Hivi nyie mko hapo kuitetea tu simba? Maana nyie mnapenda kuzungumzia tu simba kwa vizuri lakini mazuri ya Young Africans hampendagi kuyapa Uzi to unaostahili hata robo yake. Yanga wafiwa na jambo zuri mnaanza kama mnalizungumzia na ghafla mnageuza kibao na kuanza kuzungumzia simba tena kwa namna ya kufanya lile zuri la Young Africans kiwe halina uzuri wowote. Hivi mbona simba walivyofungwa jana hamkutoa uzito unaostahili tena kwa namna hiyo ya kufungwa, lakini Young Africans walivyotoka safe juzi mlilipigia kelele kwamba kitumbua kimeingia mchango kama vile ni kufungwa. Ifanyeni KiLi FM ipendwe na mashabiki wa club zote siyo wa simba tu. Tafuteni mchambuzi anayependa Young Africans naye ajiunge na ninyi maana nyie hamuwezi kuitendea haki Young Africans