Рет қаралды 4,096
#HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili
Kwa kutambua juhudi zinazofanywa na Chuo cha Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) pia kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni moja ya nchi 10 zinazochangia zaidi vikosi vya ulinzi wa amani, Umoja wa Mataifa umeipa fursa Tanzania kuendesha programu mbalimbali za mafunzo ambapo Chuo cha ulinzi wa amani kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ‘UNITA’ na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Operesheni za Ulinzi waliandaa mpango wa ufundishaji. Katika mahojiano yaliyofanikishwa na Laurean Kiiza wa UNIC Dar es Salaam na Kapteni Mwijage Francis Inyoma wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kusimuliwa na Flora Nducha wa Idhaa hii…Brigedia Jenerali George Itang’are ambaye ni Mkuu wa chuo hicho anaeleza.