndo mana anajuwa kupika vizur
@hatamimnimempendabulejaman1596
@hatamimnimempendabulejaman1596 4 жыл бұрын
Ya tulifundishwa hayo mambo ya wee ni mzur hata mimi nilisemaga
@amriyaaziz2199
@amriyaaziz2199 4 жыл бұрын
Dada ulimpa dada machungwa elfu hamsini tunakumbuka ukamrekodi
@faithmwangosi16
@faithmwangosi16 4 жыл бұрын
Nampenda huyu dada jamani💖
@prosperpuro1712
@prosperpuro1712 4 жыл бұрын
Sema shishi chizi sana 😂😂😂 ndomana nakuelewq sana mama
@abujuhaifah7461
@abujuhaifah7461 4 жыл бұрын
Ah stori hii ya mchezo hakuna lolte shishi kama uongo flani
@elizabethjoseph2116
@elizabethjoseph2116 4 жыл бұрын
Daah shilole ananipa raha sana anavitukoo hahahahaa
@esterdanford5563
@esterdanford5563 4 жыл бұрын
Ehee sorry nimebadilikaa😀😀😀...I loved this part alot na cheko lake kwa mbelee....hehehe....intavyuuu hii na ya Gigy nimecheka sana😅😅😍😍😍
@nurumanyota1957
@nurumanyota1957 4 жыл бұрын
Mungu azidi kukulinda na kukubariki dada zuwena
@MS.independent8934
@MS.independent8934 4 жыл бұрын
shishi ni jasuli kama mm ila mm sija bakwa2 ila ugumu oote aliopitia nikama mm mpaka leo niko na wanangu2 tuu
@jacklinemichael9462
@jacklinemichael9462 4 жыл бұрын
Interview za shishi aziishi hamu kusikilza
@jamilaathumani9004
@jamilaathumani9004 4 жыл бұрын
Nanisingo mama,,, Story zinafafa nayakwangu kabisa,, by the way nampenda Sana shishi nataman nionane nae
@bahajajuma5947
@bahajajuma5947 4 жыл бұрын
Kweli Salama unampenda Shish😍co kwa kufurahi huko😂😂😂!!.....happy life
@IlhaamMarshed
@IlhaamMarshed 4 жыл бұрын
Bahaja Juma firigisi za kuku rosti kzbin.info/www/bejne/ppvUgKiobriApJY naomba subscribe tafadhal
@bahajajuma5947
@bahajajuma5947 4 жыл бұрын
Nishasubscribe
@jaychagagaltv659
@jaychagagaltv659 4 жыл бұрын
Subscribe kwenye KZbin channel yangu BONYEZA hiyo picha kushoto hapo dear
@ufugajitv4749
@ufugajitv4749 4 жыл бұрын
Toka mkasi nimemmic welcome back salama
@fellygal5414
@fellygal5414 4 жыл бұрын
Salama rudia kumuhoji shilole its a nice interview
@hadijasalimu1808
@hadijasalimu1808 4 жыл бұрын
Kwanza naweoenda nyote salama sana nakupenda shichi umeongea ukweli
@jacklinemichael9462
@jacklinemichael9462 4 жыл бұрын
Yaan shilole anajihoj mwenyewe😂😂😂
@Ivy-pn2gc
@Ivy-pn2gc 4 жыл бұрын
Da shishi we unasema manabii wa uongo lkn wewe pia ulimsaidia mdada wa machungwa ukamrecord ...save ur words sometyme
@veronicadaniel1122
@veronicadaniel1122 4 жыл бұрын
Irene Boniventure Kashasahau
@veronicadaniel1122
@veronicadaniel1122 4 жыл бұрын
Irene Boniventure Kashasahau
@kazkaz1943
@kazkaz1943 4 жыл бұрын
Irene Boniventure heheheh kashasahau ndo mana tunaambiwa tusihukumu tusije hukumiwa.
@abdulhamidumiro8236
@abdulhamidumiro8236 4 жыл бұрын
Kbsaaa iseeeeee....
@gloryyairo928
@gloryyairo928 4 жыл бұрын
Alinunuaga machungwa
@carolmuchiri9921
@carolmuchiri9921 4 жыл бұрын
Hata Sasa Shishi Wa Pendeza 👍😘
@hadijasalimu1808
@hadijasalimu1808 4 жыл бұрын
😂😂😂😂😂😂😂😂😂shishi pole yani kama wanieleza mm yalinikuta
@shaniahrachma3114
@shaniahrachma3114 4 жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣🤣🤣salama much love from 254🇰🇪🇰🇪🇰🇪🔥🔥🔥🔥🤣🤣🤣shilole ❤️❤️❤️❤️💕💕💕💕
@bintyk5149
@bintyk5149 4 жыл бұрын
Hakiamungu shishi nakupenda. Natamani cku moja uje Zanzibar tupige picha tu
@estermakasi6246
@estermakasi6246 4 жыл бұрын
iddaty mwinyi hahahah mi mwenyewe nampenda kama nini
@zuleikhakhamis3303
@zuleikhakhamis3303 4 жыл бұрын
Shishi @ vp nimecheka mabaharia sio watu wazuri nimechekaje😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
@husnazaid827
@husnazaid827 4 жыл бұрын
Kaz nzuri da Salama
@atienograce7564
@atienograce7564 4 жыл бұрын
Shilole nakupenda😭😭😭😭😭😭
@agnesbo8812
@agnesbo8812 4 жыл бұрын
Salama eti kama mtama ulivyotokea 😅😅😂😂😂
@saumuhassan6365
@saumuhassan6365 4 жыл бұрын
Nakupenda sana *shishibaby* adi naumwa 😘😍😍😍😍🌹💋
@annatariq5378
@annatariq5378 4 жыл бұрын
Hapo kwenye kuota nimecheka San uwii
@gasanajacques2247
@gasanajacques2247 4 жыл бұрын
am a big fan shishi love from canada yani nakupenda mnoo
@aronnyboy_tz7785
@aronnyboy_tz7785 4 жыл бұрын
Kama unaamin salama alikuwa danger BCC like yako
@sharonkitur5645
@sharonkitur5645 3 жыл бұрын
Shilole you are great! Great interview!
@agnesbo8812
@agnesbo8812 4 жыл бұрын
Shishi Nakupenda eti mimi mzuri 😍😍😍😍😍🤣🤣😜
@Pedeshee01
@Pedeshee01 3 жыл бұрын
Una chura?
@shukurkimat2940
@shukurkimat2940 4 жыл бұрын
Duhuuuu! Msizungumzie imani jamani hii mnajitafutia laana wenyewe acheni maana wote apo akuna anaye juwa BBLIA mwite anaye juwa BBILIA nyie acheni kabisa mnajitafutia laana
@kelvinmissingo4716
@kelvinmissingo4716 4 жыл бұрын
Na ww nabii nn
@veronicamwanyika7226
@veronicamwanyika7226 4 жыл бұрын
Kelvin Missingo wewe ni wa Muhaya wa Maruku?
@jessydaktari5209
@jessydaktari5209 4 жыл бұрын
🔥🔥🔥🔥salama na shishi😚😚😚👌👌👌👌bravoooo
@Emmy22655
@Emmy22655 4 жыл бұрын
And big up chichi love u more 😘💖😍💖😍nakumbuka sauza tulikua pamoja 💞💞💕💞ur vry strong chichi 💞💋💞💋💋💞💋
@zenamadhan2517
@zenamadhan2517 4 жыл бұрын
Lkn dada shishi ulimsaidia mwenye mavhungwa ukamrusha.insta..au ni mm nilielewa vbaya
@zaizai1350
@zaizai1350 4 жыл бұрын
Alafu awo manabii ni malaya kinyama, mtu ad anasuka dred waache kutudanganya bn
@florencebudoya3814
@florencebudoya3814 4 жыл бұрын
What a strong woman,and 🙌👌
@leonadphilibart7703
@leonadphilibart7703 4 жыл бұрын
Hao manabii wanao record huwa ni kitu kitu kimoja na hao wanao wa record matapeli watupu
@khimfarawaytz6910
@khimfarawaytz6910 4 жыл бұрын
Nakupend buree dada yanguu zuwena
@bjzee1981
@bjzee1981 3 жыл бұрын
Nakwambia huyo baharia ninge mtupia jini hata gusa mwanamke mwingine.
@agnessjohn2460
@agnessjohn2460 4 жыл бұрын
Shishi is so priceless ❤
@justdee6086
@justdee6086 4 жыл бұрын
Halafu huyu mdada ana miakili mashallah
@mathasanga4110
@mathasanga4110 4 жыл бұрын
Kweli shilole ni mama la mama, na ni mama lao
@deboramatpapaztv
@deboramatpapaztv 4 жыл бұрын
Salama umehoji vyote nilivyotaka aisee
@yasnaghump5763
@yasnaghump5763 2 жыл бұрын
salama anaangalia umma huo atar
@annasamwel9522
@annasamwel9522 4 жыл бұрын
Miaka Mia nakupenda we ni strong woman
@emmynjeri2478
@emmynjeri2478 4 жыл бұрын
Woow Salama na Shishi pendaaa sana
Salama Na Shilole Ep 5 | MAMA Part 2
25:54
YahStoneTown
Рет қаралды 122 М.
小丑揭穿坏人的阴谋 #小丑 #天使 #shorts
00:35
好人小丑
Рет қаралды 37 МЛН
MY HEIGHT vs MrBEAST CREW 🙈📏
00:22
Celine Dept
Рет қаралды 106 МЛН
КОГДА К БАТЕ ПРИШЕЛ ДРУГ😂#shorts
00:59
BATEK_OFFICIAL
Рет қаралды 6 МЛН
amazing#devil #lilith #funny #shorts
00:15
Devil Lilith
Рет қаралды 18 МЛН
Salama Na Lil Ommy  Ep 1 | Air Tabora Part 1
27:23
YahStoneTown
Рет қаралды 132 М.
Salama Na SUGU Ep 50 | UJIO WA UMRI PART 1
32:38
YahStoneTown
Рет қаралды 110 М.
Salama Na Fid Q Ep 7 | NGOSHA WA MBASA Part 1
29:51
YahStoneTown
Рет қаралды 145 М.
Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1
33:07
YahStoneTown
Рет қаралды 313 М.
Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 1
41:27
YahStoneTown
Рет қаралды 478 М.
Salama Na Baba Levo Ep 26 | ALL IN ALL Part 2
23:11
YahStoneTown
Рет қаралды 228 М.
小丑揭穿坏人的阴谋 #小丑 #天使 #shorts
00:35
好人小丑
Рет қаралды 37 МЛН