Рет қаралды 1,883
Wakoloni wa Kiingereza walimchukia sana Khalid bin Barghash kwa kuwa walijuwa asingekubaliana na mbinu zao. Siku Khalid alipoamua kurithi kiti cha usultani kutoka kwa Hamed bin Thuwein, ndipo walipoivamia Zanzibar na kuipiga kwa mabomu. Hata alipokimbilia Dar es Salaam, miaka 20 baadaye walimkamata na kumfunga jela kwa miaka 10.