Рет қаралды 382
#HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili
Uvuvi usiokuwa endelevu ni tishio kwa sio tu wavuvi bali pia walaji. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, FAO linapigia chepuo uvuvi endelevu kwani limepitisha kanuni za uvuvi huo ambazo pamoja na mambo mengine zinajikita kwenye operesheni zote za uvuvi kuanzia utafiti, uchakataji, biashara na ufugaji wa samaki. Mathalani utafiti kuhusu kiwango cha samaki ziwani au baharini ili kuhakikisha uvuvi endelevu na usioharibu mazingira. Barani Afrika, ziwa Taganyika ni chanzo cha samaki kwa nchi za Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Miaka ya karibuni nchi hizo zimeanza kuchukua hatua za kufunga ziwa, na kwa mwaka huu ziwa hilo limefungwa kuanzia tarehe 15 mwezi Mei hadi 15 mwezi Agosti. Kulikoni? Na Je, nini mtazamo wa wakazi kuhusu hatua hii? Ungana basi na Flora Nducha kwenye makala hii.