Рет қаралды 32,372
Profesa Kithure Kindiki, Aisha Jumwa, Kipchumba Murkomen, Moses Kuria na Justin Muturi ni baadhi ya wandani wa Rais William Ruto waliovuna pakubwa kwenye uteuzi wa leo wa baraza la mawaziri. Majina haya hayakuwa mageni kwenye sura za kampeni za mrengo wa Kenya Kwanza kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita. Na Kama Gatete Njoroge anavyoarifu, wanasiasa hawa ni miongoni mwa wale waliokabidhiwa nyadhifa zenye mamlaka makubwa kwenye serikali ya Rais William Ruto