Ambwene Mwasongwe - Nimeachilia (Official Music Video)

  Рет қаралды 1,138,421

Ambwene Mwasongwe

Ambwene Mwasongwe

Күн бұрын

Ambwene Mwasongwe presents the Official Music Video for "Nimeachilia"
Maelezo ya wimbo wa Nimeachilia;
Wimbo huu ni wimbo uliobeba hisia za maumivu makali ya usaliti ambayo nimekuwa nikishuhudia kutokana na maisha ya watu...
Wengi wetu tuna doa kama si vidonda moyoni kutoka kwa watu tuliowapenda na kuwaamini sana lakini hawakutulipa imani, upendo na matumaini tuliyokuwa nayo juu yao.
Je! Umewahi kuumizwa na mtu kiasi ukisikia hata jina lake linaitwa unahisi kama bomu la nyuklia limepigwa moyoni mwako?
Kwenye maisha haya watu tuliowatarajia na kuwapenda sana na kutoa kila kitu chetu, moyo, mali, muda, fedha, wakati mwingine hata tumewachangia figo ili waishi.. LAKINI BILA KUTARAJIA WAKATUAMBIA HAWANA FUTURE NASI NA HAWAJISIKII KUENDELEA NASI.
Haya maneno huwa hayatoki haraka moyoni, ni kama kisu kikali kilichokaa motoni kimeiva na kinakata moyo huku kinachoma..... Yanaleta kizunguzungu, kichomi, presha na mawazo mengj...
MIMI NAKUPA POLE KWA LOLOTE ULILOWAHI PITIA KWA MAISHA YAKO... NA KWA KUGUSWA NA MAUMIVU YAKO, MUNGU AMENIPA WIMBO NIKUAMBIAlE SAMEHE NA ACHILIA, MBELE YAKO YAKO MAISHA MENGINE.
Wewe umezungukwa na watu wengi sana wanaokupenda wa kwanza ni #YESU ANAYEKATA KIU YA UPENDO ULIYONAYO, YEYE HAWEZI KUKUAMBIA MANENO KAMA ULIYOAMBIWA..
Wa pili una wazazi wako baba na mama wanakupenda sana mpaka mwisho hawawezi kukukatia tamaa...
wa tatu ndugu zako, dada, kaka, wadogo zako na wengine... majirani na marafiki zako.
KWA NINI UFE NA UUMIE KWA SABABU YA MANENO YA KUUMIZA YA MTU MMOJA NA KWA NINI USIISHI NA KUWA NA FURAHA KWA SABABU YA MANENO YA UPENDO YA NDUGU WENGI NA #YESU AKIWA NA UPENDO MKUU ZAIDI.
NA MWISHO
NIPO MIMI #AMBWENEMWASONGWE NINAYEACHIA WIMBO WA KUKUPONYA KESHO JUMATATU TAR 13 Saa 1:00 usiku. USIKOSE WIMBO HUU #NIMEACHILIA
Kuanzia kesho tutasema kwa njia ya wimbo
Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe: • Ambwene Mwasongwe All ...
Follow Ambwene Mwasongwe
Instagram: / ambwenemwasongwe_
Subscribe to Ambwene Mwasongwe: / @ambweneobadiamwasongwe
Digital Branding & Marketing By:
Black Ozen Entertainment Limited: / blackozenentertainment...
#Nimeachilia #SemaTenaNIMEACHILIA.

Пікірлер: 1 600
@saraphinajohn9112
@saraphinajohn9112 Жыл бұрын
Tuliopona kupitia wimbo huu gonga like hapa mungu akubaliki ambwene🙏
@FurahiniSanga-i4h
@FurahiniSanga-i4h 5 ай бұрын
Nimeachiria kabisa kutoka mume nilie mpenda sana kanitelekezea watoto3na mimba ya4 na kutokujali familia yake kabisa na sasa nimesikia wimbo huu nimeinuka tena nimesamee nimeachiria ee Mungu nisaidie nilee watoto wangu
@happyneithan8438
@happyneithan8438 Ай бұрын
Pole sana. Bwana yesu akawe faraja kwako na watoto wako🙏
@AnethPaul-iw7ro
@AnethPaul-iw7ro 4 күн бұрын
Poleee Mungu akusaidie
@rachaelyusuph8492
@rachaelyusuph8492 Жыл бұрын
Wimbo unaponya maumivu yotee mtu aliyo nayo Moyoni.Mungu akubariki sana Una sehemu yako peke Yako peponi.Hunaga wimbo usio na maana kwenye maisha ya watu umezaliwa kwa Makusudi Libarikiwe Tumbo La mama yako aliyekuzaa🙏🙏🙏🙏
@DavidChangae
@DavidChangae Жыл бұрын
Kabisaaaaa mungu ni mwemaaa
@matthewjames3380
@matthewjames3380 9 ай бұрын
Huu wimbo ulitia moyo Sana wakati nimeachwa kwa mara ya kwanza nauskiliza niliurudia rudi sana kwasababu sku naachwa ndio siku ya kwanza nauskia nikajiuliza kwani huu wimbo nimetungiwa Mimi au!!! nilihakikisha napata namba ya Huyu Muimbaji nikampigia akanitia moyo nikapona Mungu Akuinue Sana Baba yangu @AmbweneMwasongwe
@mercynnko3416
@mercynnko3416 Жыл бұрын
Nimepitia mazito for the past three months I lost my son after three day of delivery mwanaume alinitesa sana nilikua nimesema siwezi pona kutoka kwenye ile experience but Thank God nipo sawa nimepata amani ya moyo baada ya kuachilia kila kitu Mungu Akubariki Ambwene Nice Song
@eliakimulimboka6748
@eliakimulimboka6748 Жыл бұрын
pole sana, MUNGU akupe nguvu na uinuke tena na tena atakuinua sana na atakupa Amani
@jenipheryese378
@jenipheryese378 Жыл бұрын
Waaah pole sana mamaa...Mungu akupe amani ya moyoo
@RmwanashaMbeteRMM
@RmwanashaMbeteRMM Жыл бұрын
Hugs
@mercynnko3416
@mercynnko3416 Жыл бұрын
@@eliakimulimboka6748 Amina
@mercynnko3416
@mercynnko3416 Жыл бұрын
@@jenipheryese378 Asante ubarikiwe
@allenangumbwikewillieson6178
@allenangumbwikewillieson6178 Жыл бұрын
Lyrics!!! Ulipanda mti mzuri ukategemea kuvuna matunda, Ila mti wenyewe umezaa miba na michingoma, Uliwekeza muda na mali ukamwagilia ukitarajia, Matarajio yamekuwa sio sasa umebaki na maumivu, Japokuwa uliiona miba ulijipa muda ukapogolea, Ulitarajia mabadiliko ladba kesho mti utazaa, Sasa imekuwa kinyume mti wako mwenyewe unakuchoma! Unaliaa aaaaaaahh! (Ukimbuka mbegu) Unaliaa aaaaaaahh! (Ukikumbuka maji uliyo mwagilia) Unaliaa aaaaaaahh! (Ukikumbuka kazi uliyo wekeza) Sio kila kinacho kuja kwako ni chako, na si kila kiondokacho kwako ni chako, Hata kama unavipenda sio vyako, Vingine Mungu huviondoa ili wewe ubaki salama, Iwe kazi, nafasi, mahusiano au cheo, Japo vyaondoka kwa maumivu, Ila jifunze kuviacha viende, Nafasi ya moyo wako mpe Mungu. Chochote kile kikuumizacho Kufikia hatua ya kukua, Jua ulikikalisha mahali Pa Mungu! Jifunze kukiacha kiende, Jifunze kusema bye bye, Maana sio vyote vyakwako! Walitoka kwetu hawakuwa wakwetu, Maana wangekuwa wetu wangelikaa nasi, Walitoka ili wafunuliwe sio wote wa kwetu! Walitoka kwetu hawakuwa wa kwetu, Wangekuwa kwetu wangelikaa nasi, Walifunuliwa ili tujue sio wote wa kwetu! Eeeeh! Eeeeh! (Nimeachiliaaaaa) Aaah! jifunze kuuambia moyo wako… (Nimeachiliaaaa) Hata kama inauma sana jifunze kusema… (Nimeachiliaaaa) Eeeh! nimesamehe Mungu anaona mimi, (Nimeachiliaaaa) Tafuta mahali pa pekeyako, Mahali hakuna akuonae, Mahali pa siri pa utulivu, Mahali hakuna akusikiae, Ukakumbuke machungu yako, Maumivu yako na machozi yako, Ukayakumbuke maneno yote, Yakuumizayo moyo wako, Ukakumbuke vitu ulivyo poteza, Kakumbuke muda na watu wa karibu, Kakumbuke hasara uliyo pata, Usiyasahau machungu yoyote, Lia usibakishe machozi, Lia usiyameze yoyote, Toa yanayo uthibu moyo, Toa yasibakie yoyote! (Aaaaah!!! Aaaaah! Aaaaah!) Toa usibaki na machungu, Hakikisha umetuliza moyo, Umesahau yote yaliyo pita, Achilia wote ulio shikilia, Waache waende si riziki yako, Hakikisha umekuwa mwepesi, Ji’editi moyo ubaki salama, Inuka sema kwa ujasiri, Nimeachilia ninaanza upya, Inuka jikung’ute mavumbi, Yakale yamepita sasa ni mapya! Nimeachiliaaa semaa, Nime achi lia!! Nimeesamehe yote, (Nimeeachilia) Nimejinyonyoa manyoya ya kale, Sasa ni mwepesi (Nimeeachiliiia) nimeota mapya, Aaaaah! Aaaaah! Aaaaah! Sasa niko huru, Nina luka luka na maisha mapya, Nimeeachilia (Nimeeachilia) Nimesamehe sasa ninayo amani, Ooh ooh Oooh Maumivu ya kale nimeyaacha nyuma. Nimeeachilia!! Yooow! Nimefunguliwa, nimewekwa huru, nina amani Bwana kaniwezesha!! Yooow! Yooow! Yooow! Sijinyongi tena, sijiui tena! Bwana Yeye ni Bwana wangu wa moyo wangu! Yooow!!
@yonasingooi7458
@yonasingooi7458 Жыл бұрын
@enjoysabuni3635
@enjoysabuni3635 Жыл бұрын
🙏🙏🥰🥰🥰
@barakamwakajumba
@barakamwakajumba Жыл бұрын
Ambwene umebarikiwa Kwa wimbaji napenda wimbaji wako saana yaan tangu nimeanza kusikiliza nyimbo zako nabarikiwa sana nataman siku moja nijekua kama wewe, Mungu aendelee kukubaliki.
@jacksonmrema4737
@jacksonmrema4737 Жыл бұрын
Mungu naomba unisamehe na unisaidie pale mm nilipokuwa sababu ya yeyote kuimba wimbo huu aachilie awe na amani, naomba Umpe nguvu na usimame naye awe imara kama Tai...Na mm nimeachilia kwa Machozi moyo wangu usahau, Mungu naomba Unipe Nguvu. 08 August 2023
@Amina-o7x1h
@Amina-o7x1h 2 ай бұрын
Naombeni like.maana nimejifunza mengi sana
@yohanaagastinymasumbuko8181
@yohanaagastinymasumbuko8181 Жыл бұрын
Jamn ambao tumesubilia kwa ham gonga like bas
@yohanaagastinymasumbuko8181
@yohanaagastinymasumbuko8181 Жыл бұрын
Namshukul mungu man Badi namtegemea ataniinua na mm mana naipenda hii kaz
@dynesssanga1948
@dynesssanga1948 Жыл бұрын
Haleluja nimejifunza kusema byebye
@wilsonemanuel9915
@wilsonemanuel9915 Жыл бұрын
Ulipenda mti mzuri ila siyo chako, Napenda sana kaka nyimbo zako
@wilsonemanuel9915
@wilsonemanuel9915 Жыл бұрын
Na mm nimeachilia
@estamichoromichoro5634
@estamichoromichoro5634 Жыл бұрын
Hata nami naachilia kwa jina la YESU. Naamini kwa neema ya Mungu nitapata mme ambaye yuko sahihi kwangu naomba na kuamini AMINA 🙏
@mfariji
@mfariji Жыл бұрын
Nimelia sana nikiangalia wimbo huu. Hujapitia usaliti, huwezi kujua maumivu yake. Kuachilia ni muhimu lakini sio rahisi kabisa. Mungu atusaidie, tuachilie. Nahisi nahitaji kujifunza kuacha viende, nahisi nahitaji kupata mahali pa peke yangu, mahali pa siri, pa utulivu ambapo hakuta kuwa na anisikiaye, nilie tu, nisamehe yote, nikakumbuke machungu yote, nikayatoe yote, nikaachilie wote walionisibu moyo, nikayatoe machozi yote niweze kusema nimeachilia. MUNGU NISAIDIE.
@beatricekalisti3372
@beatricekalisti3372 Жыл бұрын
Yani nimeusikiliza huu wimbo hadi nimeamua kubadili maisha nimemrudia mungu nilikua sifai kabisa ameen ubarikiwe kaka ambwene🙏
@luizaathanas2904
@luizaathanas2904 Жыл бұрын
Yesu anakupenda ♥️
@josephmusa6990
@josephmusa6990 Жыл бұрын
Amen kagusa huasilia wa maish ya watu
@happylema3801
@happylema3801 Жыл бұрын
Barikiwa
@jacksonygodiwe7417
@jacksonygodiwe7417 Жыл бұрын
huu wimbo Like umeniimbia mimi, Ahsante sana Mtumish wa Mungu, Yesu akutunze sana
@BritPhonce
@BritPhonce 4 ай бұрын
Tuko wengi
@babygwede4982
@babygwede4982 4 ай бұрын
NIMEACHILIA ❤ ASANTE MUNGU KWA UPONYAJI NA KUNIINUA KATIKA MAISHA YANGU NILIHISI NDY MWISHO WANGU, KUMBE MUNGU ULIKUWA NDY UMEANZA KUSHUGULIKA NA MAISHA YANGU VYEMA❤ ASANTE MUNGU WANGU NAKUPENDA ❤ KILA ASOMAE MUNGU AKUPIGANIE AKUTUNZE AKUPE KILA HITAJI WAKO. WEWE NI WA THAMANI SANA MBELE YA MUNGU USIJICHUKULIE POA KABISA
@jaccquelinemakungu1777
@jaccquelinemakungu1777 6 ай бұрын
Huu wimbo naona nimetungiwa Mimi maana nilikuwa naishi kwenye maumivu nashindwa kutoka siku natoka ndio naona wimbo unapigwa duuh si mchezo ku move on na watoto 3. Nimeachilia Sasa I'm so happy nime edit moyo kwa kweli
@janethmabwa1012
@janethmabwa1012 Жыл бұрын
ubarikiwa sana mtumishi ,nimepita kipindi kigumu sana nusura ya kupoteza uhai wangu ,wimbo huu ni kama Mungu amekutumia uutoe wakati huu kwaajili yangu mtumishi ...Amen nimebarikiwa na nimejifunza kua kumbe sio vyote ni vya kwetu na vinavyoondoka kwetu sio vyetu na nafasi ya moyo wangu nimpe Yesu🙏
@wistonbigera989
@wistonbigera989 Жыл бұрын
Pole Sana, trust in God
@afcambassador4566
@afcambassador4566 Жыл бұрын
Pole sana
@anusiatamichael1957
@anusiatamichael1957 Жыл бұрын
Umesema kweli..
@jamesfanuel4595
@jamesfanuel4595 Жыл бұрын
1 Yohana 2:19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
@janethmabwa1012
@janethmabwa1012 Жыл бұрын
@@wistonbigera989 ahsante amina
@cleveraziz1673
@cleveraziz1673 Жыл бұрын
Uuuuu wimbo visa vinafanana na vyangu nimeachiliaa nafasii imebakii kwakoo mungu , gospel upande juuu ihubiriwe injilii
@sharonlivingstone9415
@sharonlivingstone9415 9 ай бұрын
I remember I had pregnant,,lakini jamaa alikata kiukweli nilipata maumivu makali maana ckuwai waza kwamba hili jaribu lingenipata,,after some time due to stress while I was pregnant nilipata shida kiafya nikazaa wakati ambao sio na mtoto hakueweza kusurvive for long,,japo nilikimbiwa huh wimbo utanipa ujasiri wa kusame na kusau na kupata mwanzo mpya,,ubarikiwe sana
@lisserbrown9304
@lisserbrown9304 5 ай бұрын
🫂 dear
@tumainielmaruwa3148
@tumainielmaruwa3148 Жыл бұрын
Huu wimbo umenikumbusha mbali sana alikuja kama mti wa matunda mazuri ila wanadam wakasimama hata wale walikuwa karibu pia wakawa wanafiki kumbe wanalao jambo. Kweli sio Kinachokuja kwako ni chako maana Mungu aweza kuwa na njia zake. Nikweli ukiona jambo lakuuma ujuwe umelikalisha mahali pa Mungu. Yusuf ktk nyumba ya Potifa alipotezwa kwa kumkatalia Boss Mungu akampa muujiza wa Uwaziri Mkuu akitokea gerezani😭😭😭🙏🙏🙏
@mbalilax162
@mbalilax162 Жыл бұрын
It's not just a song, it's a therapy📌
@shadrackwilfred1828
@shadrackwilfred1828 Жыл бұрын
It's very nice song...be blessed brother Ambwene
@kissajaphet2928
@kissajaphet2928 Жыл бұрын
Absolutely true
@siamrema
@siamrema Жыл бұрын
Indeed
@_fizzle
@_fizzle Жыл бұрын
yu said it correctly
@rosemuhandoofficial5676
@rosemuhandoofficial5676 Жыл бұрын
Kakangu ubarikiwe kazi nzuriungu akutunze sana
@berthabraison7979
@berthabraison7979 Жыл бұрын
Umenibariki sana mtumishi nilifiwa na mchumba wangu 😢 sijakaa vzr Mama yangu mzazi sina Baba hatasikuwahi kumuona leo Mama nae Ameniacha nililia nilipousikia Wimbo nililia sikubakiza machozi namshukuru Mungu
@selinagwandu8183
@selinagwandu8183 Жыл бұрын
Pole dear
@JosephatBalikulije
@JosephatBalikulije Жыл бұрын
Mungu ni mwanifu nilifiwa na baba na namiaka 13 na baada ya miaka 6 mama kututoka na nyuma yangu watt wa 5 Mimi nilibaki baba na mama wa wadogo zangu niliumia kupita kawada,wimbo huu wanipa faraja tunashukuru Mungu tuna ishi vyemaa ko wimbo huu uwe faraja kwa wote
@lisserbrown9304
@lisserbrown9304 5 ай бұрын
Hugs 🫂 dear Mungu akupe faraja kuu
@MariaWaYesu
@MariaWaYesu 8 ай бұрын
Ninapitia Wakati Mgumu Sana ambao Sijawahi pitia katika Maisha yangu tongue nizaliwe, YESU nishike Mkono Usiniache, Ukiniacha Ndo mwisho wangu BABA 🙏🙏😭😭😭😭
@RispaNehemia
@RispaNehemia 8 ай бұрын
Pole kipenzi kila kitu kitakaa sawa
@lisserbrown9304
@lisserbrown9304 5 ай бұрын
Hugs dear
@GraceMario-kg2im
@GraceMario-kg2im 3 ай бұрын
Habari rafiki
@Susy0610
@Susy0610 Жыл бұрын
This is what we call Ministry, barikiwa Mtumishi Kwa kweli nimeachilia 🙏🙏
@jiskakablack3402
@jiskakablack3402 Жыл бұрын
Ambwene, kweli vita Yako ni kubwa anayekupambania ni mkubwa Sana. Huu wimbo umepambana ndgu .sijui ilikuwaje ila naamini ubora huu wimbo ni ukubwa wa vita na mzigo ndani Moyo
@deborajoseph5270
@deborajoseph5270 Жыл бұрын
Nimeachilia hata Kama kinauma😭, barikiwe mtumishi
@Susy0610
@Susy0610 Жыл бұрын
Ingawa ni uchungu na inauma, itabidi tuachilie ndio Yesu Kristo akaweza kuponya mioyo yetu. Let go and let God Shalom
@jp.productionpasho6893
@jp.productionpasho6893 Жыл бұрын
How How 7th is 0
@mdoefernandes5442
@mdoefernandes5442 Жыл бұрын
Im Muslim but hii nyimbo haitaji ITIKADI KALI saana kusikilizaa ujumbe mzuri saaana
@gloriousnp
@gloriousnp Жыл бұрын
Ikr 🙏🏿
@emmymwanjala2788
@emmymwanjala2788 Жыл бұрын
Huu wimbo nimeuona live ktk maisha yangu mwaka 2023. Namshkuru Mungu alinivusha salqma ktk kipindi cha msongo wa mawazo. Amina.. nimesamehe Mungu anaona
@eddylava94
@eddylava94 2 ай бұрын
Habar mtumishi ambwene mwasongwe nimekuwa nikiangalia kama umetoa nyimbo mpya lakin hakuna please mm nimmoja wapo ninaependa nyimbo zako toa nyingine tena ikiwezekana album maana napenda sana nyimbo zako
@tukuyufm
@tukuyufm Жыл бұрын
wimbo huu umeshirikisha kila tarajio la fikra zetu, na ndiyo maisha ya kila mmoja, "mtumishi anaimba universal lessons - mafunzo yanayolenga kila mtu duniani. katika umbo la ndani Napendelea sana maudhui ya mguso wa roho unayoifanya ( fikra + utashi wa kuamua mema). Hakika mungu amekupa mbio za akili kwa urefu na upana wa kuzikatiza fikra za jamii kwa nyimbo za FARAJA ZINAZOTIBU MATUMAINI kwa ukubwa nyimbo ulizoimba tunaishi nazo kilasiku zinaachilia bado mienendo mizuri. Mungu akubariki sana namwomba mungu aibariki familia ya mwamlenga kwa kazi njema ya mungu unayoitumikia hapa duniani.
@emmanueljacobo-iy5sf
@emmanueljacobo-iy5sf Жыл бұрын
Hakika
@tukuyufm
@tukuyufm Жыл бұрын
@@emmanueljacobo-iy5sf mfumo wa muziki wa injili unatupa faraja na MATUMAINI yenye uhakika. Tupo hapa duniani tumezingirwa na hali zinazojiri katika miguso ya huzuni, masononeko, chuki, na kujikatia hamu ya kuendelea kuishi. Pamoja na miguso ya furaha, amani na upendo ambapo ndio mahali sahihi pa kuishi kwa macho ya elimu ya nje.
@tukuyufm
@tukuyufm Жыл бұрын
ndugu @@emmanueljacobo-iy5sf tunahitaji sana elimu ya ndani (elimuyaroho) kuzistahimili hali pasipo kujali utegemezi tuliouwekeza awali .
@UweraPeruth-tw2hz
@UweraPeruth-tw2hz Жыл бұрын
huu wimbo ulinigusa moja kwa moja nilipo pitia mambo magumu yakumpoteza my first born wangu 😭😭😭
@eliamwita-leokatikahistori1271
@eliamwita-leokatikahistori1271 Жыл бұрын
Pole sanaaaa
@PaulinaSemindu-ob3de
@PaulinaSemindu-ob3de Жыл бұрын
Pole mpendwa 😭
@UweraPeruth-tw2hz
@UweraPeruth-tw2hz Жыл бұрын
@@eliamwita-leokatikahistori1271 asante sana
@UweraPeruth-tw2hz
@UweraPeruth-tw2hz Жыл бұрын
@@PaulinaSemindu-ob3de asante my dear
@lilianokomba1607
@lilianokomba1607 Жыл бұрын
Nimeurudia huu wimbo almost 100 times. Si shibi kuusikiza. Thank you for using your talent to bless us. Beautifully done.
@preshTzpreshTz553
@preshTzpreshTz553 Жыл бұрын
Nenda Joachim sitaki tena nikufikilie maisha yangu yote hata kama nipo kwenye mji wenu hata nikikuon uwe wa kawaida sana naachalia kila kitu
@chimsmulumbi8937
@chimsmulumbi8937 Жыл бұрын
Ni kama Roho wa Mungu aliniongoza nipate wimbo huu... Two days ago nilifiata hubiri kuhusu Kusamehe, I told to God that I want but sina nguvu ya kuachiliya... Ndipo wimbo huu nikaupata. Kwa hakika nnimehudumiwa n'a Roho wa Mungu kupitiya wimbo huu...
@carlowilly1600
@carlowilly1600 Жыл бұрын
nimeachilia ee bwana kama ni mahusiano n ndoa vtkuja kwa wakat wake
@mercykasyoka4007
@mercykasyoka4007 Жыл бұрын
Mpenzi wangu ndiye amenitumia wimbo huu na anadhani mimi smpendi sasa ameenda naomba mungu amrudishe kwangu kwa utukufu wa Mungu 😢😢😢😢
@chesangfaith3132
@chesangfaith3132 17 күн бұрын
🎉❤ewe mungu nawachilia vyote 2025...nataka kuanza nawe wewe yesu🎉🎉❤
@gotafostv7305
@gotafostv7305 Жыл бұрын
Mtumishi Ambwene nimekuelewa sana baba ,nakujua kuwa ni mtu wa point(hoja) nzito sana zenye fikra na tafakari za rohoni sana ,mimi huwa nasikiliza nyimbo zako kwa umakini mkubwa,neno hata neno ,kwa mfano kwenye huu wimbo nimenukuu neno zito sana ulilosema (NIACHILIE KWAKUWA HAWA WALIOONDOKA WALICHUKUA NAFASI YA MUNGU) ,Kumbe hiyo nafasi ilikuwa akae Mungu ,lakini cha ajabu nilimkaisha huyo mtu,nimeelewa kwakuwa mimi ni moja ya vijana niliyesaidia sana watu wengi sana kumjua Mungu na kuwagharamikia sana,kiasi cha mimi kuishi maisha magumu sana,lakini waliniacha na kuondoka ,aiseeh nimebarikiwa na kuelewa sana ujumbe huu
@zuberinyenzi1982
@zuberinyenzi1982 Жыл бұрын
@@maryemmanuel8462 😳
@maryemmanuel8462
@maryemmanuel8462 Жыл бұрын
Ndugu yangu pole Sana hii simu kunamtu aliishika kwakweli hadi nimeogopa
@kashindiseti4493
@kashindiseti4493 Жыл бұрын
Therapy❤️🙏. Nimeachilia; Jehovah wewe wajuwa❤️🧎‍♀️🙏
@amosizebedayo9190
@amosizebedayo9190 Жыл бұрын
Hakika wote walio niumiza nimeachilia 🙏😌 ubarikiwe Mtumishi Ambwene
@faustinammilla757
@faustinammilla757 Жыл бұрын
Uwiiii nimemuumiza mtu but still nampenda
@farajahalenko924
@farajahalenko924 Жыл бұрын
Amina mtumishi wa bwana,barikiwa sana🙏🙏kwa wimbo mzuri hakika nimebarikiwa sana pia nimejifunza kupitia wimbo huu kuachilia napitia mambo mengi ila mungu akanifunge mkanda kupitia wimbo huu.
@innocensiamwabena3787
@innocensiamwabena3787 Жыл бұрын
Nimebarikiwa mno
@agathasungura5047
@agathasungura5047 Жыл бұрын
Hii nyimbo sichoki kuisikilizaa
@amosizebedayo9190
@amosizebedayo9190 Жыл бұрын
@@agathasungura5047 hakika
@witymazubu2977
@witymazubu2977 Жыл бұрын
2023 huu nilianza vyema lakin katikati ya mwaka nilipitia magumu ambayo nilisema mungu hichi kikombe kwangu kikubwa sana kupoteza nyumba ,kazi ,mume , biashara kuanza moja siyo jambo rahisi tena kwa mara moja ila siku nasikia hi nyimbo nilijipiga kifuwa nikasema nahitaji kuachilia na kushukuru paka leo November 3 nasema mungu asante sana niliachilia ukanipa mwanzo mpya
@anethturinge2472
@anethturinge2472 Жыл бұрын
Nilikua na mwanaume nampenda sanaa lakn aliniumiza sanaa nilikua nafikilia adi kujiuwa lakn kupitia hu wimbo nimejifunza kuachilia sio kilakinacho kuja kwako ni chako balikiwa🙏🏼mtumishi🙏🏼 wa mungu kwakweli nimeachilia sijiuwi tena🙏🏼
@pascallyaruu
@pascallyaruu Жыл бұрын
Kwa huu wimbo kuna jambo inabd niachilie maisha yasonge, siyo kwa Maisha haya aisee,ahsantee Ambwene mwasonge umenifar sanaaaaa sanaaa.Amina mtumishi.
@liannsambu7264
@liannsambu7264 10 ай бұрын
Ila kwenye hii Dunia jamani , hapana hapo ndipo unaona Bora kuwa pekeyako na YESU TU , Maana people mmmmm hapana jamani
@BenedictoMahilane
@BenedictoMahilane Жыл бұрын
Naenda kuachilia kusamehe kutoka moyoni stalia tena nimekusamehe mme wangu nilikubeba moyoni nenda uweda mm sio fungu lako
@EliadaSamson
@EliadaSamson Жыл бұрын
❤❤❤😅😅 😅
@gaspersafari3816
@gaspersafari3816 5 ай бұрын
Huu wimbo unaponya moyo
@florapaschal5727
@florapaschal5727 4 ай бұрын
Amen😭😭ikawe hv na kwang
@zakiaramadhan9657
@zakiaramadhan9657 2 ай бұрын
Asante nimesikiliza kwa rudia rudia wimbo huu mpaka nimepata amani ya moyo ...umenisaidia Sana Asante Sina mengi ya kusema.
@ivvansiwiti9085
@ivvansiwiti9085 Жыл бұрын
AMBWENE WEWE MUIMBAJI WA MFANO NIMEJIFUNZA KUJUA HII 🙏🙏
@sophiakyalo1
@sophiakyalo1 5 ай бұрын
Amen🙏🙏🙏🙏 After suffering for months finally my heart is at peace 🙏🙏🙏🙏🙏 si rahisi but let them go , achilia everything that is hurting you and tormenting you , may we all fine peace
@jovinmwesige8520
@jovinmwesige8520 Жыл бұрын
Ambwene Bwana akutunze,nawe uutunze moyo wako usije ukamwacha Bwana kwa namna yeyote.kama waimbaji wenzako wanavyozidi kumwacha kila siku,ili uendelee kuimba nyimbo zenye Roho wa Mungu ndani yake.Hakika zinatubariki sana.
@frida-oi6kw
@frida-oi6kw 5 ай бұрын
Umewaona wanavyomuacha Mungu??
@neykidoti102
@neykidoti102 Жыл бұрын
Message nzuri sana ubarikiwe mtumishi wa Mungu Ambwene
@apostlejoshuakuhanda5524
@apostlejoshuakuhanda5524 Жыл бұрын
My brother Ambwene. Thank you for this deep message. Your song and the message in it has healed and restored my heart. I'm a new person. I cried out for help and now through this song I realise that the lord God has heard my prayer. May you be more anointed and live long in his presence. Amen Amen Amen
@luizaathanas2904
@luizaathanas2904 Жыл бұрын
Amen get healed 🙏
@mwajumabinwa604
@mwajumabinwa604 Жыл бұрын
nime barikiwa sana na mwibo huu mpaka naurudia kusikia kila nikiweka nyimbo ata nikiwa nafanya kazi nasikia moyowaku unaimba mwibo uhu bila kutarajia 🙏🙏💯💯 Mungu akubariki mtumishi amen.
@DannyMuvunga-cz9zs
@DannyMuvunga-cz9zs 5 ай бұрын
Nduguyangu Ambwene Mungu wa Mbinguni aku tumiye kama chombo kyake kya sifa
@VictorEdison-w5u
@VictorEdison-w5u Жыл бұрын
Jamani ihi nyimbo inaniusu mwanzo mwisho mim kabisa nimeumia Sana mwaka 223 mwanamke nilio mpa kipaumbele kwenye Maisha yangu tena tulipanga nimuoe mwezi wakumi nambili Ila akayavunja mapenzi yangu na kwenda kuolewa na mtu mwengi mwenzi hule hule nilio panga nilipitia magumu sana na nilikata tamaha kwa kila kitu .Ila bado najitia moyo japo muda unazidi kusonga .
@VictorEdison-w5u
@VictorEdison-w5u Жыл бұрын
Nimeachilia 😂😂
@brandymassay2142
@brandymassay2142 Жыл бұрын
I pray everything goes well on your side in Jesus name
@VictorEdison-w5u
@VictorEdison-w5u Жыл бұрын
Thank you brandy
@lisserbrown9304
@lisserbrown9304 5 ай бұрын
Hugs dear Mungu atakupa mwingine wako wa pekee 🫂
@dashconceptz
@dashconceptz Жыл бұрын
100% Ministry When you know the assignment and the One who has called you for His purpose you do not worry about views but you just worry about fulfilling His will. May God remember you man of God
@JoyceChristopher-d9x
@JoyceChristopher-d9x 4 ай бұрын
Nimeachilia na naanza mwanzo mpya machungu yame nifanya niwe karibu na mungu
@MirryKirungi-u2p
@MirryKirungi-u2p Жыл бұрын
Duh ni mara ya kwanza leo nausikiliza huu wimbo nimefiwa na Bibi yangu kipenzi nilikuwa na maumivu makali coz nilimpenda sana Bibi yangu alikuwa zaidi ya rafiki iliniuma sana nimeachilia Asante Kaka ambwene kwa nyimbo hi imenifariji
@TynaRichard
@TynaRichard 9 ай бұрын
Nakupenda Sana huu wimbo unanigusa
@eunicenyaboke86
@eunicenyaboke86 Жыл бұрын
najuwa na nimeamini Mungu uko na sababu na mimi huu wimbo umenipata wakati wa machozi 😭😭wacha nilie yote kisha niwachilie 💔🙌 ahsante mtumishi wa Mungu umenifunza kitu 🙏
@afcambassador4566
@afcambassador4566 Жыл бұрын
Pole
@rusimgoya1449
@rusimgoya1449 Жыл бұрын
Pole san
@witnesmkemwa2562
@witnesmkemwa2562 Жыл бұрын
2023naona umekuwa mwaka wa shetan🙏🙌🙌nilipitia magumu sana😭😭but mapenz Yana changamoto sana🙏🙏ILa nyimbo hii ilinipa moyo sana
@mathewmassawe5982
@mathewmassawe5982 Жыл бұрын
Ameeen!! Nimeachilia,! huyu ndo AMBWENE MWASONGWE! MUNGU akubariki sana kwa ujumbe huu mzuri, MUNGU aendelee kukutunza kwenye huu utumishi wa kumuimbia, uendelee kumuimbia kwa uzuri na utakatifu.
@sophiarichard9592
@sophiarichard9592 Күн бұрын
Kuachilia ni maamuzi magumu inahitajika nguvu ya roho mtakatifu
@tuwenimgohamwende7012
@tuwenimgohamwende7012 2 ай бұрын
MUNGU nakuomba nakuomba,nakuomba,nipe kuachilia nlowabeba moyon mwangu
@SPK450
@SPK450 Жыл бұрын
Ambwene is not only talented, but also blessed I really feel blessed too listening to this song
@esteragustino6141
@esteragustino6141 Жыл бұрын
Amina
@sir_niccobrian
@sir_niccobrian Жыл бұрын
The wait is a finally over Kenyans 🇰🇪🇰🇪leave a Like and show this Great Man Of God love
@joshuaayoub840
@joshuaayoub840 Жыл бұрын
Ni nyimbo ambayo kama vile nilikua naisubiri katika uponyaji wangu wa kuachilia niliyoyashika na yalionitesa kwa mdaa. Ubarikiwe sanaa mtumishi wa bwana. #NIMEACHILIA SASA😢
@SekelaMwakagile
@SekelaMwakagile Жыл бұрын
Be blessed alot son of God
@nebartsanga7890
@nebartsanga7890 Жыл бұрын
Ubarikiwe mtumishi kwakwel umefanyika baraka sana kwa utunzi wa nyimbo zako zote zina tia moyo sana na kufariji saana Najivunia uwepo wako ktk Tanzania yetu Mungu akubariki sanaaa
@jeninyereu5576
@jeninyereu5576 Жыл бұрын
Barikiwa mtumishi wa Mungu binafsi nimeachilia yoooteee
@sarahmmbando2467
@sarahmmbando2467 Жыл бұрын
Ni Mungu tu anajua 😢nimeachilia imeniponya 🙏🏻😭Utukufu kwake aliyeweka huduma hii ndani yako
@surendereka5982
@surendereka5982 Жыл бұрын
Huu wimbo Mungu ameuleta ili useme nami, NIMEACHILIA NA NIMESAMEHE, ninaimani YESU atalejesha yote maradufu🙏🙏🙏🙏🙏
@roseasimwe827
@roseasimwe827 Жыл бұрын
Walitoka kwetu hawakuwa wetu wangekuwa wetu wangekaa kwetu amen, ubarikiwe mtumishi
@siscoministry8400
@siscoministry8400 Жыл бұрын
Mtumishi wa Mungu .... I declare you are the best song writer in Tz....this is healing song...🔥🔥🔥...no one expected ....huu wimbo ni Balaa... Umechana( Rap) 😂🙌🏿🙌🏿🙌🏿..... Walitoka kwetu ,hawakua wa kwetu..wangekua wa kwetu wangelikaa kwetu ..walifunuliwa ili tujue sio wetu 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿, Umebarikiwa Sana Daddy Ambwene Mwasongwe.🤴🏾
@JoyceAmlima-mg4hl
@JoyceAmlima-mg4hl Жыл бұрын
Hiyo Rap from 1 Yohana 2:19 & Ambwene yupo vizuri abarikiwe
@mabulaamos9256
@mabulaamos9256 Жыл бұрын
Kaka napenda unavyopangilia maudhui yako na uimbaji wako, Mwenyezi Mungu azidi kukubariki sana.
@mikenickson6585
@mikenickson6585 Жыл бұрын
Imenichukua takribani miaka 2 lakini baada ya kuskiliza hii nyimbo nimepata mwanzo mpya ......Nimeachilia mimi nimesamehe 😭😭😭ijapokuwa ilikuwa ni ngumu maumivu makali sana lakini leo nimepona
@majormanaseh5668
@majormanaseh5668 Жыл бұрын
"Sio kila kinachokuja kwako ni chako" this part went deep down in me🤲🥹🥹
@gracejoshua6519
@gracejoshua6519 Жыл бұрын
Me too brother
@ipyanakajembula7879
@ipyanakajembula7879 Жыл бұрын
Sure brother
@MariamHassan-j4g
@MariamHassan-j4g 3 ай бұрын
Mungu akubaliki mtumishi maana maumivu ya kumbeba mtu moyoni yamenitesa sana 😢😢😢
@SandrahTumain
@SandrahTumain 3 ай бұрын
Nimeachiliaa .nimesamehe..nimesahau..thanks God🙏 Ma fav song nikiskiliza ni machozii tu yananitokaa
@yustomwaisomania2587
@yustomwaisomania2587 Жыл бұрын
Kuna waombaji Alaf Kuna Ambwene mwasongwe/Mwamlenga🙏🙏🙏 our gifted gospel singer
@RodahAdonice-dz4sm
@RodahAdonice-dz4sm 19 күн бұрын
Kama una mtu ulimuamini sana sana ila akaishia kukusaliti na kugeuka kuwa mwiba wenye makali sana kwako , ni ngumu kuhimili maumivu moyoni ila ukiamua kusimama na BWANA YESU KRISTO yote yanabaki kuwa kumbukumbu tu
@Ngendaruheze
@Ngendaruheze 11 ай бұрын
Moja ya mtumishi wangu bola nchi hii namba Moja wewe
@abelpilato8851
@abelpilato8851 Жыл бұрын
Congratulations mwamba hakika siku zote huwa nasema hujawahi kosea kwenye kazi zako uko full package mtumishi hukurupuki mungu akutunze my brother God is good all the time 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿💛💚💛💪
@eliahjeremiah6487
@eliahjeremiah6487 Жыл бұрын
Hii nilikuwa naipenda since siku ya kwanza naiskia nilikuwa naimba mwenyew ndan kwangu mpaka nalia na nilikuwa sjui kwann na sikuwa najua nini nmeachilia now ni two month toka nilipoamua kubadilisha maisha yangu na leo nmejua kitu gan nilikuwa namaanisha wakati naimba kipind kile😢😢😢😢
@GabrielManyaji-zl2zh
@GabrielManyaji-zl2zh Жыл бұрын
Kaka ambwene kweli unakarama njema San mungu akubariki sana
@juliekahambu7474
@juliekahambu7474 4 ай бұрын
Mungu wezeshe kuachiliya kwani maumivu yamenjaa moyo
@veronicahlusekelo5205
@veronicahlusekelo5205 4 ай бұрын
Amina🙏
@JoyceAmlima-mg4hl
@JoyceAmlima-mg4hl Жыл бұрын
🙏🙏🙏 huu wimbo umenigusa sana ni maisha yangu kabisa.... Ubarikiwe sana ambwene ♥️♥️♥️ nikweli vingine Mungu huviondoa Ili tubaki salama.
@kwilasajunior5367
@kwilasajunior5367 Жыл бұрын
Hiii nyimbo Ina nifikilisha mengi mnoo dah nasijawahi imaliza kusikiliza coz ninameng ya moyon now nachiliaa Niko na amani Asante mungu 🙏🏼
@crisndembwele4016
@crisndembwele4016 Жыл бұрын
😥😥😥Daah umenigusa sana kaka nilikata tamaa niliona km MUNGU anawatu wake nilipoteza Kila nilichotegemea kiwe msaada kwangu mipango yangu yote iliyeyuka 😥😥😥lakini umenifanya nione naweza kuanza upya 🙏🙏🙏 MUNGU akubariki sana kwakutibu mioyo yetu iliyopondeka
@SaraMdoe
@SaraMdoe 8 ай бұрын
Kwa wimbo huu naamini nitavuka maumivu haya maana kwa uwezo wangu siwezi😢
@MariamSanga.
@MariamSanga. Жыл бұрын
😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭thx for the therapy only God knw how much i needed this..🙏
@emmanuelmhina7176
@emmanuelmhina7176 Жыл бұрын
True story about me. Wakati nikitafakari nikakuta mtu mwingine anasononeka Kwa anayoyapitia, rafiki ake akamwambia usilie, sikiliza NIMEACHILIA. Ndipo nami nikajikuta hapa. Naamini lipo suluhisho mbeleni 🙏
@Allyabdalah-oj2wc
@Allyabdalah-oj2wc Жыл бұрын
Asante kwa wimbo mzur nilipousikia tu 2024 nikaingia kwa aman mpaka sasa jaman barikiwa Ambwene
@kwilasajunior5367
@kwilasajunior5367 5 ай бұрын
KUNA NYAKATI TUNAZIPITIA HAKIKA HUU WIMBO UNAKUPONYA KABISA 🎉🎉🎉
@ChobaaB4
@ChobaaB4 10 ай бұрын
Nimeachilia maumivu yote ndan ya moyo wangu
@LawrenceYobuNdosi
@LawrenceYobuNdosi Жыл бұрын
Ubarikiwe mno mtumishi kwa ujumbe na uandishi mzuri wa huu wimbo. Kuna mtu anaponywa moyo wake kwa huu wimbo #lawrencendosi
@angelinaboli-rd5ty
@angelinaboli-rd5ty Жыл бұрын
Nimeachilia🙌
@damodargeita9039
@damodargeita9039 Жыл бұрын
wimbo huu unafundisha sana na unakupa nguvu ya kuanza upya maisha kwa maana tunaishi mara moja na upendo wa kweli upo kwa Mungu pekee. chilia samehe na endelea na maisha kila jambo lina sababu mbele ya mungu lakin wandamu huwa tuko wagumu kuamin na kuruhusu mapenzi ya Mungu.
@nehemiamwashinani1821
@nehemiamwashinani1821 Жыл бұрын
Thank you 🙏 Dear Lord nilisha achilia yote yamepita nashukuru Mungu ulinivusha salama!! 🙏🙏✅
@GlorySimbaya
@GlorySimbaya 17 сағат бұрын
Naachilia yote yaliyoniumiza kwa jina la yesu nafasi ya moyo wangu nampa mungu
@carolinejohn9201
@carolinejohn9201 Жыл бұрын
Kwakweli inatupasa tuachilie ili Mungu Ainue ukuu wake ndani yetu 🙌🏾🙌🏾
@JosephineSamila-uy4cg
@JosephineSamila-uy4cg 10 ай бұрын
Nimeweza kusamehe kupitia wimbo huu Mungu akubariki kaka
@Frednzunda-sl7qn
@Frednzunda-sl7qn Жыл бұрын
Barikiwa sana mtumishi nyimbo zako zinafariji sana maisha ya mtu
@bestchoice383
@bestchoice383 Жыл бұрын
Yani huyu kaka anaimba jamani ...nyimbo zake zinanirudisha sana kwenye uwepo ....God bless you @ ambwene
@bonifacelutumo1196
@bonifacelutumo1196 Жыл бұрын
Huu wimbo umetaja Kila kitu kunihusu Asante yehova Kwa uzima Asante pia Kwa mtumishi
@DivineSoundStudio
@DivineSoundStudio Жыл бұрын
WIMBO HUU UMEWAPONYA WENGI. Ninauhakika kwamba kila aliyefika hapa na kidonda; (Heart Breaks, businesses failure, kugeukiwa na uliyemsaidia, unforgiven burdens and e.t.c) naamini wengi wameachilia mengi, wamesamehe na pia kukubaliana na kauli ilivyo na ku MOVE ON . Ambwene Thanks soo much be blessed wewe sio muimbaji wa kawaida bali wewe ni chombo cha Mungu unatuhudumia sanaa. barikiwa Baba mchungaji. Mafuta ya Mungu yazidi kufurika kwako. Much Love from Kenya.
Israel Mbonyi - Kaa Nami
13:40
Israel Mbonyi
Рет қаралды 8 МЛН
Маусымашар-2023 / Гала-концерт / АТУ қоштасу
1:27:35
Jaidarman OFFICIAL / JCI
Рет қаралды 390 М.
24 Часа в БОУЛИНГЕ !
27:03
A4
Рет қаралды 7 МЛН
SLIDE #shortssprintbrasil
0:31
Natan por Aí
Рет қаралды 49 МЛН
UNAITWA MUNGU  BY ANNE GAHAU [OFFICIAL VIDEO]
6:04
Anne Gachau media
Рет қаралды 101
Nyimbo za Kuabudu na Maombi
1:00:07
Lucas Kaaya
Рет қаралды 771 М.
Ambwene Mwasongwe - Nifundishe Kuomba (Official Music Video)
7:15
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 280 М.
KISA SINA by Japhet Zabron (Official Video)
5:00
Japhet Zabron
Рет қаралды 121 М.
Rehema Simfukwe - Chanzo ( Official Video Lyric)
9:19
Rehema Simfukwe
Рет қаралды 698 М.
Ambwene Mwasongwe - Tumekubalika na Mungu(Official Music Video)
7:17
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 773 М.
Dr.Ipyana - NAWEZAJE KUNYAMAZA//NAMNA HII SIJAONA
15:41
Dr Ipyana
Рет қаралды 3 МЛН
Маусымашар-2023 / Гала-концерт / АТУ қоштасу
1:27:35
Jaidarman OFFICIAL / JCI
Рет қаралды 390 М.